Wednesday, 5 November 2014

Makubwa Haya!! HARUSI YA NYANI YAKUSANYA MAMIA YA WANAKIJIJI,UNAAMBIWA NYANI HAO WANAPENDANA SANA!!



Haharusi wakipitishwa mtaani
Zaidi ya wakazi 200 katika kijiji kimoja kaskazini mwa India wamehudhuria sherehe ya harusi ya nyani wawili. 

Harusi hiyo iliandaliwa na mmiliki wa nyani hao, ambaye alisema nyani dume ni kama "mwanaye".

Sherehe hiyo ilifanyika siku ya Jumatatu katika wilaya ya Bettiah, katika jimbo la Bihar, huku "bi harusi" akiwa amevalia gauni maridadi. 

Nyani ni viumbe wanaopendwa na watu wa jamii ya wa-Hindu.

"Bwana harusi" ambaye anajulikana kama Ramu pamoja na mkewe mpya aitwaye Ramdulari walipitishwa katika mitaa ya kijiji wakiwa juu ya gari lililopambwa kwa maua na muziki ukichezwa, huku mamia ya wanakijiji wakijipanga kuwashangilia.
Mmiliki wa nyani hao Udesh Mahto ambaye ana watoto watatu wa kiume amesema nyani Ramu ni kama mtoto wake wa kwanza.

"Nilitaka yeye ndio aanze kuoa," ameiambia Idhaa ya BBC ya Kihindi.
Bwana Mahto alimnunua Ramu kutoka Nepal miaka saba iliyopita, na baadaye kumnunua Ramdulari katika soko la kijiji.

"Mwanzoni hawakuwa wakielewana sana, lakini baadaye wakaanza kupendana, kwa hivyo nikaamua kuwafungisha ndoa," amesema.

Padre wa Kihindu Sunil Shastri "alifungisha" ndoa hiyo.

"Mwanzoni nilikuwa na mashaka, kufungisha ndoa ya nyani, lakini nilibadili mawazo baada ya kuona Bwana Mahto hafanyi mzaha," amesema. 

"Tulipanga siku na saa ya sherehe hiyo."
Kadi za mwaliko zilichapishwa na bendi kukodishwa, huku wageni wakipatiwa makulaji.

Watu wengi kutoka vijiji vya jirani walihudhuria na wengine kupiga picha za kuziweka kwenye mitandao ya kijamii.

VENGU MUNGU AMETENDA


MUNGU mkubwa! Vengu is back from hell (Vengu amerudi toka kuzimu). Msanii staa wa Kundi la Orijino Komedi ‘OK’, Joseph Shamba ’Vengu’ ameanza kurejea katika ‘fomu’ baada ya kuugua kwa muda mrefu, Risasi Jumatano linathibitisha.
Msanii staa wa Kundi la Orijino Komedi ‘OK’, Joseph Shamba ’Vengu’.
Kwa mujibu wa ndugu wa karibu wa msanii huyo (jina tunalo), Vengu ambaye kwa muda mrefu alipoteza kumbukumbu kiasi cha kushindwa kuwatambua watu, sasa amejaliwa kwani anaweza kuwafahamu watu mbalimbali wanaopata nafasi ya kwenda kumjulia hali, Kigamboni jijini Dar anakoishi.
AMEANZA KUTOA ‘HI’ KWA WATU
“Bado yupo chini ya uangalizi maalum wa kifamilia, ni watu wachache wanaruhusiwa kumuona, lakini sasa hivi huwezi kuamini, watu wanaofika kumtazama anawatambua na anawapa ‘hi’.
TATIZO USIRI
Kutokana na usiri wa hali ya msanii huyo unaofanywa na familia yake, kumekuwa na maneno chini kwa chini ikiwa ni pamoja na uzushi wa mara kwa mara kuwa, mchekeshaji huyo maarufu, amefariki dunia na kuzikwa kwa siri jambo ambalo si la kweli.
Hata hivyo, katika namna ya kusikitisha, ndugu huyo alisema kuwa kila Vengu anapomtambua mtu anayemtembelea amekuwa akimwaga machozi hali inayoonesha kuwa anarejesha nyuma kumbukumbu zake na kugundua amekuwa mbali naye kwa muda mrefu.
Mfano wa nyumba ya Vengu.
KUREJEA KWENYE FANI
Pia ndugu huyo alisema kwa hali ya Vengu sasa anaweza kurejea kwenye kazi zake za kuchekesha kama zamani zile.“Kwa jinsi ilivyo, Vengu atarejea hivi karibuni katika kazi yake ya kuburudisha akiwa sambamba na wenzake wa Orijino Komedi kwa sababu afya yake inaimarika sana,” alisema ndugu huyo huku akikataa katakata kutoa ramani ya nyumba anayoishi Vengu ili mapaparazi wetu wende wakamjulie hali.
APEWA NYUMBA
Kana kwamba haitoshi, wakati hali yake ikisemwa na ndugu inaendelea vizuri, kuna madai kwamba msanii huyo na familia yake wamepewa nyumba ya kisasa yenye thamani ya shilingi milioni 120, sawa na wasanii wenzake akina Wakuvanga kufuatia mkataba wa kundi hilo na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).
“Ni kweli afya ya Vengu kwa sasa ipo vizuri, anajitambua. Pia amepewa nyumba, kubwa tu ipo kulekule Kigamboni anakoishi lakini bado hajahamia.”
KUMBUKUMBU
Vengu alianza kuugua kidogokidogo mwaka 2009, lakini Agosti, 2011 hali yake ilikuwa mbaya, akalazwa kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar. Rais Jakaya Kikwete ‘JK’ aliwahi kwenda kumjulia hali.
Baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya, alipelekwa kwenye Hospitali ya Apollo nchini India ambako alipatiwa matibabu na kurejeshwa nchini akiaendelea kuuguzwa na familia yake huku taarifa zake zikiwa ngumu kupatikana mpaka hivi karibuni ambapo ndugu mmoja aliamua kuweka wazi hali ilivyo kwa sasa.
Ugonjwa wake mkubwa ulitajwa kushambulia sehemu ya kichwa, hasa kwenye ubongo.

