Thursday, 28 November 2013

KCK old skool rap kama hajadaka kazi za hawa majamaa zinapatikana kwangu halafu ni mp3 album ngoma 39 kwa buku 5000 tuh....

VERA SIDIKA ASHINDANA HUYU SHOST KWA MAKALIO MAZURI CHEK MAPICHA HAPA!!!


As we prepare for the big December holidays...once again,
we bring to you the Battle of the Booties....a rare chance
for our audience to vote whose Booty is the most
bootylicious. This month's contest is pitted between the
Sexy "Socialite" and business lady, Vera Sidika and the
current queen of Booty Risper Faith.
To vote for Risper Faith, comment with letter "R" and to
vote for Vera Sidika comment with letter "V"
Best of Best: Risper Faith

PICHA....Amber Rose Baada Ya Zoezi Kali La Kurudisha Mwili Wake....


Baada Ya kujifungua mtoto mzuri wa rapper Wiz Khalifa,
Amber aliingia gym kwa ajili ya mazoezi ya nguvu ya
kurudisha mwili na muonekano wake ukizingatia kazi zake
nyingi zinahitaji muonekano mzuri.
......

TANZANIA..CONGO NA BURUNDI WAUNDA MUUNGANO WAO BAADA YA KUTENGENGWA..


Wakati Kenya, Rwanda na Uganda zimeunda umoja
unaoitwa `Umoja wa Walio Tayari’ , Tanzania, Burundi na
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC ) nazo zimeanzisha
ushirikiano baina yao.
Katika siku za karibuni kumekuwa na mtikisiko ndani ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) baada ya Tanzania na
Burundi kutengwa na wenzao wa Kenya, Rwanda na
Uganda katika baadhi ya masuala muhimu ya ushirikiano
hasa wa kiuchumi.
Tanzania, Burundi na DRC nazo zimekutana ikiwa ni
utekelezaji wa ahadi ya Waziri wa Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Samuel Sitta ambaye aliliambia Bunge lililopita
kuwa Tanzania inafikiria kushirikiana na nchi hizo.
Mkutano wa ujirani mwema
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano
wa Ujirani Mwema uliofanyika mjini Bujumbura, Burundi
jana, Sitta alisema Tanzania, Burundi na Kongo
zimekubaliana kuendeleza miundombinu ya barabara, reli,
anga na usafiri wa maji katika Ziwa Tanganyika.
Alisema mkutano huo ulilenga kuboresha miundombinu ya
usafiri katika Ziwa Tanganyika ambalo linaziunganisha
Burundi Tanzania, DRC na Zambia.
“Pia tumepanga kuendeleza reli ya kati kutoka eneo la
Uvinza, Tanzania hadi Msongati, Burundi na pia
kuunganisha Barabara ya Manyoni - Tabora - Kigoma
kupitia Bujumbura hadi Kivu ya Kusini, DRC, ” alisema Sitta.
Mkutano huo ulihudhuriwa na Sitta pamoja na Waziri wa
Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Burundi, Leontine
Nzeyimana na Waziri wa Uchukuzi wa DRC, Jack Lukeba.
“Pia tulitembelea Bandari ya Kalindo iliyoko katika Ziwa
Tanganyika upande wa Burundi kwani tunataka kuboresha
bandari za ziwa hilo, ” alisema Sitta.
Waziri huyo alisema Tanzania na Burundi zitaunganishwa
na Barabara ya Manyoni – Tabora - Kigoma na Barabara
ya Manyovu - Mgina, Mabanda - Bujumbura
itakayounganishwa mpaka Kivu ya Kusini, DRC.
Kuhusu usafiri wa anga, Sitta alisema nchi hizo zinaangalia
uwezekano wa kuanzisha safari za ndege za Dar es
Salaam mpaka Bujumbura.

MWIGAMBA:SITOKI CHADEMA NA WALA SIOMBI RADHI -ATOA UFAFANUZI KUHUSU WARAKA WA MKAKATI WA MABADILIKO 2013 TAARIFA YA SAMSON MWIGAMBA KWA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU WARAKA WA MKAKATI WA MABADILIKO 2013


Jumatano, 27 Novemba 2013
Jana katika taarifa kwa waandishi wa habari, Mhe.
Tundu Lissu na Mhe. John Mnyika waliudanganya
umma kuhusu waraka unaohusu Mkakati wa
Mabadiliko 2013. Katika maelezo yao
waheshimiwa hawa, pamoja na mambo mengine,
walidai kuwa waraka uliosambazwa kwenye
vyombo mbalimbali vya habari ni feki. Ukweli ni
kwamba:
Ninathibitisha kwamba waraka uliosambazwa
kwenye vyombo mbalimbali vya habari na
mitandao ya kijamii ni sahihi neno kwa neno kama
nilivyousoma katika magazeti ya HabariLeo,
Jamhuri na Rai, pamoja na nakala iliyopo Jamii
Forum. Ili kuthibitisha kwamba waraka ule ndio
wenyewe, nawatumieni ‘soft copy’ kutoka kwenye
kompyuta mpakato (laptop) yangu ambako ndiko
ulikoibwa na viongozi wa chama baada ya
kunipora kwa nguvu laptop yangu Oktoba 25 na
kukaa nayo hadi jioni ya Oktoba 28. Naomba kila
mtu asome neno kwa neno waraka ninaowapa leo
halafu afananishe na ule uliopo kwenye magazeti
na kwenye mtandao ili mjiridhishe kama kweli sio
wenyewe. Kama Lissu na wenzake wana mpango
wa kuuchakachua waraka huu wamekwama!
Waraka huu si wa uhaini wala mapinduzi wala
usaliti kama inavyodaiwa na akina Lissu. Huu ni
waraka wa kusaka ushindi katika uchaguzi halali
ndani ya chama ambao ulikuwa ufanyike Desemba
2013, na ambao sasa umesogezwa mbele.
Napenda ijulikane kwamba wakati wa uchaguzi si
jambo la ajabu kuwa kwa wanachama kuwaunga
mkono wagombea tofauti. Nimekuwa karibu na
Mwenyekiti Mbowe kwa miaka mingi na ninajua
kwamba yeye naye anao mkakati tena
unaohusisha mbinu haramu za kuhakikisha
anammaliza Zitto na yeye kupita bila kupingwa
kwenye uchaguzi huo. Wanaoshiriki mkakati wake
ni pamoja na Lema, Lissu na wakurugenzi kadhaa
waliopo makao makuu.
Waraka huu ulipaswa kuwa siri ndani ya watu
watatu tu (M1, M2 na M3) na haikutarajiwa
kwamba ungevuja kwa jamii. Bahati mbaya
viongozi wa chama baada ya kuunasa waraka huu
kutoka kwenye komputa yangu mpakato (laptop),
na baada ya kikao cha Kamati Kuu, waliamua, kwa
jazba na bila kutumia busara ya kiuongozi,
kuusambaza waraka huo kwenye vyombo vya
habari kwa lengo la kuwakomoa na kuwadhalilisha
waandaji. Sasa baaada ya kugundua madhara ya
waraka huo machoni pa jamii wameamua kuukana.
Ni ajabu kwamba wanaukana waraka ambao
waliusambaza wenyewe.
Nasisitiza kwamba mambo yaliyopo kwenye
waraka ni bayana na dhahiri. Sibahatishi kwa
sababu mimi nimefanya kazi makao makuu kama
Mhasibu Mkuu hadi Mwezi Aprili 2012. Ni kwa
kutambua uozo uliopo katika uongozi wa chama
makao makuu niliona umuhimu wa kubadilisha
uongozi kwa njia za kidemokrasia ili tukiokoe
chama na hatukuwa na nia wala sababu za
kuanika haya yote kwenye umma. Kwa sababu za
chuki na kukosa busara za kiuongozi huyo
anayeitwa Mwanasheria Mkuu akawashauri
viongozi wetu kijinga wauanike waraka mbele ya
macho ya watanzania. Wangekuwa na akili na
busara baada ya yote haya kutokea wangejiuzulu
au kuitisha uchaguzi mara moja.
Tunatambua kwamba viongozi wetu wanamchukia
Mheshimiwa Zitto Kabwe kwa siku nyingi sana na
wametamani kumfukuza siku nyingi. Hata hivyo,
ninawashauri watafute sababu nzuri za kumfukuza
uongozi na hata uanachama kwa sababu yeye
hahusiki na waraka wetu wa Mkakati wa
Mabadiliko 2013 hata chembe, pamoja na kwamba
yeye ndiye alikuwa na bado ndiye mlengwa mkuu,
kama atakubali.

DIAMOND "PICHA ZA ZOEZI LA KUWAFANYIA INTERVIEW WALE WALIOTUMA MAOMBI YA KAZIi


Siku ya jana tulifanya zoezi la kuwafanyia
interview
baadhi ya watu waliotuma maombi yao kwa
mujibu wa ,tangazo la kazi nilillolitoa
juzi,mwitikio
wa watu ulikuwa mkubwa,watu waliotuma
email zao pamoja simu,kiasi ilituwia vigumu
kuwataka wote waje kwenye interview,ilitubidi
tuchague baadhi ya watu ambao tulihisi wanaweza
kukidhi sifa tulizozihitaji ingawa nao pia tulipata
changamoto ya wengi wao kuja pasipo kuzingatia
maelekezo
na maagizo ya tangazo lilivyotaka,hivyo jana
nikishilikiana na wataalamu wa hizo sekta tulisaili
na mwisho wa siku tutachukua wale wenye
viwango
tunavyovihitaji na kuungana na team ya WCB-
WASAFI,.....
Ahsanteni sana.

SHILOLE......SUMA MANAZERETI ANATAFUTA UMAARUFU.


Nakomaa na jiji ndiyo nyimbo yake inayofanya vizuri
katika radio station pamoja television hapa
nchini.Muite Shilole Kiuno ambae pia ni staa wa
tasnia ya bongo movie.
Shilole ambae aliulizwa na Team tizniz juu ya Suma
Mnazaret kuimba katika nyimbo yake
ya Umechelewa aliyoshirikiana ana Richard na katika
wimbo huo suma alisema"Eti umeenda marekani soon
utafanya nyimbo mpya na Jlo kwa muziki gani wewe
umechelewa"Team tizniz ikamuuliza Shilole
anazungumziaje hili?
Shilole alisema"Kijana mdogo huyu anatafuta
umaarufu kupitia watu maarufu kama sisi.Hivyo sina
time ya kumjibu chochote aendelee kujipanga
kivingine.

HII NAYO KALI!!....SUGU AITA SNITCHES WOTE WALIOVULIWA VYEO CHADEMA!!

The A - Z Of An Elderly Husband And Wife Visit Their Doctor When They Begin Forgetting Little Things.


An elderly husband and wife visit their doctor when they
begin forgetting little things. Their doctor tells them that
many people find it useful to write themselves little notes.
When they get home, the wife says, "Dear, will you please
go to the kitchen and get me a dish of ice cream? And
maybe write that down so you won't forget?"
"Nonsense," says the husband, "I can remember a dish of
ice cream."
"Well," says the wife, "I'd also like some strawberries and
whipped cream on it."
"My memory's not all that bad," says the husband. "No
problem -- a dish of ice cream with strawberries and
whipped cream. I don't need to write it down."
He goes into the kitchen; his wife hears pots and pans
banging around. The husband finally emerges from the
kitchen and presents his wife with a plate of bacon and
eggs.
She looks at the plate and asks, "Hey, where's the toast I
asked for?"
DO YOU LOVE THIS POST ? WELL PLEASE SHARE IT WITH
YOUR FRIENDS !

Info Kuhusu Mix Tape Ya Kwanza Ya Songa Kama Solo Artist.


Rapper wa Tamaduni muziki Songa aliyewahi kufanya
mixtape ya kushirikiana na rapper Ghetto Ambassador
amesema yupo tayari kutoa mixtape yake ya kwanza kama
solo artist.
Songa kupitia sammisago.com amesema kuwa Mixtape
itaitwa WAKATI na itatoka tarehe 7 December 2013 kupitia
cd. Producers walioshiriki ni Kalulete, Ray Techno Hammer,
Nikki Mbishi Na One Da Incredible. Wasanii
walioshirikishwa ni Nikki Mbishi, One Da Incredible, P Da
Mc Na Stamina.
Nyimbo zitakuwa 14 zikiwemo Intro na Outro. Midundo
iliyotumika yote imetengenezwa hapa Tanzania na sio
midundo ya Mbele.
Songo ameshawahi kufanya vizuri kupitia nyimbo kama
Chini Ya Ulinzi ft Stamina, Ushauri wa Bure Na Niite Songa.

