Tuesday, 20 January 2015

MUME AUA MKE WAKE KWA KUMCHOMA CHOMA KWA VISU MWILI MZIMA AJARIBU KUJIUA YASHINDIKANA HUKO TABORA



Marehemu Zuhura Juma (31) baada ya kuuliwa na mumewe.


 
 
DUNIA inazidi kwenda kubaya! Mwanaume aliyejulikana kwa jina la Maulid Mussa (35), mkazi wa Kijiji cha Igoko wilayani Uyuwi, Tabora anashikiliwa na jeshi la polisi kwa madai ya kumuua mkewe, Zuhura Juma (31) kwa kumchoma visu sehemu mbalimbali za mwili.

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea saa tisa usiku wa kuamkia Jumatatu ya Januari 12, mwaka huu katika Kijiji cha Usagala Kata ya Magengati Tarafa ya Puge wilayani Nzega, Tabora nyumbani kwa wazazi wa mwanamke huyo.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, Maulid alifikia uamuzi huo mgumu baada ya mkewe kumuuliza habari alizozisikia kuwa aliuza shamba la tumbaku la familia bila yeye kujua hali ambayo haikumpendeza mwanaume huyo.


 
 
Bw. Maulid Mussa (35) anayetuhumiwa kumuua mkewe na kujichoma kisu mwenyewe.

Baada ya taarifa hizo  mwanahabari wetu alifika kwenye kijiji hicho ili kupata maelezo ya kina kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo.

Kwa mujibu wa shuhuda, siku moja kabla ya tukio, Maulid alimfuata marehemu kwa wazazi wake alipokimbilia baada ya mzozo wa shamba akimtaka arudi nyumbani kuendelea na maisha.

Alipofika, alimkuta mkewe na watoto wao wanne wakila. Alikaribishwa chakula cha mchana, akajumuika.

Siku iliyofuata alimweleza mkewe sababu ya yeye kumfuata ni kutaka arejee nyumbani, lakini mke alikataa kwa vile wazazi wake walikuwa nje ya kijiji hicho.

MUME AWAFUATA WAZAZI
“Baada ya Maulid kupewa maelezo hayo, alichukua uamuzi wa kuwafuata wakwe zake katika Kijiji cha Busondo ambacho ni jirani na kijiji hicho, akawaeleza lengo la safari yake ambapo wakwe hao walimwambia arudi kijijini akawasubiri.”

 
 
 ALA CHAKULA CHA MWISHO NA FAMILIA
“Maulid alirudi katika kijiji cha wakwe zake. Ilikuwa jioni, akamkuta mkewe ameandaa chakula cha jioni, walikula wote na watoto wao kisha akaaga kwa furaha kwamba anarudi nyumbani kwake,” alisema shuhuda mmoja akiomba jina lake kusitiriwa.

MTOTO WA KAKA WA MAREHEMU ASIMULIA
Shuhuda mwingine wa tukio hilo ni mtoto wa kaka wa marehemu ambaye naye aliomba jina lake lihifadhiwe, yeye alisema:

“Usiku wa tukio nilisikia sauti ya mtoto akilia kuashiria kuna tatizo, nikaamka na kutoka nje ili kujua kuna tatazo gani.
“Nilipofika nje niliona baiskeli ya mume wa marehemu ikiwa imeegeshwa kwenye nyumba aliyolala. Sikuwa na wasiwasi.

 
 
“Lakini muda mfupi baada ya kurudi ndani nilisikia sauti ya mwanamke akiomba msaada eneo la nyuma ya nyumba aliyolala marehemu. 
Alikuwa akisema, ‘jamani nauawa, naomba mnisaidie nakufa! Nakufa!’ Nikatoka nje na kwenda ilikokuwa ikitokea sauti.
 Nilishtuka kumkuta Zuhura amelala chini huku akiwa ametapakaa damu na majeraha mgongoni na shingoni. “Nilipiga kelele kuomba msaada, watu wakaja. Ndipo tukaanza kumfuatilia Maulid kwani niliwaambia niliiona baiskeli yake nje ya nyumba.

“Tulimkuta Maulidi kichakani naye akiwa ametapakaa damu. Kumbe alijaribu kujichinja mwenyewe shingoni kwa lengo la kujimaliza baada ya zoezi la kujiua kwa kunywa sumu kushindikana ambapo alitapika.”

BABA WA MAREHEMU
Naye baba wa marehemu Zuhura, Juma Ramadhani alipozungumza na mwandishi wa habari hizi kuhusu mauaji ya mwanaye alisema:


Marehemu Zuhura Juma enzi za uhai wake. 
 