ANGALIA PICHA_ MAZISHI YA MWANAFUNZI ALIYEFARIKI MASAA MATATU KABLA YA KUANZA KUFANYA MTIHANI WAKE WA FORM FOUR HUKO SIMIYU



Mwili wa aliyekuwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Simba wa Yuda Yunis Festo aliyefariki dunia siku ya Jumatatu wiki hii saa 11 alfajiri muda mchache kabla ya kuanza kufanya mtihani wa kuhitimu kidato cha nne mwaka 2014
Eneo la msiba wa aliyekuwa mwanafunzi wa shule ya sekondari Simba wa Yuda  Yunis Festo 

Mwili wa marehemu Yunis Festo ukiwa umebebwa kwenye jeneza tayari kwa mazishi nyumbani kwao na mwanafunzi huyo katika kijiji cha Igembe wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza


 mwili wa marehemu ukiwa kwenye jeneza wakati wa ibada ya mazishi mchana huu kabla ya mazishi
 Watu mbalimbali wenye mapenzi mema wakifuatilia ibada ya mazishi
 Watu mbalimbali wenye mapenzi mema wamejitokeza katika mazishi hayo
Mmoja wa walimu wa mwanafunzi huyo bwana Damian Kageba Kupimo akiwa msibani leo

 Jeneza la marehemu
mwili wa marehemu ukipelekwa makaburini kwa ajili ya mazishi

Mwanafunzi Yunis Festo enzi za uhai wake.Hii picha alipiga tarehe 1,Novemba 2014 siku ya mahafali ya shule ya sekondari Simba wa Yuda



 Mazishi ya mwanafunzi Yunis Festo aliyekuwa anasoma kidato cha nne katika shule ya sekondari Simba wa Yuda iliyoko katika kijiji cha Bulima wilaya ya Busega yamefanyika mchana huu katika kijiji cha Igembe wilaya ya  Kwimba mkoani Mwanza .

Watu mbalimbali wenye mapenzi mema wakiwemo walimu,wanafunzi,viongozi wa dini na wakazi wa kijiji hicho na wengine kutoka mikoa ya jirani wamehudhuria mazishi hayo.

Ibada ya mazishi imeongozwa na mchungaji Josephares Ihoneyo Mtebe.


Yunis Festo aliyezaliwa tarehe 26.02.1996 amefariki dunia juzi saa 11 alfajiri  zikiwa zimesalia saa tatukuanza kufanyika kwa mtihani wa kidato cha nne kote nchini ulioanza juzi Jumatatu.

Malunde1 blog iliiambiwa kuwa mwanafunzi huyo amefariki dunia juzi baada ya kukimbizwa  katika kituo cha afya  Bulima na wanafunzi wenzake aliokuwa nao bwenini alipozidiwa majira ya saa 9 usiku wa kuamkia siku ya Jumatatu.