JB: MLOKOLE MWENYE KICHAA CHA MUZIKI


AKISIKIA muziki unapigwa mahali fulani vinyweleo
humsisimka, kichwa hutingishika na kama yuko
mahali ambako anaweza kujiachia basi lazima
aingie kati kuchangamsha mwili kwa kusakata
rhumba.
Haijalishi ni muziki wa aina gani unapigwa wakati
huo isipokuwa anachoangalia ni mazingira tu.
Ukimpigia Bolingo, R&B, Country, Bongo Fleva zote
zitamkuna. Yote kwa yote mwanamuziki
anayeikonga roho ya JB duniani kote ni Don
Williams.
“Ninapenda kusikiliza na kucheza muziki, lakini
inategemea wakati huo nipo kama nani, nikiwa
kama JB yaani mwigizaji kuna aina ya muziki
huwa napendelea halikadhalika nikiwa Jacob,”
anasema JB.
Anasema kutokana na kazi yake amejikuta akizijua
aina nyingi za muziki na kujiongezea orodha ya
nyimbo katika maktaba yake, lakini hii
haijambadilisha kuwa yule mtu wa kawaida
mwenye chaguo la kipekee.
“Unaniona kwenye majukwaa ya muziki, kumbi za
starehe na kwingineko nikijirusha vilivyo, lakini
huyo ni JB na si Jacob, Jacob anaenda kanisani na
kucheza nyimbo za Injili,” anasema JB.
JB anasema yeye ni mlokole, hivyo katika maisha
ya kawaida hupendelea kusikiliza nyimbo za Injili
kwa kuwa ndivyo imani yake inavyomruhusu.
“Nimeokoka, mara nyingi huwa ninasikiliza nyimbo
za Injili, lakini kwa sababu ninapenda aina
nyingine ya muziki huwa ninasikiliza zile ambazo
zina mafundisho,” anasema JB.
Anasema mbali na kusikiliza nyimbo za Injili, huwa
anapenda kuwasikiliza wanamuziki kama Jose
Chameleon, Ben Pol, Profesa Jay, Lady Jay Dee,
Twanga Pepeta na wengineo wa nyimbo za
kidunia.
“Ninapenda sana muziki, maisha yangu
yametawaliwa na kusikiliza au hata kucheza pale
ninapopata nafasi iwe nyumbani, kanisani hata
kwenye hadhira,” anasema.
Anasema pamoja na kuwa huonekana katika kumbi
za starehe na klabu za usiku, haimaanishi kuwa
anakwenda huko kucheza muziki bali hufanya
hivyo kujifunza mambo mbalimbali.
“Kama utakumbuka kabla ya kutengeneza filamu
yangu ya ‘Senior Bachelor’, nilikuwa naenda sana
klabu, sikwenda kule kufuata muziki ingawa
kiukweli nilikuwa nafurahia, lengo langu lilikuwa
kujifunza namna mapedeshee na madj
wanavyojirusha ili niweze kuicheza nafasi hiyo
vizuri,” anasema JB.
Akizungumzia ujio wake mpya katika filamu,
mwigizaji huyo amesema yupo mbioni kuachia kazi
mfululizo huku akisisitiza kuwa filamu yake mpya
aliyoshirikisha mwanamitindo, Jokate Mwegelo,
itatoka baada ya miezi sita.
“Napigiwa simu nyingi, kila mtu anataka kuiona
filamu aliyocheza Jokate, lakini siwezi kuitoa
mpaka mwezi wa nne mwakani kwani nina kazi
nyingi ambazo inabidi zitoke kwanza,” anasema.
Akizungumzia sababu za kumshirikisha Jokate
katika filamu hiyo iliyopewa jina la ‘Mikono
Salama’, anasema ni kutokana na umbo lake
ambalo lilionekana kuwa lingefaa katika nafasi
hiyo.
“Unajua Jokate ana kaumbo fulani kazuri ambako
unaweza kukachezesha nafasi yoyote, wasanii
wengi wamezeeka kuna nafasi huwezi
kuwachezesha tena,” anamalizia.
-Mwanaspot

RAIS WA MALAWI JOYCE BANDA ASHITAKIWE UMOJA WA NCHI ZA AFRICA


Taasisi isiyo ya kiserikali inayoshughulikia mambo
ya utawala bora na maendeleo nchini (The Center
for Good Governance and Development in Tanzania
-CEGODETA), imeitaka Serikali ya Tanzania
kumshtaki Rais wa Malawi, Joyce Banda Umoja
wa Nchi za Afrika (AU).
Taarifa ya taasisi hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi
Mtendaji wa taasisi hiyo, Thomas Ngawaiya
ilisema uamuzi huo ni kutokana na kauli za dharau
za Banda dhidi ya viongozi wanaoshughulikia
mgogoro wa Ziwa Nyasa.
“Serikali imshtaki kiongozi huyo wa Malawi AU ili
aulizwe ana dhamira gani kwa Tanzania na Afrika
kabla hajaleta madhara makubwa kwa nchi yetu na
Bara zima la Afrika.
Waswahili husema ‘Mchelea mwana kulia hulia
yeye’ na ‘Mdharau mwiba mguu huota tende’,
maana yake ni kuwa inawezekana huyu mtu ana
mtandao mbaya sana tusioujua, tufanye uchunguzi
kuubaini,” inasema taarifa hiyo.
Inasema kuwa, mara tu baada ya kuingia
madarakani Rais Banda alidai kuwa Ziwa Nyasa ni
mali ya Malawi kwa asilimia 100 na Tanzania
haina haki ya kulitumia ziwa hilo kwa njia yoyote
ile.
Taarifa hiyo inasema kuwa, mgogoro huo kwa sasa
uko kwenye jopo la usuluhishi la marais wastaafu
wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa
Afrika (SADC) chini ya Rais Mstaafu, Joachim
Chissano wa Msumbiji.

WARAKA HALISI WA MKAKATI WA MADILIKO 2013 CHADEMA UTATA MTUPU


Utata mkubwa umeibuka kuhusu waraka halisi wa
‘Mkakati wa Mabadiliko 2013’ uliosababisha Zitto
Kabwe kuvuliwa wadhifa wake wa Naibu Katibu
Mkuu wa Chadema na kikao cha Kamati Kuu ya
chama hicho kilichofanyika Novemba 20 - 22,
mwaka huu.
Baada ya juzi, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa
Chadema, John Mnyika kuwaeleza wanahabari
kuwa waraka uliochapishwa katika magazeti na
mitandao ya kijamii, siyo halisi, aliyekuwa
Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha,
Samson Mwigamba amejitokeza na kuutetea huku
akidai kwamba huo unaodaiwa na uongozi kuwa
ndiyo halisi umeghushiwa.
Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini
(Chadema), alivuliwa uongozi pamoja na
aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitila
Mkumbo na Mwigamba kutokana na madai ya
kuandaa waraka huo ambao Chadema kimesema
ulikuwa unaeleza mbinu za uasi za viongozi hao
ambazo zingetumika wakati wa uchaguzi mkuu wa
ndani wa chama hicho jambo ambalo ni kinyume
na katiba, sheria na itifaki zake.
Katika tamko alilotoa jana, Mwigamba alidai
kwamba
kuna njama zinazofanywa na baadhi ya viongozi
wa Chadema ili kuubadili waraka halisi wa
‘Mkakati wa Mabadiliko 2013’ kwa lengo la
kupoteza maana yake, huku akisisitiza kuwa
waraka halisi hauna tatizo lolote.
Katika madai yake, Mnyika alisema waraka huo
unaosambazwa na kuchapishwa, si ule
uliowasilishwa na kujadiliwa katika kikao cha
Kamati Kuu na kuahidi kuutoa waraka halisi ambao
una mambo makubwa na mengi zaidi.
“Waraka utakaotumika katika mashtaka yao siyo
huo. Sisi tutautumia ule ambao uliwasilishwa
katika Kamati Kuu ambao una mambo makubwa na
mengi zaidi kuliko huo unaochapishwa sehemu
mbalimbali, ikibidi tutautoa huo waraka halisi,”
alisema.
Hata hivyo, jana Mwigamba alisema waraka halisi
ni ule ambao upo katika kompyuta mpakato
(Laptop) aliyonyang’anywa na wanachama wa
Chadema, Oktoba 25, mwaka huu, katika mkutano
mjini Arusha.
“Waraka uliosambazwa kwenye vyombo
mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii ni
sahihi neno kwa neno kama nilivyousoma katika
magazeti ya jana (juzi), pamoja na nakala iliyopo
katika mtandao wa kijamii wa Jamii Forums.”
Aliongeza: “Ili kuthibitisha kwamba waraka ule
ndiyo wenyewe, nawatumieni ‘soft copy’ kutoka
kwenye kompyuta yangu kwani waraka huo uliibwa
kutoka katika kompyuta hiyo ambayo nilirudishiwa
baada ya wao kuikagua na kukuta waraka huo
halisi.”
Mwigamba alisema waraka wake unatofautiana
kwa kiasi kikubwa na ule ambao Chadema
kinasema kuwa ndiyo halisi: “Lissu na wenzake
wana mpango wa kuuchakachua waraka huu, lakini
wamekwama.”
Alisema kuandaa waraka huo siyo uhaini kama
ambavyo imekuwa ikielezwa na viongozi wa
Chadema na kusisitiza kuwa ni waraka wa kusaka
ushindi katika uchaguzi halali ndani ya chama
hicho uliopangwa kufanyika Desemba mwaka huu
na baadaye kusogezwa hadi Juni mwakani.
“Wakati wa uchaguzi si ajabu kuwepo kwa
wanachama wanaounga mkono wagombea tofauti.
Nimekuwa karibu na Mwenyekiti wa Chadema,
Freeman Mbowe kwa miaka mingi, najua hata yeye
ana mikakati na wanaoshiriki mkakati wake ni
Lissu na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless
Lema,” alisema.
Alisema anashangazwa kwa kitendo cha Chadema
kuusambaza waraka huo, wakati ulikuwa ni
mpango wa siri kati yake, Dk Kitila pamoja na mtu
mwingine anayetajwa kwa jina la M2.
“Baada ya kugundua madhara ya kusambaza ovyo
waraka huo, sasa wameamua kuukana, waraka
wangu ni sahihi na unaeleza ukweli. Binafsi
nimefanya kazi ofisi ya makao makuu ya chama
kama Mhasibu Mkuu ningeweza kuanika mengi
lakini sijafanya hivyo kwa masilahi ya chama,”
alisema na kuongeza:
“Tunatambua kwamba viongozi wetu wanamchukia
Zitto na tangu siku nyingi walipanga kumfukuza.
Nawashauri watafute sababu nzuri za kumfukuza
uongozi na hata uanachama. Zitto hahusiki na
mkakati huu pamoja na kwamba alikuwa ndiye
mhusika mkuu, alikuwa hajui lolote.”
Jumamosi iliyopita, mama yake mzazi Zitto, Shida
Salum ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya
Chadema alisema waraka huo ulikuwa
umeongezwa maneno.
“Hata ule waraka uliongezwa maneno baada ya
baadhi ya wanachama kumpora Mwigamba
`laptop’ yake alipokuwa mkoani Arusha katika
kikao cha Chadema,” alisema bila kutaka
kufafanua ulibadilishwa vipi, licha ya kuwataja kwa
majina waliohusika kuubadili wakiwamo wabunge
wawili wa chama hicho na viongozi wa ngazi za
juu.
Sitoki Chadema
Kuhusu hatima yake ndani ya Chadema,
Mwigamba alisema hana mpango wa kuondoka
hata baada ya kuvuliwa uongozi, huku akisisitiza
kuwa hakusudii kuomba radhi kutokana na
kuandaa waraka huo.
Alisema hakusudii kuhama kwa kuwa ana historia
ndefu na Chadema na anaamini kuwa ndicho
mkombozi wa Watanzania.
“Nimekuwa kiongozi wa kata, wilaya, mkoa hadi
taifa. Nimetumia muda wangu mwingi na hata
kuhatarisha maisha yangu kwa ajili ya chama hiki,
siwezi kuondoka kutokana na tofauti za
kimitazamo na viongozi wangu,” alisema.
Mwigamba, ambaye alikuwa mfanyakazi katika
Mahakama ya Kimataifa inayosikiliza Kesi za
Mauaji ya Halaiki ya Rwanda (ICTR) na baadaye
kujiondoa ili ajikite kwenye siasa, alisema ana
imani yanayotokea sasa katika chama hicho
yatapita salama.
Mwananchi

