|
Mwili
wa aliyekuwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Simba wa Yuda Yunis Festo
aliyefariki dunia siku ya Jumatatu wiki hii saa 11 alfajiri muda
mchache kabla ya kuanza kufanya mtihani wa kuhitimu kidato cha nne mwaka
2014
Eneo la msiba wa aliyekuwa mwanafunzi wa shule ya sekondari Simba wa Yuda Yunis Festo
Mwili
wa marehemu Yunis Festo ukiwa umebebwa kwenye jeneza tayari kwa mazishi
nyumbani kwao na mwanafunzi huyo katika kijiji cha Igembe wilaya ya
Kwimba mkoani Mwanza
mwili wa marehemu ukiwa kwenye jeneza wakati wa ibada ya mazishi mchana huu kabla ya mazishi
Watu mbalimbali wenye mapenzi mema wakifuatilia ibada ya mazishi
Watu mbalimbali wenye mapenzi mema wamejitokeza katika mazishi hayo
Mmoja wa walimu wa mwanafunzi huyo bwana Damian Kageba Kupimo akiwa msibani leo
Jeneza la marehemu
mwili wa marehemu ukipelekwa makaburini kwa ajili ya mazishi
 |
| Mwanafunzi
Yunis Festo enzi za uhai wake.Hii picha alipiga tarehe 1,Novemba 2014
siku ya mahafali ya shule ya sekondari Simba wa Yuda |
Mazishi ya mwanafunzi
Yunis Festo aliyekuwa anasoma kidato cha nne katika shule ya sekondari
Simba wa Yuda iliyoko katika kijiji cha Bulima wilaya ya Busega
yamefanyika mchana huu katika kijiji cha Igembe wilaya ya Kwimba mkoani
Mwanza .
Watu
mbalimbali wenye mapenzi mema wakiwemo walimu,wanafunzi,viongozi wa
dini na wakazi wa kijiji hicho na wengine kutoka mikoa ya jirani
wamehudhuria mazishi hayo.
Ibada ya mazishi imeongozwa na mchungaji Josephares Ihoneyo Mtebe.
Yunis
Festo aliyezaliwa tarehe 26.02.1996 amefariki dunia juzi saa 11
alfajiri zikiwa zimesalia saa tatukuanza kufanyika kwa mtihani wa
kidato cha nne kote nchini ulioanza juzi Jumatatu.
Malunde1
blog iliiambiwa kuwa mwanafunzi huyo amefariki dunia juzi baada ya
kukimbizwa katika kituo cha afya Bulima na wanafunzi wenzake aliokuwa
nao bwenini alipozidiwa majira ya saa 9 usiku wa kuamkia siku ya
Jumatatu.
Habari zinasema kuwa mwanafunzi huyo alikuwa anaumwa kichwa na kwamba alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa Sickle Cell.
Malunde1 blog inawapa pole ndugu,jamaa na marafiki waliofikwa na msiba huo.
Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Yunis Festo.Amina
No comments:
Post a Comment