Habari zinasema kuwa mwanafunzi huyo alikuwa anaumwa kichwa na kwamba alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa Sickle Cell.

Malunde1 blog inawapa pole ndugu,jamaa na marafiki waliofikwa na msiba huo.

Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Yunis Festo.Amina

TAZAMA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2014 HAPA!

LILE SAKATA LA MKE KUISHI NA WANAUME WAWILI ZAIDI YA MIAKA 8 LACHUKUA SURA MPYA

Mume halali Rogers Halinga wakiwa na mkewe juliana Hosea kwenye kikao cha ndugu wa mume kijijini Ishungu
j
Mume halali Rogers Halinga akiwa na baba yake Jonson Halinga pamoja na mtoto anaegombaniwa  

Baadhi ya ndugu katika kikao hicho



Sakata la mke kuishi na wanaume wawili lachukua sura mpya baada ya kikao cha ndugu wa mume halali Rogers Halinga kuketi kikao Kijiji cha Ishungu Kata ya Ruiwa Mbarali Mkoani Mbeya na kumtaka Biton Mwashilindi kufanya mazungumzo nao kabla hawajafungua madai ya ugoni Mahakani na kudai fidia.
Kikao hicho kizito kilichofanyika nyumbani kwa Baba mzazi wa Rogers Halinga mzee Jason Halinga(95) Novemba mosi mwaka huu na kuhudhuriwa na ndugu lukuki na kumsikiza mke wa Rogers ili abaini ukweli juu ya mtoto aliyezua utata kuwa ni wa nani baina ya Rogers au Biton Mwashilindi.
Mwanamke huyo  a(22) akijikanganya mara kadhaa katika kikao hicho akidai kuwa mtoto huyo ni wa Rogers kwa kuwa aliondoka baada ya kutokea mapishano na mumewe akiwa na ujauzito wa miezi minne ndipo alipoanza mahusiano ya kimapenzi na Biton hadi siku anajifungua mwaka 2012 akiwa mikononi mwa Biton ndipo alipoamua kumwandikisha mtoto katika kadi ya kliniki na cheti cha kuzaliwa jina la Biton.
Huku ndugu wakihamaki kutokana na kauli hiyo na kwamba yeye atamke wazi mtoto ni wa nani ndipo Juliana bila aibu kwa Baba Mkwe Mzee Jason Halinga alijibu kuwa mtoto ni wa Biton Mwashilindi,ambapo alimkabidhi mtoto huyo mwishoni mwa mwezi Octoba kwa hiari na wala hakuporwa kama alivyotoa taarifa Polisi.
Kauli hiyo ya Juliana ililazimu kikao kupiga simu kwa mzazi wa Juliana anayeishi Lwanjilo wilayani Chunya kujua mustakabali wa kauli ya mtoto wao kwani ilidaiwa kuwa Biton aliwahi kwenda huko kujitambulisha kuwa yeye anaishi na mtoto wao na kwamba Biton hakujua kuwa Juliana aliwahi kuolewa kwani alidai kuwa yeye ni mwanafunzi wa VETA Mbeya na asimwambie kuwa yeye ni mwanandoa.
Baba mzazi wa Juliana Hosea Mwalukasa alidai kuwa ni kweli Biton alifika kwake lakini hakumpokea kwa kuwa alidai kuwa Juliana ni mke halali wa Rogers Halinga hivyo kama amezaa na Juliana amefanya kosa na kwamba atatozwa ugoni kwani Juliana hakuwahi kupewa talaka na Halinga.
Kikao hicho baada ya mvutano wa muda mrefu kiliamua kuwa endapo Biton anadai kuwa mtoto aliyezaliwa na Juliana aliyefahamika kwa jina la Zalida Biton(2) ni mtoto wake basi alipe fidia ya kuzaa na mke wa mtu kiasi cha shilingi milioni kumi au alipe n'gombe saba ili aweze kumkomboa mtoto wake na kwamba Juliana bado ni mke halali wa Rogers.
Kwa upande wake Biton Mwashilindi alidai kuwa hayuko tayari kulipa pesa hizo na kwamba yeye alikabidhiwa mtoto kihalali na Jeshi la Polisi Ocktoba 31 mwaka huu kituo kikuu cha kat mbele ya maafisa wa Jeshi la Polisi na kwamba hana kesi ya kujibu na kwamba anasubiri tu mtoto afikishe umri wa miaka saba ndipo amchuke.
Katika suala hili baadhi ya wadau wamelalamikia Jeshi la Polisi kwa kuamua  masuala ya kisheria katika vituo vya Polisi badala ya mamlaka za kisheria zipo kama mahakama kuliko uamuzi uliotolewa na hali hii husababisha baadhi ya wananchi kujichukulia sheria mkononi.
Wamedai kitendo cha kukabidhiwa mtoto Biton bila kuchukuliwa vipimo vya DNA bado hakujatutua mgogoro huu na kwamba bado suluhu katika ndoa hiyo hiyo itakuwa ni kitendawiri kisicho na majibu.