KAMA KUNA WANAWAKE WANAO TAKA KUZAA NA MIMI WAJITOKEZE"BABA KANUMBA"


BABA wa marehemu Steven Kanumba, Charles
Kusekwa amefunguka kuwa baada ya kutangaza
kuwa wanawake wanaotaka uzao wake wajitokeze
azae nao, wamejitokeza kumi lakini akawapa
masharti, yakawashinda.
Akizungumza na mwandishi wetu, baba Kanumba
aliweka bayana kuwa warembo hao waliojitokeza
aliwapa sharti la kwenda kupima Ukimwi lakini
ajabu wote waliingia mitini.
“Wamejitokeza vizuri lakini nashangaa wote
wamekuwa wazito katika suala la kupima Ukimwi
wameingia mitini, kama wapo wengine
watakaolimudu sharti hilo, nawakaribisha,” alisema
baba Kanumba

BAADA YA ZITTO KUVULIWA UONGOZI VIJANA CHADEMA WACHAPANA MAKONDE NA KUCHANA BENDERA MKOANI MBEYA


Uamuzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) wa kuwavua nafasi za uongozi vigogo
wake watatu akiwamo aliyekuwa Naibu Katibu
Mkuu, Zitto Kabwe, umepokelewa vibaya na baadhi
ya wafuasi wao ambao wameamua kupigana
ngumi na kuchana bendera za chama hicho.
Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini,
alivuliwa nyadhifa zake sambamba na aliyekuwa
mjumbe wa Kamati Kuu, Dk. Mkumbo Kitila na
aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa
Arusha, Samson Mwigamba.
Kamati Kuu ya chama hicho ilichukua hatua hiyo
Ijumaa iliyopita, baada ya kubaini waraka wa
usaliti waliouandaa ukiibua tuhuma mbalimbali
dhidi ya chama na viongozi wake ngazi ya taifa.
NGUMI ZAPIGWA MBEYA
Kundi la vijana wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa
Zitto jijini Mbeya wanadaiwa kuchana bendera za
chama hicho na kurushiana makonde na viongozi
wa Chadema katika ofisi ya chama hicho Wilaya ya
Mbeya Mjini kwa madai ya kutofautiana msimamo
kuhusiana na uamuzi wa Kamati Kuu.
Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Mbeya Mjini,
David Mwambigija maarufu kwa jina la ‘Mzee wa
Upako’, alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo juzi
mchana.
Mwambigija alisema kuwa chanzo cha vurugu hizo
ni vijana zaidi ya 18 wanaodaiwa kuwa ni wafuasi
wa Zitto kuanza kufanya vikao vya siri mjini
Mbeya kwa nia ya kukihujumu chama.
Alisema uongozi wa chama ngazi ya wilaya
ulipopata taarifa hizo alizodai kuwa ni za
kiintelijensia na kuwa yeye (Mwambigija) ambaye
ni Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya chama hicho
wilaya, aliamua kuwaandikia barua ya kuwaita
ofisini kwa lengo la kuwahoji.
Alisema vijana hao walipofika ofisini kwake huku
wajumbe wa Kamati Tendaji wakiwa tayari
wameketi kwa ajili ya kuwahoji, waliingia ndani ya
ofisi na kulazimisha wahojiwe kwa pamoja badala
ya kuhojiwa mmoja mmoja.
Alisema walipotakiwa watoke nje ili kila mmoja
ahojiwe kwa wakati wake, waligoma na kukataa
kutoka ofisini na ndipo yeye kama Mwenyekiti
alipoamuru kikosi cha ulinzi wa chama hicho
maarufu kwa jina la Red Bridged kuwatoa nje kwa
nguvu na ndipo vurugu hizo zilipoanza.
“Ni kweli kumetokea vurugu kubwa ofisini kwetu
wakati kikao cha kamati ya utendaji kikihitaji
kuwahoji vijana wanaoendesha vikao vya siri
kutaka kukihujumu chama kutokana na uamuzi wa
Kamati Kuu kumvua Zitto madaraka, tumepata
taarifa hizi kwa njia zetu za kiintelijensia kuwa
vijana hawa wapo kwenye kundi la Zitto,” alisema
Mwambigija.
Hata hivyo, Mwambigija alipotakiwa kuonyesha
uthibitisho juu ya tuhuma dhidi ya vijana hao,
alisema kuwa ushahidi bado ni siri kwa vile
wametumia njia zao za kiintelijensia kubaini
mtandao wa vijana hao.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana
Mkoa wa Mbeya, Joseph Kasambala ambaye ni
mmoja wa vijana walioitwa kuhojiwa na kamati ya
utendaji alikanusha madai hayo na kusema kuwa
vurugu hizo hazikuwa na uhusiano hata kidogo na
usaliti wa chama.
Alisema chanzo cha vurugu hizo ni Kamati hiyo
kumuita na kutaka kumuhoji kinyume cha katiba
ya Chadema yeye (Kasambala) ambaye ni kiongozi
wa mkoa, hivyo hawezi kuhojiwa wala
kuwajibishwa na kamati hiyo ambayo ni ngazi ya
wilaya.
Alisema kuwa Katiba ya Chadema inaeleza wazi
kuwa kingozi wa mkoa mamlaka yake ya nidhamu
ni Kamati Kuu ya Chadema Taifa, hivyo kitendo
cha ngazi ya wilaya kumuita na kutaka kumuhoji ni
ukiukwaji wa Katiba.
“Mimi baada ya kupata barua ya kuitwa na
Kamati hiyo ikinieleza kuwa nina tuhuma ambazo
hazikuandikwa kwenye barua waliyoniletea,
nilikwenda ofisini ili nipewe tuhuma zangu kwa
maandishi kama ambavyo Katiba inaelekeza, lakini
nikashangaa eti wanataka wanihoji, nikakataa
walipotaka kunishinikiza vijana wakawajia juu
wakipinga nisidhalilishwe na ndipo vurugu zile
zilipoanza,” alisema Kasambala.

TANGA ILIKUWA HIVI,DAR ES SALAAM KAENI TAYARI KWA MITIKISIKO YA PWANI 2013............!!!

Picha Na Video, Boy Friend Wa Rapper Nicki Minaj Achorwa Tattoo Ya Nicki Mkononi...


Boy Friend wa Rapper Nicki Minaj amesema wayi wengi
hujichora tattoo za watu wasio wafahamu na hata
hawajawahi kukutana nao ila yeye anafanya kitu tofauti
kabisa kwenye mkono wake kwa kuchora tattoo ya baby
mama wake dats Nicki Minaj Baby.
Video akichorwa Tatto na anachosema iko hapa.

JE? WAJUA KWAMBA, KUA NA HIPS AU MAKALIO MAKUBWA....NI ISHARA YA AFYA KITAALAM


Uchunguzi uliofanywa nchini Uingereza umeendelea
kulipandisha chati umbo la kibantu, kwa kusema
kwamba, kuwa na unene zaidi eneo la mapajani,
katika makalio na katika mahips ni vizuri kiafya, na
humzuia mtu asipate matatizo ya kiafya.
Wataalamu wanasema kuwa, mafuta yanayopatikana
katika mahips, huondoa fati asidi mbaya kiafya
ambazo huwa na mada za kuzuia uvimbe ambazo
huifanya mishipa ya damu isizibe. Timu hiyo ya
wachunguzi imesema kuwa, makaliao
makubwa ni bora kuliko mafuta ya zaida
yanayojilundika katika mzunguko wa kiuno, ambayo
hayasaidii chochote.
Wachunguzi hao wamesema katika Jarida la Kimataifa
la Obesiti kwamba, sayansi inapaswa kuangalia jinsi ya
kuongeza mafuta katika eneo la mahips na pengine
katika siku zijazo madaktari watatakiwa kuangalia
njia za kuyahamisha mafuta mwilini na kuyapalekea
katika sehemu za mahips ili kulinda afya za watu
kutokana na magonjwa ya mishipa ya moyo na
magonjwa mengineyo kama kisukari.
Watafiti hao wameeleza kwamba, kuwa na mafuta
kidogo katika hips kunaweza kupelekea matatizo
makubwa ya umetaboli.
Wataalamu hao wameendelea kusema kwamba,
ushahidi unaonyesha kwamba, mafuta yanayozunguka
mapaja na sehemu za nyuma ni vigumu kuyeyuka
kuliko yale yaliyo katika kiuno.
Ingawa suala hilo linaonekama kana kama ni kinyume,
lakini ni kweli kwamba kutoyeyuka huko kuna faida
kwani, wakati mafuta yanapoyeyuka kwa urahisi
hutoa mada inayoitwa cytokines ambayo huleta
uvimbe katika mwili.Mada za cytokines zinahusiana
moja kwa moja na magonjwa ya moyo na kisukari.
Kuyeyuka taratibu kwa mafuta katika mapaja pia
husababisha homoni ya adiponectin izalishwe kwa
wingi na husaidia kudhibiti sukari katika damu na
jinsi mafuta yanavyochomeka.
Dakta Konstantinos Manolopoulos aliyeongoza utafiti
huo kutoka chuo kikuu cha Oxford amesema kuwa, la
muhimu ni umbo na wapi mafuta yanakusanyika, na
kwamba unene wa mahips na mapaja ni mzuri kuliko
unene wa tumbo.

YALIYOMKUTA DIAMOND PLATINUMZ, YAMKUTA MSANII STL TOKA KENYA... UNAJUA NI NINI??...........SOMA HAPA


Kile kilichomkuta msanii diamond hapa tz baada ya ngoma
yake ku-leak kwenye media bila ya permission yake yeye
mwenyewe,kitu hicho hicho kimemtokeamsanii
wa “haba haba” kutoka nchini Kenya ajulikanaye kama
Stela Mwangi aka STL.
Bila ya idhini yake msanii huyo anayehiti  hapa east Africa
na dunia kwa nyimbo kali kama “haba haba” ,yalimkuta
pale ngoma yake iliyo-leak katika media ijulikanayo
kama”Kudinyana” ngoma yenye mashairi makali na
yasiyofaa kwa maadili jamii especially jamii ya ki-
africa,nakufanya fans wake wamjie juu kwa kutopenda
alichoimba katika track hiyo.
Baada ya kushtukia tukio hilo “haba haba”singer huyo
aliamua ku-apologise kwa fans wake kupitia mtandao
wakijamii wa tweeter na kusema kwamba hikuwa lengo lake
kwa nyimbo hiyo kuwa release kwa public na pia
hakumaanisha kile alichokiimba kwenye track hiyo,hata
hivyo baadhi ya mashabiki they don’t buy the apologise na
kufanya aweze kupoteza image yake iliyojengwa kwa
baadhi yamashabiki wake ingawa some fans waliamini
nakumsamehe.
-VIBE

MUME AMUUA MKEWE MWENYE MIMBA YA SIKU 2 AJIFUNGUE KWA KUMPIGA NA MAWE NA MATOFALiI


JESHI la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, linamshikilia
Philemon Ng’ambi, mkazi wa Madale Kata ya Wazo, jijini
Dar es Salaam kwa tuhuma za kumuua mkewe, Enea
Kagine kwa kumshambulia kwa mawe na matofali hadi
kumuua.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Enea Kagine likibebwa na
waombolezaji.
Philemon anadaiwa kufanya unyama huo kwa marehemu
mkewe aliyekuwa amebakiza siku mbili kabla ya
kujivungua usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita
nyumbani kwake Wazo-Hill.
Akisimulia mkasa huo kwa mapaparazi wetu, jirani wa
wanandoa hao aliyejitambulisha kwa jina la Fikiri Rashid
alisema:
“Mimi nyumba yangu na yao zinatazamana hivyo siku ya
tukio majira ya saa tisa usiku, nilianza kumsikia marehemu
akipiga mayowe ya kuomba msaada akisema mumewe
anamuua.
Marehemu Enea Kagine enzi za uhai wake.
“Nilitoka nje kwa lengo la kutaka kutoa msaada lakini
nilihofia maisha yangu hivyo ilinibidi niwaite vijana wa
ulinzi shirikishi ambao baada ya muda walifika eneo la
tukio na kumkuta mtuhumiwa akivunja vyombo vya ndani
kama mtu aliyechanganyikiwa, wakati huo tayari alikuwa
ameshamuua mkewe.
“Baada ya kuwaona ulinzi shirikishi, alikimbilia chumbani
na kwenda kujificha uvunguni kwenye kitanda huku watoto
wao watatu wakiwa wamelala.
Mtuhumiwa wa mauaji hayo, Philemon Ng’ambi.
“Bila kuchelewa, askari wa ulinzi shirikishi walimkamata
na kuwasiliana na Askari wa Kituo cha Polisi cha Wazo
ambao walifika eneo la tukio na kumtia mbaroni
mtuhumiwa pamoja na kuuchukua mwili wa marehemu kwa
ajili ya taratibu za kipolisi,” alisema Fikiri.
Mama mzazi wa marehemu Enea akiwa na simanzi nzito.
Kufuatia tukio hilo la kusikitisha wanahabari wetu walifika
katika Hospitali ya Mwananyamala ulipohifadhiwa mwili
wa mwanamke huyo na mtoto wake waliyemtoa akiwa
amefia tumboni.
Miili hiyo ilizikwa Jumatatu iliyopita (Novemba 25) mwaka
huu katika kaburi moja kwenye Makaburi ya Madale, Dar es
Salaam.

HIVI NDIVYO NILIVYOBAKWA NA MCHUNGAJI WANGU" MTOTO WA MIAKA 12 ATOA USHUHUDA....!!


The girl claimed the pastor of her church, Rhema
Ministries in Oyeagu Abagana in Njikoka Local
Government Area of Anambra State, Rev Sampson Otisi
allegedly lured her to a hotel, under the pretence of
conducting deliverance for her but ended up raping
her all through the night.
Ijeoma, who is said to have hearing problems hearing
claimed she went to the church to seek prayers from
the pastor so that she could hear loudly again.
However, she said she was lured to the hotel and
raped from 9 pm to the next morning and dumped in
the hotel room, where she cried until hotel attendants
rescued her.
Ijeoma who spoke at the Magistrate Court Abagana
said she prayed all night reminding the pastor of the
consequence of his act, but his pleas fell on deaf ears.
The victim came to the court aided as a result of the
injuries she sustained during the alleged act.
According to her, “It started on a Tuesday when I went
to the church for prayers. I have not been hearing
clearly with my ears for sometime, so I went to the
pastor for prayers and when I told him my problem,
he said I should stay behind that he will pray for me
after everyone has gone”.
She continued that, “After the session that day, he
called me to the backyard and started praying for me.
He poured anointing oil into my ear and mouth. He
now ordered me to remove my dress and he poured
some on my tummy and started massaging it. After
sometime, he started putting his hand inside(Vagina),
to which I objected. He said he will leave me if I do
not want him to pray for me”.
Ijeoma narrated that as usual the pastor had asked her
to stay behind, that he will conduct a special prayer for
her and her hearing will be okay again.
“After the service, only he and his friend were left, he
said he will take me to the house and pray for me, but
when I objected and told him that my father will kill
me, he said I should not mind that nothing will happen
to me.
“He took me to a hotel, ran upstairs and came back
and ordered me and his friend to come with him. He
took us up and put his friend in another room and
took me to a separate room. He ordered food for me
and hot drink, to which I objected. He said the drink
was part of the deliverance that I had to drink it. He
forced it down my throat and when I started to feel
sleepy he undressed me and inserted his ‘something’
into me; then he started pushing it in and pushing out.
“Even when blood was gushing out of me, he continued
to push the ‘thing’ inside. I tried shouting but he
covered my mouth, when I could not help myself, I
started praying and telling him of the implication of
what he was doing to me before God but he kept on”.
She said she was only freed the next morning when
she regained consciousness and started banging the
door of the hotel room asking for assistance.
Though Ijeoma said she complained to her mum when
she got back after the first incident, her mum, Mrs
Ifeoma who also spoke to DailyPost said she confronted
the pastor the next day and he denied putting his hand
under the girls pant, claiming he was only praying for
her; a defense which led the gullible woman to accept
that the pastor meant well.
She stated that the truth, however, dawned on her on
the following Tuesday when her daughter went to the
same church and failed to return home.
“I thought she had been kidnapped, in fact I believe
this is also kidnap”, she told our reporter.
A copy of medical report issued to her by the Chief
Medical Officer of Enugu Ukwu General Hospital, Dr
J.O Akuka which her parents showed to our reporter
revealed that she sustained bruises, and a torn hymen.
This showed that there was a penetration in her
vagina.
Ijeoma’s father pleaded with the relevant authorities to
help her find justice for her innocent daughter who
was violated by a man she trusted to be a Man of God,
as the matter is currently before a Magistrate court in
Abagana.
He told our reporter that the pastor had allegedly
offered him N500, 000 to keep sealed lips, an offer he
rejected, but expressed fears that the pastor may use
the money to subvert justice.
The pastor, Rev Otisi, who is the senior pastor of a
branch of Rhema Church in Abagana refused to make
comments when he was approached.
His counsel, Barr CC Achi, however, said that the
matter was only being engineered by unseen hands
from behind as his client occupied a land that is in
dispute.
“The issue here is land dispute, but these people are
being used by someone who is in tussle over a piece of
land with our client. On a separate allegation of being
previously charged with the rape of 8-year-old in his
church, the lawyer said it was not true, adding that it
was meant to paint his client in bad light.

Uanachama wa Zitto Changamoto Ndani ya CHADEMA....Wasira adai dhambi ya Ukabila Itakimaliza Chama Hicho...!!


UANACHAMA wa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa
Chadema, Zitto Kabwe umetajwa kuwa ‘kaa la moto’ kwa
uongozi wa chama hicho hata kabla ya kiongozi huyo
kujibu mashitaka 11 yanayomkabili ili kunusuru
uanachama wake.
Duru za siasa ndani ya chama hicho, zinasema Chadema
haiko tayari kukabiliana na mtikisiko wa Zitto kuvuliwa
uanachama, kwa kuwa hatua ya kuvuliwa madaraka tayari
imegharimu umoja na utulivu wa chama hicho.
Taarifa hizo zinasema kwa sasa kuanzia Kamati Kuu
mpaka wanachama, kuna mpasuko mkubwa ambao namna
pekee ya kuuziba ni kumshawishi Zitto na Mwenyekiti
Freeman Mbowe, kupatana.
Hata hivyo, wakati jitihada za kuwapatanisha zikiendelea,
duru za siasa zinaeleza kuwa kambi ya Mbowe ina
wajumbe wanaoshinikiza kumtosa Zitto na kuwa tayari
kukabiliana na gharama zake.
Majimbo
Mtoa habari wetu kutoka ndani ya Chadema anaeleza kuwa
hofu kubwa iliyopo kama Zitto atanyang’anywa
uanachama, ni ukweli kuwa katika Uchaguzi Mkuu wa
2015, wanaweza kupoteza majimbo mengi na kuipa
mwanya CCM kupita kirahisi.
“Ni kweli huu si mgogoro wa kwanza kwa Chadema na
mara zote viongozi walipovuliwa madaraka kulitokea
mtikisiko, lakini si kama huu wa Zitto… mbaya zaidi,
majimbo ya viongozi tuliowavua madaraka leo hii
yamepokwa na CCM, hatuko tayari kupoteza zaidi,”
alisema mtoa habari huyo ambaye hakuwa tayari kutajwa
jina.
Akitoa mfano, alisema mgogoro kati ya Chadema na Katibu
Mkuu wa zamani Dk Aman Kabourou, ndio ulisababisha
jimbo la Kigoma Mjini lililokuwa moja ya majimbo ya
Chadema, leo hii kukaliwa na CCM.
Mbali na Kigoma Mjini, mtoa habari huyo alikumbushia pia
jimbo la Tarime, alikokuwa Makamu Mwenyekiti, Chacha
Wangwe, ambalo mbali na kushinda katika uchaguzi
mdogo baada ya kifo chake, leo linashikiliwa na CCM.
“Unajua hata kwa Zitto (Kigoma Kaskazini) ukiangalia
kama kweli tukimtosa, sina hakika kama tutarejesha lile
jimbo. Na hata kwa Arfi (Said, Makamu Mwenyekiti
aliyejiuzulu, Mbunge wa Mpanda Kati), kama yule mzee
tukimchezea hatuna chetu,” alisema.
Alipoulizwa afafanue kuhusu mpasuko huo, alikataa na
kuhoji: “Kwani wewe huoni, mbona wenzenu wameandika
mpasuko uliotokea katika Kamati Kuu?”
Mbali na mtoa habari huyo, hata katika waraka unaodaiwa
kusababisha mtafaruku huo ambao Dk Kitilla Mkumbo
alikiri kuuandaa, Chadema imetajwa kuwa na udhaifu wa
kushinda majimbo katika uchaguzi mdogo.
“Tangu uongozi huu uingie madarakani, kumefanyika
uchaguzi mdogo mara nane, lakini tumeshinda mara mbili
tu sawa na asilimia 25,” alisema Dk Mkumbo katika
waraka wake.
Usuluhishi
Pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu
kutangaza kumwandikia Zitto mashitaka yake na kumpa
siku 14 za kujibu, tayari kumeripotiwa kuwa nyuma ya
pazia chama hicho kimeamua kumwangukia Zitto yaishe,
ikiwa ni pamoja na kumwahidi cheo kikubwa kuliko Naibu
Katibu Mkuu.
Kwa mujibu wa taarifa hizo katika uchaguzi mkuu wa
Chadema Juni mwakani, Zitto atashawishiwa kugombea
nafasi ya Makamu Mwenyekiti bila mpinzani au na
mpinzani dhaifu na Mbowe ataachiwa kugombea uenyekiti
bila mpinzani au na mpinzani dhaifu, lengo likiwa
kurejesha umoja wakati wakijiandaa na Uchaguzi Mkuu wa
2015.
Pia inadaiwa Zitto ataahidiwa kupewa fursa ya kugombea
urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa 2020.
Wasira
Akizungumzia mgogoro huo akiwa mkoani Kagera, Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCM, Stephen Wasira, alisema anajivuna
kwamba ndani ya chama chake hakuna ubaguzi kama
ilivyo katika vyama vingine vya upinzani a mbavyo alidai
kiongozi wa ngazi ya juu lazima atoke kabila fulani.
Alidai katika baadhi ya vyama, ikitokea mtu ametoka kabila
tofauti akataka kugombea uongozi ngazi ya juu, kunazuka
vurugu na kufukuzana kwa visingizio vya kuvunja katiba za
vyama hivyo.
“Mara nyingi huwa natumia kauli ya Mwalimu Julius
Nyerere kuwa ubaguzi ni sawa na kula nyama ya mtu,
ukiishaionja huiachi kwa hiyo wameionja inawatafuna.
“CCM hatuna sababu ya kushangilia matatizo yao na
hatuwaogopi wala hatutaki upinzani ufe, kwa sababu
upinzani ni mfumo ulio ndani ya nchi, ila nasi tuache
makundi yanayotokana na uchaguzi, ili tuendelee kushika
Dola kama ilivyo ada yetu,” alisema Wasira.
Vyuo vikuu
Baadhi ya wanachama wa Chadema, wakiwamo wanafunzi
wa vyuo vikuu, walikutana Dar es Salaam jana na
kutangaza mgogoro wa kiutawala kati ya wapigania
demokrasia ndani ya chama hicho na wahafidhina.
Wanachama hao waasi ambao walisema ni wapigania
demokrasia ndani ya chama hicho; lakini kwa tafsiri ya
viongozi wa Chadema ni ‘wahaini’, wametangaza
kuzunguka nchi nzima kuhamasisha wanachama wa
chama hicho wakatae baadhi ya watu waliopandikizwa
kwa kukaimishwa nafasi za uenyekiti kwa manufaa ya
wahafidhina.
Baadhi ya wanachama hao wakiongozwa na Greyson
Nyakarungu, walidai wanatambua kuwa mgogoro ndani ya
Chadema umetokana na Mwenyekiti Mbowe kutamani
kuendelea kuongoza chama kwa gharama yoyote.
Nyakarungu alidai Mbowe anatamani aendelee kutawala
hivyo kuzunguka katika baadhi ya mikoa na kuwaondoa
katika nafasi zao viongozi waliochaguliwa kidemokrasia,
ambao wanaonekana kutomwunga mkono kwa kisingizio
cha kutowajibika.
Nyakarungu ambaye alijiita Brigedia wa Uasi huo, alisema
watu wote waliopenyezwa kukaimu nafasi hizo za uongozi
mikoani wajiondoe haraka “kabla hatujawaondoa kwa
nguvu.
“Sisi tumeamua kama tulivyozunguka nchi nzima na
kampeni ya Washa Taa Mchana, tutazunguka nchi nzima
kuwaambia wanachama ubovu huu wa wahafidhina.
“Tunamwonya Zitto na Dk Mkumbo tabia zao za kusema
kuwa wanaheshimu uamuzi wa CC huku wakijua ni nini
kitatokea, waache mara moja, kwani unyonge wa aina hii ni
kuendelea kuruhusu baadhi ya watu kupora rasilimali za
chama,” alidai Nyakarungu.
Nyakarungu, Jeremia Fumbe wa Chuo Kikuu cha Ardhi na
Likapo Bakari ambaye alifukuzwa Chuo Kikuu cha Dodoma,
walisema wao ni majeruhi wa kufinyangwa kwa
demokrasia ndani ya chama hicho, na kila hoja ambayo
wanatoa wamekuwa wanaitwa masalia ya Zitto.
Nyakarungu alisema watu wote wanaoitwa wasaliti ndani
ya chama hicho au ‘wanaotumwa na CCM’ hoja yao
imekuwa moja tu ya matumizi ya fedha za chama hicho,
hoja ambayo pia walidai imemgharimu Zitto.
“Tunafikia hatua wahafidhina wanasema wazi kuwa ni
bora chama kishuke daraja kuliko kupewa mtu wa nje, mtu
wa kuja, mtu wasiyemfahamu,” alisema Nyakarungu na
kusisitiza kuwa wanachama wa Chadema kutoka Mara na
Kigoma ndio wamekuwa wahanga zaidi.
Nyakarungu, ambaye alidai alijiunga na chama hicho
mwaka 2005 na kushiriki kujenga, alisema kilichomponza
Zitto ndani ya chama hicho ni kuhoji matumizi ya chama
hicho kupitia kamati ya Bunge ya PAC, ndio maana
alishambuliwa yeye binafsi wakati huo ulikuwa uamuzi wa
Kamati ya Bunge.
“Viongozi wetu wa Chadema wanahoji Serikali na matumizi
ya fedha za walipa kodi wakitaka uwazi na usawa, leo
wanataka kutonywa mapema ili wafanye marekebisho ya
kuficha uovu wa matumizi ya pesa? “Zitto kama kiongozi
anayejipambanua asingeweza kuwatonya ili wafiche uchafu
katika matumizi ya fedha huku akitengeneza nafasi ya
kuumiza vyama vingine, hii ni dalili ya udikteta. Na kwa
kuwa aligusa mkia wa mfalme nge ni lazima ang’atwe,”
alidai Nyakarungu.
-Habari leo