MKIENDELEA KUYAFUMBIA MACHO TUTEGEMEE AIBU ZAIDI KWENU RITA!



Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), bila shaka mko vizuri mnaendelea kusimamia jukumu zito katika taifa letu.Usajili, Ufilisi na Udhamini siyo kazi ndogo. Ni kazi inayohitaji umakini wa hali ya juu maana matokeo ya ufanisi wenu ndiyo majibu ya shughuli nyingi katika nchi.
Watu wakitaka kusafiri, kutambulika katika maeneo mbalimbali nyinyi lazima mhusike kutatua.
Mkitaka kujua afya yangu, mimi ni mzima. Namshukuru Mungu naendelea na majukumu yangu kama kawaida. Nimewakumbuka leo kupitia barua hii ili niweze kuwafikishia yaliyoko katika akili yangu ndogo. 

Madhumuni ya barua hii kwanza kabisa ni kutaka kuwauliza, hivi mmewahi kuwaza kwamba kuna uwezekano mkubwa wa watu kufanya madudu ya kufoji vyeti kama anavyodaiwa kufanya mshindi wa Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu?Kwa kuanzia eneo hilo, ni vyema basi chombo chenu kikafanya tathmini upya katika kuhakiki taarifa mbalimbali na kuweka mfumo mzuri wa kudhibiti mtu kufanya udanganyifu wa aina yoyote. Msisubiri hadi yatokee ya kutokea

NGWEA FEKI AGOMBEA MAITI YA MAMA’KE


Stori: Gabriel Ng’osha
Kijana Mohamed Said almaarufu Ngwea feki, anayefananishwa na aliyekuwa staa wa Bongo Fleva, marehemu Alberth Mangweha ‘Ngwea’, ameingia katika mzozo mkali na ndugu zake akidaiwa kugombea maiti ya mama yake mzazi, Mariamu Enock (54).
Kijana Mohamed Said almaarufu Ngwea feki.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, tukio hilo lilijiri kwenye makazi ya familia hiyo, Tandale, Dar hivi karibuni ambapo mama huyo alifariki dunia kwa kuugua kwa muda mrefu.
Ngwea feki akizozana eneo la msiba.
Ilidaiwa kwamba, baada ya kifo hicho, uliibuka mzozo ambapo ndugu wa upande wa mama yake walitaka mwili wakaupumzishe mkoani Iringa huku Ngwea feki akitaka uzikwe Dar. Ilisemekana kwamba jamaa huyo alitaka iwe hivyo kwa sababu alikuwa na mama yake muda wote na alitumia gharama kubwa kumtibu.
Kaka wa Ngwea Feki, Hassan Said.
Akizungumza na mwanahabari wetu kuhusiana na sakata hilo, msemaji wa familia hiyo, Laurence Enock ambaye ni kaka wa marehemu (yaani mjomba wa Ngwea feki), alisema:  “Sisi kama familia tumeamua kumsafirisha ndugu yetu kwenda kumzika Iringa, ndiko kuna mashamba ya familia yetu lakini Mohamed (Ngwea feki) amekataa.”
Baba wa marehemu (babu wa Ngwea Feki), mzee Enock Mayenje.
Alisema kwamba, baada ya vuta nikuvute ndipo Ngwea feki akadai alipwe shilingi laki tatu (300,000/=) alizotumia kumtibu mama yake wakati anaumwa.Kwa upande wake, ndugu wa Ngwea feki aliyefahamika kwa jina la Hassan Said alionekana kutomuunga mkono ndugu yake.
Ndugu wa Ngwea feki, Hassan Said (kushoto) akiwa eneo la msiba.
Hassan alisema: “Mimi siko tayari kugawana vitu vya mama yangu kwa kuwa ndugu yangu amekataa mwili wa mama usisafirishwe hadi alipwe fidia yake hivyo imebidi tuuze vitu vya mama ili alipwe hiyo laki tatu.
Wa pili kushoto ni msemaji wa familia hiyo, Laurence Enock ambaye ni kaka wa marehemu (yaani mjomba wa Ngwea feki)
Alipofuatwa Ngwea feki ili kusikia upande wake aligoma kutoa ushirikiano: “Siko vizuri kwa sasa nicheki baadaye.”
Kwa mujibu wa baba wa marehemu, Enock Mayenje, mjukuu wake huyo amekuwa akijitenga na familia hivyo hawezi kumlazimisha ila amesikitika kwa kitendo chake cha ‘kuwauzia’ maiti ya mama yake mzazi.
Marehemu Mariamu Enock enzi za uhai wake.
Kamanda wa Ulinzi Mtaa wa Mkunduge, Tandale jijini Dar, Yusuph Banda, amekiri kutokea kwa tukio hilo na wamekubaliana kuuzwa kwa vitu vya marehemu ili gharama hizo zilipwe kwa Ngwea feki ili mwili huo usafirishwe kwenda Iringa kwa mazishi.