JACKLINE WOLPER "ALIKIBA NDIYE ALIYENITOA USICHANA WANGU",SIWEZI KUMSAHAU KAMWE...!!!....


MOYO;
huhifadhi mengi mazito hasa ya kuumiza! Staa mkubwa wa
sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe amejikuta
akimwaga machozi wakati akianika siri tano nzito kuhusu
mapenzi katika mahojiano (exclusive interview)
Katika ‘intavyu’ hiyo iliyofanyika Jumatatu iliyopita kwenye
Ofisi za Global Publishers, Bamaga-Mwenge jijini Dar
kuanzia saa 8:44 alasiri hadi saa 10:44 jioni, Wolper
alifunguka vitu vingi.
KISA/MKASA
Akizungumza kwa masikitiko, uchungu na majuto, Wolper
alisema hawezi kumsahau mwanaume huyo ambaye ni
Abdallah Mtoro ‘Dallas’ kwa namna alivyomwingia kijanja
na kutaka kumvunjia heshima aliyoijenga karibia miaka
kumi nyuma.
ALIANZIA WAPI NA DALLAS?
“Siku ya kwanza Dallas alinipigia simu na kuniambia
aliniona Magomeni (Dar). Naikumbuka sana siku hiyo,
ilikuwa baada ya mizunguko yangu, mwanzoni sikupokea
simu yake kwa sababu ilikuwa namba ngeni kwangu.
“Nilimsikiliza sana. Jamani yule mwanaume anaongea kwa
ushawishi wa hali ya juu mno. Nilishangaa aliponieleza
kila kitu kuhusu familia yangu na nyumbani kwetu. Kumbe
tayari alishaunda urafiki na baba yangu (mzee Massawe).
“Mwanzoni nilidhani ni tapeli. Nikamkatia simu.
Akaendelea kunipigia na nilipoona imekuwa kero kubwa
nilipokea. Ili kuthibitisha anawajua wazazi wangu,
alinitajia namba zao za simu ambazo ni za kweli.
“Pamoja na hilo nilimfanyia nyodo, si unajua mtoto wa
kike? Lakini aliniongelesha kwa upole hadi nikapunguza
nyodo zangu.
“Aliniuliza nataka anifungulie biashara gani. Nikamwambia
biashara ya nguo. Akaniuliza nataka mtaji kiasi gani.
nikamwambia dola laki moja kwa sababu nilikuwa sitaki
fremu moja, nilitaka nyumba nzima. Akaniambia hakuna
tatizo.
“Pia aliniuliza naishi wapi? Nikamwambia Sinza (Dar)
alionesha dharau kwenye simu akaniambia atanihamishia
Mbezi Beach.
“Aliniuliza natembelea gari gani? Nikamwambia Toyota
Noah. Akaniambia ningependa aninunulie gari gani?
Nikamjibu Toyota Discovery lakini yeye akasema
ataninunulia Toyota Harrier.
“Kweli baada ya siku mbili-tatu nililetewa Toyota Harrier
nyeusi nyumbani. Niliogopa isijekuwa mtego nikaingia
kwenye matatizo hivyo nilimzungusha mtu aliyeniletea
hadi Sinza-Mori nikamwambia apaki kwenye kituo cha
teksi, nikaenda na dereva nikalichukua hadharani ili lolote
likitokea nipate msaada.
“Nilikabidhiwa funguo za lile gari na documents zake,
nikaondoka nalo hadi nyumbani kwangu. Kesho yake
Dallas alimtuma mtu aniletee dola za Kimarekani 15,000
(zaidi ya Sh. milioni 24). Nilipouliza za nini aliniambia ni
kwa ajili ya shopping ya kutembelea Harrier niachane na
zile swaga za kwenye Noah (fedha inaongea). Kisha
akanitumia cheni ya dhahabu.
“Siku iliyofuata alinitumia Sh. milioni 15 nipeleke nyumbani
nikawaambie wazazi nimepata mchumba ambaye
angeenda kujitambulisha baadaye. Niliwaambia ni Dallas
ambaye walikiri kumfahamu kwa sababu alishawapigia
simu na kujitambulisha kuwa ni mkwe wao.”
AMESHAKUTANA NA DALLAS?
“Hadi hapo nilikuwa sijamuona Dallas kwa sura na fedha
nilikuwa natumiwa kila siku.
“Wakati hayo yakiendelea akaagiza nihamishiwe Mbezi
Beach na kununuliwa lile gari lililoibua mzozo BMW X6.
“Nakumbuka siku niliyokabidhiwa lile gari nililia sana.
Sikuamini macho yangu kwa sababu Dallas aliniambia
amenitumia kazawadi kumbe ni BMW X6 (lina stori ndefu
inakuja)!
“Kumbuka mwanzoni nilikuwa na boyfriend ambaye
tulipendana sana lakini hatukupanga kufunga ndoa.
Nilimweleza kila kitu akakubaliana na mimi japokuwa
aliumia.
“Maskini! Kuanzia hapo nikawa nimeachana na yule
boyfriend wangu lakini hakukuwa na namna kwa sababu
niliamini nimepata mchumba wa kunioa.
ATAKIWA KUBADILI DINI
“Baadaye Dallas aliniambia nimeshakuwa mchumba wake
hivyo nibadili dini. Kweli nilibadili nikawa Muislam na jina
langu likawa Ilham. Hicho kilikuwa kipindi kigumu sana
maishani mwangu kwa sababu nilionekana ni muasi katika
dini yangu ambayo mama ni mzee wa usharika na mwimba
kwaya, baba ni mtu wa kanisani sana.”
NINI KILIFUATA?
“Siku moja nilikuwa Tanga nashuti filamu, nilikuwa nikitoka
hapo niende Morogoro. Dallas alinipigia simu akaniambia
yupo Nairobi (Kenya) anakuja Tanzania. Nilimwambia nipo
Tanga akaniambia atanifuata kule. “Niliendelea kupiga
mzigo. Zilipita saa nyingi, baadaye nikiwa na kruu yangu,
Dallas alinipigia simu akaniambia ameniona.
“Nilikataa, akaniambia namna nilivyo, nguo nilizovaa na
watu niliokuwa nao, alipatia. Kumbe alikuja na Toyota
Prado.
WOLPER MORO, DALLAS DAR
“Tulipomaliza kurekodi Tanga tulikwenda Morogoro, yeye
aliniambia anaelekea Dar. Tulikuwa tunawasiliana.
Nilipomaliza kurekodi Moro nilirejea Dar. Hapo ndipo
vituko vikawa juu ya vituko.
“Niliambiwa mara kaonekana sehemu akiwa na mwanamke
au wanawake. Mimi sikujali kwa sababu nilipomuuliza
aliniambia hatuwezi kuonana kwa sababu kipindi hicho
alikuwa katika swaumu hivyo akionana na mimi
nitamharibia. (ulikuwa mwezi mtukufu).
BADO HAWAJAKUTANA?
“(Mguno) Hapo bado hatujakutana lakini yupo mjini na
amejaa tele kwenye kumbi za starehe.
“Baada ya kumaliza swaumu, siku moja aliniambia anakuja
nyumbani Mbezi Beach. Niliwaalika marafiki zangu
tukapika vyakula, tukafanya usafi na kufukiza udi
chumbani. Nilitandika mashuka meupe kitandani na
kujipara kisha nikavaa ushungi kuanzia mchana nikakaa
kama malkia nikimsubiri mchumba.
“Huwezi amini, hadi giza linaingia Dallas hakutia mguu.
Nilipataje aibu kwa rafiki zangu waliotaka kumuona huyo
mchumba? Ninyi acheni tu!
“Nilipomuuliza aliniambia alipata dharura kuna biashara
alikuwa anafanya
HATIMAYE WAKUTANA LAKINI…
“Nilikasirika sana, nikasema huyu ni mchumba gani
asiyetaka kuja kwangu? Nikampa muda wa siku tatu aje
nyumbani na alete nguo zake zote. Kweli, siku ya tatu,
asubuhi nilimsikia mtu akiita ‘Ilham Wolper Dallas’.
Nilishajua sauti yake kupitia simu hivyo nilimkaribisha na
nguo zake nikaingiza ndani. Lakini cha kushangaza alikuja
na pikipiki!
“Alishinda nyumbani siku hiyo maana kuna ndugu zake
walikuja. Hatukufanya chochote. Dallas aliishia kunibusu
shavuni kisha jioni akaondoka.
“Mjini kukawa hakukaliki. Natumiwa picha akiwa na
wanawake tofautitofauti. Mmoja wa wanawake hao
niliambiwa eti ana ‘ngoma’! Jamani hii dunia ina kichaa!
“Muda ukasonga, vitimbi vikawa vingi. Dallas simuoni.
Muda wa kukaa kwenye ile nyumba uliisha hivyo nikahama
na nikamwambia akachukue nguo zake.
UCHUMBA WAVUNJIKA, SASA ANAPUMZIKA HAPA
“Baadaye uchumba ukavunjika tena mimi ndiyo
nilimwambia simtaki tena. Nilikaa muda hadi baadaye
nilipopata mwanaume wangu wa sasa. Anani-control vizuri
kwa sababu kanipita umri na ana busara. Tunapendana
sana. Najuta kumfahamu Dallas. Siwezi kusahau tukio hilo
katika maisha yangu. Dallas alicheza na hisia za moyo
wangu. (akaangua kilio) Niliteseka sana. Ni Mungu tu
anajua…
VIPI KURUDIA UKRISTO?
“Nimekaa muda siendi kanisani. Nilikuwa najifungia ndani
nalia kama mama yangu alivyokuwa anafanya. Siku moja
nilimwambia mwanaume wangu akaniambia kuliko kulia
kila siku bora nirudi kanisani. Ndipo nikarudia ukristo. Kwa
sasa nasali Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),
Usharika wa Kijitonyama, Dar,” alisema.
MBALI NA DALLAS
Kwa mara ya kwanza Wolper alikubali kuorodhesha listi ya
wanaume aliowahi kuwa nao kimapenzi kwa kuwachambua
mmoja mmoja.
ALI KIBA
Bila kupepesa macho, Wolper alikiri kuwa msanii wa Bongo
Fleva, Ali Saleh Kiba ndiye aliyemfundisha mapenzi: “Ni
kitambo kidogo. Wote hatukuwa mastaa lakini yeye
alifanikiwa kuchomoka. Kabla ya Ali (Kiba) nilikuwa na
mwanaume lakini hatukuduu kwa maana ya utu uzima,
ilikuwa yale ya kitoto. Lakini Ali ndiye hasa aliyeniingiza
kwenye ulimwengu wa mapenzi.
KWA NINI WALIACHANA?
“Ali akawa staa. Alipokwenda nje nikasikia wanawake
wanamshobokea. Sasa mimi sikutaka karaha nikakaa
pembeni lakini jamaa ni mtu poa sana na tukikutana
tunasalimiana freshi kabisa.”
DIAMOND VIPI?
“Ni kweli niliwahi kuwa na Diamond (msanii wa Bongo
Fleva, Nasibu Abdul). Tulikuwa na uhusiano lakini pia
alikuwa mshirika wa kibiashara (hataki kuitaja). Yeye
alikuwa hawezi kulala bila kuniona, lakini tulikaa kama
mwezi mmoja, kwa sasa amebaki kuwa rafiki yangu na siyo
mpenzi tena kama zamani,” alisema Wolper.
VIPI KUHUSU JUX?
“Jux (msanii wa Bongo Fleva, Juma Khalid) nilikuwa naye
kabla ya Dallas na yule mwanaume wangu niliyeachana
naye wakati wa Dallas. Katika maisha yangu nilimpenda
sana Jux. Siyo marioo ni mwanaume mtafutaji aliyejiamini.
Kwa sasa sipo naye. Dallas pia alichangia mimi kuachana
na Jux,” alimalizia Wolper ambaye kwa sasa ana
mwanaume asiyependa kumwanika.
-Gpl