JINSI YA KUMFAIDI MWANAMKE MNENE


 
Mwanamke mnene ni mtamu sana, ana joto kali sana ndani ya uke, ana nyamanyama ambazo hazimuumizi mwanaume wakati wa kutoa mastyle, mwanamke mnene akikaa style ya chuma mboga basi lile sponji la nyuma loooote lasababisha maangamizi ya muda mfupi kwa abdalah kichwa wazi, mwanamke mnene ana degree ya kwenda miondoko ya r ...N b kitandani ambayo huwa so romantic na haitoi jasho, mwanamke mnene akivua nguo akalala kifudifudi basi mkaka hata kama anaangalia mpira lzm atadata, mwanamke mnene ana sifa ya kukojoa bila kumwaga maji mengi. 


Watu wanasema eti wanawake wanene wananuka na huwa na fangasi?

Aliewaambia wanene wananuka nani? wanaonuka ni kwa sababu hawajui kujisafisha.Kama mwanamke hajisafishi au sio msafi kiujumla ndio ananuka na hata kupata fungus.

Mkubali mkatae wanaume nao wana machaguo yao, kama ni wembamba ua unene, kila mtu ana chaguo lake...ila ziwa na tako ndio mpango mzima. 

ukiwa kimbau mbau hata ukipita hustui watu.

Subirini sifa ya wanawake wembamba asanteni sana sifa kwenu wanene.

JK APIGA MARUFUKU, UKAWA WANASA WARAKA MZITO


Dar/mikoani. Wakati Rais Jakaya Kikwete akipiga marufuku vyama vya siasa na asasi za kiraia kufanya mapema kampeni za kuhamasisha wananchi kuhusu Katiba Inayopendekezwa, Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) umenasa waraka wa mkakati wa kutumia Sh2.5 bilioni za umma kuipigia debe katiba hiyo.
Pamoja na kauli ya Rais Kikwete aliyoitoa jana wakati akilihutubia Taifa kupitia wazee wa Dodoma, Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein jana hiyohiyo, aliwataka Wazanzibari kuipitisha Katiba Inayopendekezwa bila kufanya makosa.
Nyuma ya kauli hizo za marais, Ukawa umesema umeandaliwa mkakati kabambe wa kuvitumia vyombo vya habari kwa fedha za umma kutoka Ikulu kuwashawishi wananchi kupigia kura ya ‘ndiyo’ katiba hiyo.
Kauli ya Rais Kikwete
“Kwa sababu hiyo naomba Watanzania wenzangu tuzingatie mamlaka ya Sheria ya Kura ya Maoni ambayo imeelekeza vizuri lini kura ya maoni itafanyika na lini kampeni zitafanyika, lini wadau watatoa elimu naomba tuwe na subira. Tukizingatia sheria hii hakuna ugomvi.”
Aliongeza hadi Tume itakapotoa maelekezo ya utekelezaji, wakati wa kampeni na kutoa elimu kwa umma bado na kwamba sheria ipo na imezipanga siku maalumu za kufanya hivyo.
Alisema licha ya sheria kuruhusu kampeni kufanyika ndani ya siku 60 kabla ya kura za maoni kupigwa, kwa mamlaka yake akiwa kiongozi wa nchi, kura na kampeni vitafanyika ndani ya siku 30 tu.
“Kampeni zitaanza tarehe 30 Machi na kumalizika tarehe 29 Aprili ikiwa ni siku moja kabla ya kupiga kura ya maoni. Muda huo ndiyo utakuwa wa kufanya hivyo,” alisema Kikwete.
Dk Shein aipigia debe
Wakati Kikwete akisema hayo, Dk Shein amesema Katiba Inayopendekezwa ni mwarobaini wa kero nyingi za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na Wazanzibari wasifanye makosa kuikataa wakati wa kura ya maoni mwakani.
Akizungumza katika kongamano la kuadhimisha miaka minne ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, Dk Shein alisema iwapo Katiba hiyo itapitishwa, itasaidia kuimarisha Muungano kwa kuwa imezingatia makubaliano ya Muungano ya kuwa na Serikali mbili.