RAIS JK ATANGAZA KUANZA KWA UJENZI WA KIMATAIFA WA RELI YA KATI.....SOMA HAPA...


Rais Jakaya Kikwete ametangaza kuanza mara moja
mpango mkubwa wa ujenzi wa kimataifa wa reli ya
kati baada ya kupatikana kwa mafanikio makubwa
ya ujenzi wa miundo mbinu ya barabara kwa
kiwango cha lami nchini kote.
Mh rais kikwete ametangaza mpango huo mkubwa
wa ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha
kimataifa,wakati akihutumia maelfu ya wananchi
wa mji wa Old Maswa wilayani Bariadi mkoani
Simiyu muda mfupi kabla ya kuweka jiwe la msingi
kwa ujenzi wa barabara ya kilometa 71.7
inayojengwa na kampuni ya cc ya nchini China kwa
kutumia fedha za ndani kiasi cha shilingi bilioni 70.
Hata hivyo rais Kikwete,amesema serikali,imekuwa
ikitumia fedha nyingi katika ujenzi wa
miundombinu ya barabara yakiwemo madaraja ili
kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi, huku akisema
kati ya madaraja makubwa matano yalipangwa
kujengwa baada ya uhuru,rais wa kwanza Mwl
Julius Nyerere ameweza kujenga daraja la Kirumi
mkoani Mara na rais wa awamu ya tatu Benjamin
Mkapa amejenga daraja la mto Rufiji na sasa
serikali yake imekamilisha ujenzi wa madaraja
matatu yaliosalia.
Awali waziri wa ujenzi Mh. John Pombe
Magufuli,akimkaribisha rais Kikwete kuzungumza
na wananchi ambao wamejitokeza kushuhudia
uwekaji wa jiwe hilo la msingi,amesema ujenzi wa
barabara hiyo itakuwa na manufaa makubwa kwa
wananchi wa mkoa wa Simiyu kwa kuunganishwa
na mikoa ya Mwanza na mara pamoja na nchi jirani
ya Kenya,huku mtendaji mkuu wa wakala wa
barabara mhandisi Patrick Mfugale,akitoa kilio kwa
rais kusaidia upatikanaji wa fedha kwa ajili ya
kulipa wakandarasi nchini.

[AUDIO] MSIKILIZE HAPA MADAM RITA AJIBU MASWALI TISA MUHIMU KUHUSU EBSS 2013 ....!


Shindano la EBSS 2013 linaelekea ukingoni ambapo
November 30, atatangazwa mshindi wa shindano hilo pale
Escape 1, Dar es Salaam.
Washiriki watano waliobaki katika shindano hilo ni
Emmanuel Msuya, Elizabeth Mwakijambile, Amina Chibaba,
Melisa John na Maina Thadei.
Times Fm imefanya mahojiano na Chief Judge wa shindano
hilo, Rita Paulsen aka Madam Rita, na ameweza kujibu
vizuri maswali tisa muhimu.
Watu wengi hawakutegemea Mandela angeondolewa kati ya
washiriki sita, na walitegemea awe kati ya watano, ni upi
mtazamo wako kwa kuzingatia kuwa ulionesha kumkubali
sana?
Mandela pale alipofikia wamemshinda wenzake, lakini sio
kwamba sio muimbaji mzuri. Tunahitaji mshindi mmoja,
kwa hiyo ubora umezidiana na nafikiri hata watazamaji
wanakubalina kwamba hapo alipokuwa amefikia wenzake
ambao wamebaki wanamzidi hata ukiwaweka kwa pamoja,
I’m sure.
Kwa hiyo, ndio kuna mashabiki lakini mshindi lazima awe
na uwezo wa kuimba sio tu mshindi kwa sababu watu
wanashabikia. Lakini sio kwamba hawezi, huwezi kuwa
kama huwezi halafu ukafika top ten, Mandela amefika hadi
top six.
Kuna wasichana wanne na mvulana mmoja tu kati ya
washiriki walioingia fainali, je hii inaonesha kuwa
wasichana wanauwezo zaidi?
Imetokea, sisi huwa tunaangalia vipaji zaidi kuliko gender,
imetokea kwamba wasichana wamefanya vizuri kuliko
wanaume this year. Kwa hiyo kitu ambacho kimetokea na
sio kwamba imepangwa au nini…Imetokea kwamba this
year wasichana wamekaza buti na wamefanya vizuri
mpaka wakafikia top 4.
Kuna wakati nyie kama Majaji huwa mnatofautiana na
unaonesha kukasirika, je huwa iko serious?
yeah..Huwa inakuwa serious, yeah ni serious!
Unazungumziaje comments za Salama kwa kuwa mara
nyingi amekua ‘akimchana’ mshiriki, halafu unaoneka
haufarahii alichokisema na hata unabadilika emotionally?
Mimi sina tatizo nae na na-react kutokana na ninavyokuwa
najisikia. Lakini Salama mimi namkubali kwa sababu
analeta changamoto kwa washiriki na analeta changamoto
kwenye meza ya Majaji na ndio maana yupo leo mwaka wa
saba. Sina tatizo nayo kwa sababu otherwise itakuwa
boring inabidi kuwepo na changamoto. Yeye anaujasiri wa
kuweza kuongea anavyoongea na mimi naweza kuongea
ninavyoongea.
Niseme tu kwamba kila Jaji ambaye yuko kwenye ile meza
ni real, hakuna mtu anafake au whatever. Kila mtu
anakuwa anaongea hisia zake zinavyomtuma.
Ukizingatia hii ni reality show na kuna washiriki wanataka
kusikia yeye anasema nini na hawajali mimi nasema nini,
na kuna watazamaji wanataka kusikia yeye anasema nini
na wala hawataki kusikia mimi nasema nini. Na hiyo ndio
imeifanya EBSS kuwa EBSS…Entertainment.
Kwa kuwa washiriki wote wamekaa nyumba moja kama
familia, je huwa wanagombana? Na kama ndiyo, ni njia gani
inatumika kuhakikisha wanaenda sawa?
Of course wanagombana, kuna uongozi kuna sheria ambao
wanakuwa wanafuatilia, kuna walimu na kuna watu
wanaowakosoa. Kwa hiyo it’s a proper organized thing,
kuna uongozi kabisa kwenye EBSS. Na ikitokea nisema nao
natokea, kwa hiyo kuna discipline ya hali ya juu na
discipliners wapo pia.
Ni mshiriki yupi ambaye wewe unaweza kumtaja kama
mshiriki mwenye nidhamu/mtiifu zaidi?
Kusema ukweli wote walioshiriki mwaka huu ni watiifu na
wana tabia nzuri, they are good kids nashukuru Mungu.
Hatujawa na matatizo ya watu kukosa nidhamu, ni vijana
wazuri na wasikivu na hakuna hata mmoja wao mwenye
tatizo
Ni mshiriki gani ‘mmoja’ aliyetoka katika shindano hilo
lakini kutokana na uwezo wake ungependa sana angekuwa
kati ya hawa watano?
Mandela, Mandela..! Tutaangalia pia jinsi ya kumsaidia
kama muigizaji (Benchmark Production), I think ni
muigizaji zaidi kuliko muimbaji.
Ni ipi picha halisi ya show ijayo ya fainali ya EBSS 2013 na
maandalizi, kwa kuzingatia kuwa siku hizi watu huangalia
zaidi ubora wa show?
Ni changamoto, lakini mimi naweza kuzungumza kuwa
itakuwa very nice, itakua nzuri sana kutokana na..sisi
tunapenda kubadilisha na kuwa na vitu vipya kila mwaka.
Na mwaka huu hiyo ni changamoto kwetu, hiyo ni sehemu
mpya kwetu ni venue mpya pale Escape 1, lakini itakuwa
bomba kinoma.
Watu wengi wanatamani P-Funk Majani arudi kwenye meza
ya Majaji, wewe kama Chief Judge unalichukuliaje?
Hili tutalifanyia kazi!
by timesfmradio
Times Q&A, Madame Rita akiongea na www.timesfm.co.tz
07:05
97 0 0 0 Share Like
Share

Wednesday, 27 November 2013

DIAMOND BAADA YA KUTANGAZA AJIRA SASA ATANGAZA DEMU ANAYEMPENDA JE WAMJUA?


UKIFIKA katika mtaa anaoishi mwanamuziki Diamond
maeneo ya Sinza Mori jijini Dar es Salaam utaanza kuhisi
kuwa kuna staa anayeishi maeneo hayo, macho ya wengi
huanza kumtazama mtu anayeelekea katika geti la nyumba
anayoishi msanii huyo. (HM)
Muda wote geti hilo limefungwa. Ili uweze kuingia ndani
itakulazimu ubonyeze kengele itakayoashiria kuwa kuna
mgeni nje anahitaji kuingia ndani. Hata hivyo hauwezi
kupenya kirahisi ndani hadi uulizwe shida yako na kama
hauna miadi na mtu yeyote anayeishi ndani ya nyumba hiyo
haitakuwa rahisi kuingia.
Mwanaspoti lilitinga katika nyumba ya msanii huyo
na kushuhudia ukimya wa hali ya juu ilhali kuna watu
ndani. Baada ya kufunguliwa geti tuliingia ndani na
kupokewa na Diamond aliyekuwa ameketi katika sebule
iliyonakshiwa na mapambo makini ukutani huku ikiwa na
samani chache lakini za gharama kubwa.
Tulitumia saa mbili mfululizo katika mahojiano na Diamond
ambaye alifunguka kwa kila swali aliloulizwa na kujibu kwa
ufasaha na ufafanuzi mpana.
Mwanaspoti: Utendaji kazi wako ukoje katika muziki?
Diamond: Nina mipango makini katika kazi zangu. Mambo
yote lazima yapitie kwa meneja wangu ndipo yanifikie
mimi, mara nyingi mtu hawezi kuzungumza na mimi moja
kwa moja lazima apite huko na hiyo ndiyo staili ya
Diamond. Nimejipanga kuhakikisha nafanya kazi gani, kwa
wakati gani na sikurupuki tu, japo katika utengenezaji wa
nyimbo zangu naweza nikapata wazo basi hapo hapo
nikatengeneza mistari.
Mwanaspoti: Utendaji kazi wako ukoje kuanzia asubuhi
hadi jioni?
Diamond: Saa tano asubuhi, nikishaamka kitu cha kwanza
ni kwenda 'gym', mara nyingi ni hapa nyumbani kama
unavyoona hapo nje kuna sehemu ya mazoezi na sehemu
nyingine zilizopo ndani, mara nyingi hutumia muda wa saa
moja. Ifikapo saa sita na nusu huwa naanza kufanya kazi
zangu lakini itategemea na ratiba zangu za siku ambazo
ndio mwongozo wangu wa kuimaliza siku. Baada ya hapo
napumzika kwa muda fulani na baadaye jioni huendelea na
kazi na mara nyingi kazi zangu huwa nazimaliza usiku wa
manane.
Mwanaspoti: Unalala saa ngapi? Na unalala kwa muda
gani?
Diamond: Muda wangu wa kulala mara nyingi ni saa kumi
na moja alfajiri na kama sikuwa na kazi nyingi studio basi
nitalala saa nane usiku. Muda wangu wa kulala ni saa sita
mpaka nane kwa siku. Ila hata kama nikilala mapema
kuamka ni saa tano asubuhi ila itategemea na nini
ninakifanya siku inayofuata na kama nina kazi maalumu na
ya mapema itanilazimu niamke mapema ili kuzikamilisha.
Mwanaspoti: Shughuli gani zinazokuchelewesha mara kwa
mara kulala?
Diamond: Ni kurekodi na wakati mwingine shoo. Kwa wiki
ninafanya shoo nyingi, kama ni tatu basi siku zote tatu
nitalala alfajiri. Siku nyingine zinazosalia ninalala usiku wa
manane kwa kuwa huwa nakuwa studio na sehemu
nyingine ambazo hunilazimu kufanya kazi kwa kipindi
kirefu usiku.
Mwanaspoti: Kati ya usiku na mchana ni muda upi
unaopenda kurekodi?
Diamond: Kazi zangu narekodi usiku na ndiyo muda
ninaopendelea zaidi. Mara nyingi napenda kurekodi saa 7
usiku ili niwe na muda na saa nyingine ni kuepuka lawama
kurekodi mchana, kwasababu vijana wengi chipukizi
wataona napendelewa. Unajua ninapoingia studio napenda
kufanya kazi kwa muda mrefu, hata hivyo iliyo bora sifanyi
bora liende na siwezi kufanya kazi na prodyuza
anayenipeleka tu, ni lazima na mimi nipime kama kazi
niliyoifanya inakwenda vile ninavyotaka au kama yeye
anavyotaka ilimradi tufanye kazi nzuri na iliyo
bora.
Mwanaspoti: Unatumia muda gani kurekodi singo moja na
kwa upande wa video ni siku ngapi?
Diamond: Inategemea, inaweza kuwa siku mbili au miezi
sita lakini nyimbo nyingi zinatumia muda mwingi
kwasababu wakati mwingine naanza halafu napata shoo
hivyo inanibidi nipange muda mwingine wa kurekodi. Kuna
nyimbo zangu ambazo nilizifanya kwa muda mrefu sana
hizo huwa sizisahau ikiwemo Ukimwona, Mbagala, Nataka
Kulewa na nyinginezo. Nakumbuka katika kazi nilizofanya
kwa muda mfupi ni My Number One nilioufanya kwa
prodyuza Sheddy Clever kwa kipindi kifupi sana pamoja na
Mapenzi Basi sambamba na Binadamu hizi ni baadhi ya
kazi ambazo hazikunipasua sana kichwa kuzikamilisha.
Mwanaspoti: Una prodyuza wako maalumu au studio yako
mwenyewe?
Diamond: Sina prodyuza maalumu kila kazi nitakayotaka
kuifanya ninatafuta prodyuza yule ninayemtaka hata kama
sijawahi kufanya naye kazi. Ninafanya hivi nikiwa na
malengo maalumu kwa kujiweka vizuri mimi kama msanii
na hata kuwapa nafasi maprodyuza mbalimbali kutia
mkono kwenye kazi ya mikono yangu. Ninaogopa kuwa na
prodyuza maalumu kwa kuwa najua atanisumbua ikiwa
atajua kwamba namtegemea yeye pekee katika kazi zangu.
Studio sina kwa sasa ila nina mikakati ya kuwa na studio
kwani nimeshanunua baadhi ya vifaa.
Mwanaspoti: Unadhani ndiyo sababu iliyokufanya
ukagombana na Bob Junior au Manecky?
Diamond: Hapana haya mambo yalishapita lakini nilijifunza
mengi ndiyo maana niliamua kuja na staili hii. Naogopa
kubaki kuwa msanii ninayetegemea prodyuza fulani, bila
yeye siwezi kufanya muziki, lakini mimi ni Diamond
ninaweza kufanya muziki na prodyuza yeyote naye
akaonyesha ufundi wake kupitia kazi yangu.
Mwanaspoti: Shoo gani kubwa kuliko zote uliyowahi
kufanya ambayo haijawahi kujirudia?
Diamond: Diamond Forever. Hii ilikuwa kubwa sana
ambayo sitakaa nikaisahau, ilihudhuriwa na watu wakubwa
na maarufu hapa nchini hata hivyo ilikuwa ya kipekee
ambayo haijafanana na yoyote ile. Ya pili ni ile ya Dar Live
ambayo nilifanya baada ya kushuka katika helikopta ile pia
ilikuwa kubwa. Lakini kwa nje ya nchi ni Mombasa na
Comoro huko nilifanya shoo kubwa sana ambazo siwezi
kuzisahau.
Mwanaspoti: Ni shoo ipi iliyowahi kukuingizia pesa kubwa
kuliko zote?
Diamond: Shoo ile ya Mlimani City ya Diamond Forever, ile
iliniingizia pesa kubwa sana na tangu pale ndipo
nilipoanza kufurahia matunda ya kazi yangu. Nilifanya
shoo pia Burundi, Mombasa na Congo shoo hizi
ziliniingizia kiasi kikubwa sana cha pesa siwezi kutaja ni
shilingi ngapi lakini ni pesa nyingi ambazo sitakaa
nizisahau.
Mwanaspoti: Shoo ipi ilikuwa ya bei chee ambayo huwezi
kuisahau
Diamond: Kwa kweli siwezi kusahau nilipofanya shoo
yangu ya kwanza kubwa mwaka 2009 kwenye Fiesta
iliyofanyika Dar es Salaam, ilikuwa ndiyo shoo yangu ya
kwanza na kubwa wakati huo nilikuwa natamba na wimbo
Kamwambie, ilinichukua muda mrefu sana kujiandaa mimi
pamoja na madansa wangu wanne tulilipwa Sh 50,000
lakini sikukata tamaa kwani ilikuwa ndiyo mwanzo wangu
wa kujuana na watu wengi na wadau wakubwa wa muziki
hapa nchini ambao nilikutana nao kwenye ile shoo.
Mwanaspoti: Kwa hivi sasa ni shoo gani ambayo unaweza
kusema kwamba utafanya kwa bei ya chini na ni shilingi
ngapi?
Diamond: Shoo ninayoweza kufanya kwa bei ya chini
kabisa ni Sh 10 milioni za Kitanzania na hii labda nione
anayeniomba nifanye shoo hiyo hayuko vizuri na pengine
ni rafiki yangu na hawezi kuninyonya, si hivyo tu
itategemea pia ni kampuni gani na ni watu wa aina gani
ambao watanitaka nifanye nao kazi.
Mwanaspoti: Kwa kawaida Diamond ni msanii wa gharama
gani kwa shoo moja ndani na nje ya nchi?
Diamond: Kwa kawaida shoo moja ninafanya kuanzia Sh15
milioni mpaka Sh20 milioni kulingana na muda
nitakaofanya shoo. Pia zile za nje ninafanya kwa gharama
ya Dola 20,000 mpaka 30,000 yaani ni Sh32 milioni mpaka
48 milioni hivi kwa fedha za Tanzania na nikiwa huko
nahakikisha ninafanya kazi vile inavyotakiwa. Lakini hali ni
tofauti inavyokuja shoo ile ya uwanjani yaani hapa
nazungumzia shoo kubwa zinazofanyika nje ya ukumbi,
hizi natoza Dola 20,000 ambayo ni sawa na Sh32 milioni
32 kwa fedha ya Kitanzania.
Mwanaspoti: Kuhusu madansa wako unawachukuliaje?
Diamond: Ni kama kaka zangu na ninawapenda sana kwani
tumetoka nao mbali na wanajua kuwa tunafanya kazi
pamoja kutengeneza maisha hivyo ni kama ndugu zangu
na tunasaidiana kwenye kila jambo ukizingatia kuwa kile
tunachokipata tunagawana. Kwa kweli najitahidi sana
kuwaambia hasa kuhusiana na masuala ya kimaisha,
nahusika katika maisha yao ya kila siku na nijuavyo mimi
nikikosea tu mmoja akapotea kundi langu litakuwa
limeharibikiwa maana kila mtu namtegemea kwa upande
wake. Kwa sasa wamejenga nyumba zao na wanaendelea
vizuri kimaisha hilo ndilo sharti langu lazima wafanye
mambo ya maendeleo kwa kile tunachokipata.
Mwanaspoti: Umesafiri nao nchi ngapi, na kwanini
unapenda kuambatana nao?
Diamond: Nimesafiri nao sehemu mbalimbali kama Burundi,
Comorro na sehemu nyinginezo ambako nimekwenda
kufanya shoo, sina tabia ya kusafiri peke yangu hata
nikienda Ulaya na hata Marekani lazima niwe nao.
Ninapenda kuwa nao kwani ni sehemu ya muziki wangu na
imefika wakati nimekuwa nataka mapromota kuhakikisha
wanatulipia mimi na madansa wangu kwa ajili ya shoo
hasa tutakapojua kuwa shoo fulani itaingiza watu wengi au
udhamini mkubwa.
Mwanaspoti: Kuna safari ambayo umewahi kusafiri peke
yako?
Diamond: Ziko nyingi, nilienda mwenyewe kutokana na
ukubwa wa shoo, lakini ni miaka kadhaa nyuma, baadaye
nilijiwekea mikakati kwamba siwezi kusafiri mwenyewe
wakati shoo nahitaji kufanya na madansa wangu, awali
mapromota walikuwa wagumu kunielewa na wapo
waliokataa. Niliachana nao na kuwataka wakishajipanga
na kuhakikisha kwamba wanaweza kunichukua mimi na
madansa wangu watafanya hivyo.
Mwanaspoti: Umewahi kuwatema madansa?
Diamond: Sijawahi kubadilisha madansa kwa sababu
wanajua kazi yao. Ingawa nilikuwa na madansa sita
nilipokuwa naanza muziki lakini niliachana na wawili