UKAWA WADAI WAMENASA WARAKA WA IKULU


ukawa hawa
SHABANI MATUTU NA PATRICIA KIMELEMETA

UMOJA wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) umedai kunasa waraka wa Ofisi ya Rais Ikulu unaoonyesha Serikali imetenga Sh bilioni 2.5 kwa ajili ya kampeni ya kuwezesha Katiba inayopendekezwa ipitishwe   kwa kupigiwa kura ya ndiyo katika kura ya maoni.
Katibu Mkuu wa Ukawa ambaye pia ni Katibu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, alidai Dar es Salaam jana  kuwa kampeni hiyo itafanywa kupitia vyombo vya habari  kuwahamasisha wananchi waweze kupiga kura ya ndiyo na kuipitisha kwa urahisi Katiba inayopendekezwa.
Waraka huo alidai kwamba unatoka Ikulu kwenda kwa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo na kuelekeza kazi hiyo inatakiwa kuanza wiki hii zikipatikana Sh milioni 50 za kuanzia.
“Ofisi ya Rais Ikulu imetenga Sh bilioni 2.5 kwa ajili ya kuhamasisha wananchi waweze kuipigia kura ya ndiyo Katiba pendekezwa.
“Lengo ni kutaka kuipitisha Katiba hiyo bila ya kuwaelimisha wananchi jambo ambalo ni kinyume na sheria,” alisema Dk. Slaa.
Alisema suala hilo ni kinyume na sheria kwa sababu  wanaohusika na utangazaji au uhamasishaji wa Katiba mpya ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na siyo Ofisi ya Rais Ikulu.
Alidai ofisi hiyo imeandaa Kamati ya Kudumu ya Habari ya kusimamia mpango wa kuelimisha umma hadi muda wa kura ya maoni.
VYOMBO VYA HABARI
Dk. Slaa alidai baadhi ya vyombo vya habari vimetengwa kwa ajili ya kazi hiyo zikiwamo redio,   magazeti, mitandao ya jamii na televisheni mbalimbali   kuhakikisha mpango huo unafanikiwa.
Alidai wahariri wa vyombo hivyo wametengewa fedha kuhakikisha wanatumia vyombo vyao kutenga vipindi vya kutoa elimu kwa wananchi juu ya suala hilo.
Dk. Slaa alidai vipindi hivyo vitaongozwa na baadhi ya watu walioandaliwa kufanya kazi hiyo wakiwamo wasomi kutoka vyuo vikuu nchini; baadhi yao ni wale waliokuwa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba.
WASOMI
Dk. Slaa alidai  wasomi hao watalipwa Sh 500,000 kwa kila kipindi watakachoshiriki katika muda wa wiki 22  kuhakikisha suala hilo linafanikiwa.
“Wameamua kuwachukua baadhi ya wasomi kutoka vyuo vikuu, tena baadhi yao walikuwa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kuendesha vipindi hivyo  kwenye media mbalimbali nchini,” alisema.
NGOMA, VIKUNDI VYA UTAMADUNI
Dk. Slaa alidai katika kampeni hiyo pia zitatumiwa    ngoma na vikundi vya utamaduni vya asili wakiwamo   maofisa utamaduni wa maeneo mbalimbalia kwa ajili ya kuvikusanya pamoja vikundi hivyo.
Njia nyingine alizitaja kuwa ni kubandika mabango katika miji mikuu ya mikoa kuongeza uelewa wa Katiba inayopendekezwa ili wananchi waipigie kura ya ndiyo.
Alipotafutwa kwa simu kuzungumzia madai hayo, Mkurugenzi wa Mawasiliano Ofisi ya Rais Ikulu, Salva  Rweyemamu alisema; “nitakupigia baadaye”.
Hata hivyo hakuweza kupiga na alipotafutwa mara kadhaa baadaye simu yake haikupatikana hadi tunakwenda mtamboni.
MTANZANIA