kutokana na utendaji wao wa kazi. Wawili hawa hawakuwa
wabunifu kila siku walikuwa na staili ileile, niliamua
kuchagua vichwa ambavyo vikikaa na mimi mwishowe
tunatoka na kitu makini na chenye kueleweka. Kulikuwa na
tatizo pia la kukosea stepu wakati wa shoo hili lilikuwa
likinishushia sana hadhi yangu jukwaani, hapo ndipo
nilipoamua kuwaondoa.
Mwanaspoti: Kwa upande wa malipo unawalipaje?
Diamond: Ninawalipa vizuri lakini siwezi kutaja kiwango ila
ingekuwa kwangu ningetaja, hiyo ni haki yao wao wenyewe
kutamka ila mimi siwezi kutaja. Malipo ninayowalipa yapo
machoni mwa watu wanaowazunguka, dansa kujenga
nyumba kumiliki baadhi ya biashara si jambo dogo, hivyo
ninawalipa vizuri. Na hata gharama za kusafiri ndani na nje
ya nchi vyote ni juu yangu, malipo tunayoyapata
tunagawana.
Mwanaspoti: Unakumbana na changamoto zipi katika kazi
yako?
Diamond: Nakumbana na mengi, kwanza unapokuwa
msanii unayeongoza lazima upate vikwazo vingi.
Nakumbana na watu wengi wanaonichukia na kunitusi bila
sababu za msingi, hata hivyo nasingiziwa vitu vingi
ambavyo havipo nadhani hii ni changamoto iliyotokana na
kufanya vizuri katika muziki.
Wapo ambao wanamwona Diamond anafanya vizuri
kwenye muziki badala ya kukaa na kuangalia nimepita
wapi na wapi anaanza kutoa lawama kwamba ameibiwa na
mengine ambayo kimsingi hayana maana.
Mwanaspoti: Siku za hivi karibuni kuna maprodyuza na
wasanii wasiofahamika ambao walijaribu kutengeneza kazi
yako ya My Number One na kukutusi kupitia wimbo huo na
wapo waliotunga mashairi mengine yaliyozungumzia
maisha yako kabla hujawa staa, ulijisikiaje? Na unachukua
hatua gani?
Diamond: Awali niliumia sana nilipoibiwa mashairi ya
wimbo wangu wa Mbagala, iliniuma sana kwa muda wa
wiki nzima uchungu nilioupata siwezi kuuelezea. Lakini
baadaye nilikomaa, huwezi amini niliposikia zile nyimbo
nilicheka sana kisha nikawadharau sana watu waliofanya
hivyo maana nipo kwenye hii tasnia siwezi kuchukia watu
wasiojua walitendalo kwani na wao wapo katika kujitafutia
riziki. Lakini hata hivyo sheria ya muziki bado haijawa
makini hapa nchini
nitachukua hatua gani mwisho wa siku nitaacha kufanya
mambo yangu ya msingi na kushughulikia wezi wa kazi
zangu ambao hata hivyo hawatabanwa kwa lile
walilolifanya.
Mwanaspoti: Msanii yupi hapa Tanzania anakutisha kama
hayupo vipi huko nje ya nchi?
Diamond: Kwa hapa Tanzania sijaona mwanamuziki
anayenitisha, ila siwezi kujua mashabiki wao ndio majaji,
nafikiri kila mtu anaweza kuwa na mtazamo wake. Kati ya
wanamuziki ninaowahusudu mimi kwa nje ya nchi hasa
Afrika ni P Square pekee, hawa wapo katika nafasi kubwa
sana kwenye ubongo wangu na nafikiria ni lini ninaweza
kuwafikia, hiyo ndiyo ndoto yangu daima.
Mwanaspoti: Unapokuwa juu ya jukwaa unakumbana na
vishawishi vipi ukiwa kama msanii mkubwa?
Diamond: Ninapata vishawishi vingi sana ninapokuwa
jukwaani. Kwa kweli ninashawishiwa na wakinadada,
mfano kuna mwanamke mmoja ambaye alikuwa mmoja wa
mapromota wa shoo nchini Uingereza alitaka kunibusu
mdomoni kwa lazima, kitendo kile kilinifedhehesha sana na
nilishindwa nifanyeje kwani nipo ugenini na jukwaani
ilikuwa ngumu sana kwangu. Wakati mwingine wanawake
wanapanda jukwaani ili wacheze na wewe mwisho wa siku
wanaingiza mikono kwenye suruali yaani sipendezwi
kabisa na michezo ya namna hii.
Mwanaspoti: Umewahi kuibiwa ukiwa jukwaani?
Diamond: Nimeshaibiwa sana hasa katika hizi shoo ndogo
ndogo mara nyingi watu wanapanda jukwaani na kuondoka
na kitu chako. Nakumbuka nimeshawahi kuibiwa saa, pete
ya dhahabu na kuna mmoja alitoa kali ya mwaka yaani
yeye alinivua nguo kwa lazima.
Mwanaspoti: Inakuwaje nje ya muziki, unakumbana na
changamoto zipi?
Diamond: Kitu ambacho ni changamoto kubwa sana
kwangu ni simu yangu ya mkononi. Kila baada ya miezi
sita au mitatu nalazimika kubadili namba yangu ya simu,
nasumbuliwa sana na watu ambao hata hivyo hawana la
msingi la kuniambia. Ni kweli kwamba mawasiliano ni kitu
cha msingi na
ninawapenda mashabiki wangu lakini namba yangu
inasambaa kwa kasi ya ajabu kiasi kwamba nashindwa
kupokea simu za maana kwa kudhani kwamba na hao nao
ni wasumbufu.
Mwanaspoti: Ina maana milio yote ya simu hapo ni watu
wanakupigia?
Diamond: Yap, unavyoona inalia kila dakika watu wanapiga
hapa. Muda mwingi hii simu ninaweka 'silent' yaani haitoi
mlio wowote kwani inaita kila dakika.
Mwanaspoti: Tuzungumzie uhusiano wako. Mpenzi wako
wa kwanza unamkumbuka? na je uliwahi kumpa shilingi
ngapi?
Diamond: Mpenzi wangu wa kwanza kabisa enzi hizo
ninajifunza mambo haya sikumbuki vyema jina ila alikuwa
anaishi Tandale na mimi pia nilikuwa naishi huko na mama
yangu. Sikumbuki kama nimewahi kumhonga maana enzi
hizo mimi nilikuwa napewa tu na mama yangu pesa,
sikuwa na hela yoyote ya kumpa na ilikuwa ni kwa kipindi
kifupi kama miezi minne hivi, hata hivyo tulikuwa
tunaibana tu kwa siri nilikuwa mdogo.
Mwanaspoti: Kwanini mliachana?
Diamond: Kwanza nilikuwa sijajua mapenzi ni nini. Hata
hivyo haikuwa rasmi na wala nilikuwa sijawa na akili ya
kupenda sana na nilikuwa na fikra kwamba ni mchezo tu
hivyo tuliachana mapema kwani hata yeye akili yake
ilikuwa haijakomaa.
Mwanaspoti: Mpenzi wako uliyekuwa naye kabla ya kuwa
staa nasikia uliachana naye baada ya kutoka kimuziki kwa
nini?
Diamond: Nilimpenda sana lakini aliniacha kabla ya
kutoka. Mpenzi wangu wa kwanza alikuwa anaitwa Sarah
Sadick, sijawahi kumuhonga na ndiye mwanamke
niliyewahi kumpenda sana. Wakati huo Naseeb Abdul kabla
sijawa Diamond nilikuwa nahaha kuhangaika ni vipi
nitatoka kimuziki. Msichana huyu ndiye aliyenipa hasira za
kufanya muziki kwa bidii zote baada ya kunitema na
kuanza kuhangaika na wengine na aliniita majina mengi
yasiyo mazuri, kisa sina fedha. Si kwamba nilimuacha bali
yeye ndiye aliyeniacha kama zali baada ya wiki kadhaa
nikatoka na wimbo Kamwambie, taratibu nikaanza kuwa
staa naye akaanza kurudi ila nilishamuondoa moyoni
mwangu.
Mwanaspoti: Kwa nini mliachana? Unadhani hakukufaa
tena kwa kuwa ulishakuwa staa?
Diamond: Alinisumbua sana kutokana na ugumu wa
maisha niliokua nao kwa kipindi cha nyuma hadi kufikia
2009. Nilimpenda sana huwezi amini nilikuwa silali
usingizi kwa ajili yake. Nahisi ilitokana na mimi kukosa
kazi ndiyo maana ilifikia hatua alinipotezea. Lakini baada
ya kupata na kujulikana alinifuata lakini sikutaka tena hata
baada ya kuniomba msamaha.
Mwanaspoti: Umewahi kuwa na wanawake wangapi tangu
uwe staa?
Diamond: Sikumbuki kwa kweli wapo wengi mno, si unajua
tena wapo walionitaka na kunilazimisha nifanye hivyo,
lakini idadi kamili siwezi kukumbuka na kila siku
nasumbuliwa na hawa wanawake.
Mwanaspoti: Ni wapenzi wangapi ambao umekuwa nao
kipindi kirefu na kuwapenda kama wapenzi wako?
Diamond: Nimewahi kuwa na wapenzi wanne katika kipindi
chote cha ustaa wangu na sikupenda kubadili ovyo ila
wengi wao hawakuweza kutimiza haja ya moyo wangu.
Mwanaspoti: Unaweza kuwataja majina?
Diamond: Ndiyo ila wawili wanafahamika zaidi. Wa kwanza
kabisa alikuwa anaitwa Sarah na wa pili alikuwa anaitwa
Hawa yule msichana niliyeimba naye katika wimbo
'Nitarejea', huyu alizidiwa ujanja na Wema Sepetu ambaye
naye alikuja kuondoka kwangu na baadaye nikawa na
Penieli Mungilwa.
Mwanaspoti: Mwanamke yupi unahisi ulimpenda kuliko
wote?
Diamond: Mwanamke wangu wa kwanza Sarah Sadick
huyu aliniingia sana moyoni sijajua ni kwanini. Lakini
nahisi huenda kwa kuwa awali alinipenda kweli kwa kuwa
wakati huo sikuwa na kitu. Hata hivyo nahisi ilitokana na
mimi kutokuwa bize na wakati huo sikufikiria lolote zaidi ya
yeye ilitokana na kutokuwa na kazi ya kufanya. Siku hizi
sina mapenzi ya kivilee, nawaza zaidi pesa na
ninaihangaikia na zaidi ni muziki wangu, hili ndilo la
kwanza kabisa linalonifanya niwe bize mapenzi baadaye.
Mwanaspoti: Umeshawahi kutongozwa na wanawake?
Diamond: Ndiyo, wengi sana tena kuna mmoja kati ya
wanawake niliowahi kuwa nao alinitongoza yeye
mwenyewe ndipo nikawa naye na nilikaa naye katika
uhusiano kwa kipindi kirefu tu. Wanaweza kumfikiria
mwanamke fulani lakini huwezi amini ukweli ninao mimi
mwenyewe na katu hawawezi hata kumhisi. Ninatongozwa
sana kwenye mitandao ya kijamii, facebook, whatsapp,
Instagram na kwingineko na wapo wasichana ambao
wanatafuta namba zangu za simu na kuanza kunisumbua.
Mwanaspoti: Unapata usumbufu wowote toka kwa
wanawake?
Diamond: Ndiyo, wengi sana tena kuna mmoja kati ya
wanawake niliowahi kuwa nao alinitongoza yeye
mwenyewe ndipo nikawa naye na nilikaa naye katika
uhusiano kwa kipindi kirefu tu. Wanaweza kumfikiria
mwanamke fulani lakini huwezi amini ukweli ninao mimi
mwenyewe na katu hawawezi hata kumhisi. Ninatongozwa
sana kwenye mitandao ya kijamii, facebook, whatsapp,
Instagram na kwingineko na wapo wasichana ambao
wanatafuta namba zangu za simu na kuanza kunisumbua.
Mwanaspoti: Ni mwanamke wa aina gani unataka awe
mkeo?
Diamond: Kwanza ninahitaji aijue kazi yangu na ajue
kwamba mimi ni mtu maarufu hivyo akubaliane na
changamoto mbalimbali atakazokumbana nazo kwa kipindi
atakachokuwa ndani ya ndoa, siyo siku mbili anafungasha
virago. Pia ajue kwamba nitamsikiliza mama yangu
kwanza kabla ya yeye hilo naliweka wazi, yeye ana nafasi
yake katika maisha yangu lakini mama yangu nimempa
kipaumbele, tatu awe tayari kuishi na mama yangu. Nne
awe na akili na mwenye utambuzi na atakayeniongoza
katika kazi zangu, sihitaji. Itaendelea…
Chanzo: mwanaspoti