“Kusema ukweli maumivu niliyoyapata kwa kuuawa mtoto wangu tena kikatili vile siwezi kuyatolea mfano. Mimi nachukulia mauaji haya kama kuidhalilisha familia yangu. Naiomba serikali itende haki kwa kutoa hukumu na adhabu kali kwa Maulid ili iwe fundisho kwa wanaume wenye tabia ya kufanya ukatili kwa wake zao.”

MWENYEKITI WA KIJIJI
Mwenyekiti wa Kijiji cha Usagali, Ally Said Mlenda alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo na aliyapokea kwa masikitiko makubwa.

HALI YA MTUHUMIWA
Wakati habari zinakwenda mitamboni, mtuhumiwa huyo yuko chini ya ulinzi katika Kituo cha Polisi Nzega akisubiri kupandishwa mahakamani kwa madai ya kumuua mkewe.
 
~Credit GPL

Hatari sana!! COASTER YAGONGANA USO KWA USO NA LORI,WATU ZAIDI YA 40 WANUSURIKA KUFA


 


Zaidi ya watu 40 wamenusurika kifo huku mmoja akikatika viungo vya  miguu na wengine kujeruhika vibaya baada ya lori  moja lilionekana kuwa ni la jeshi kugongana uso kwa uso na gari la abiria aina ya COSTA la Ubungo -Tegeta eneo la Tegeta jijini Dar es salaam.

Tukio hilo limevuta hisia za mamia ya wakazi wa Tegeta huku baadhi ya mafundi gereji wa Tegeta wakijaribu kutumia vifaa maalumu kukata mabati ya magari kwa nia ya kunasua baadhi ya majeruhi walionasa ndani ya COASTA hiyo kusuru abiria walioonekana kunasa katika vyuma vya magari hayo.
 Baadhi ya mashuhuda na dereva wa COSTA pamoja na kuomba eneo la kibaoni kuweka njia ya mzunguko maarufu kama ROUND ABOUT kwa lengo la kuepusha madereva wanao lazimika kugeuza kwa dharura katika njia kuu maarufu kama UTAN kutokana na njia hiyo kukosa fursa ya kugeuza endapo kuna ulazima wa kufanya hivyo.
 Pia wamemtupia lawama Dereva wa Lori kama msababisha ajali kwa kukosa hekima ya kuchukua tahadhari kabla ya kufanya hivyo.
Kamanda wa polisi mkoa kipolisi Kinondoni  Kamilius Wambura amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo akieleza kutoa taarifa mara baada ya uchunguzi kufanyika.
Via>>ITV 

AZMA - WANASUBIRI NIFE OFFICCIAL HD VIDEO

AZMA MUNGU INUSURU TANZANIA OFFICIAL VIDEO

WE NEVER GIVE UP - AZMA & DARKMASTER Mwanachemba

TUSI LA KWANZA TOKA KWA AZMA

AZMA FEAT ZUZAN LHOTOVA - BUSINESS PROFILE

AZMA FEAT KITA MY GIRLFRIEND IS MY BEST FRIEND OFFICIAL HD VIDEO

AZMA FEAT CIANA THE CLOSER I GET TO U OFFICIAL VIDEO

AZMA - KUWA NA AZMA

AZMA THE AFRICAN AMBASSADOR - KILA SIKU KILA KITU

AZMA feat Kita - Jinsi ya kumfikisha mpenzi wako (Official video Dirty v...

AZMA FEAT KITA KIPIMO CHA PENZI OFFICIAL HD VIDEO

AZMA feat Kita - Jinsi ya kumfikisha mpenzi wako (Official video Dirty v...

AZMA FEAT KITA & CANT DIDAS - UTATA WA KATIBA 2014 OFFICIAL VIDEO HD

AZMA & KITA - I KNOW WHAT U WANT OFFICIAL HD VIDEO

AZMA ft Kita - Jinsi ya kumfikisha mpenzi wako (teaser)

AZMA feat Kita - Jinsi ya kumfikisha mpenzi wako ( Official video clean ...

Friday, 9 January 2015

Afande Sele: Daz Baba havuti unga, anakunywa pombe kupita kiasi ndio maana kakonda na kuchakaa




10899566_521193114690641_1830059398_n




Afande
Sele amedai kuwa Daz Baba havuti unga kama watu wengi wanavyodhani bali
amekuwa akinywa pombe bila kuzingatia kula hali inayomfanya akonde. 

Akiongea na paparazi, Afande
amesema huu ni wakati wa wasanii na wadau wa muziki nchini kuonyesha
juhudi za kumuokoa katika hali hiyo ili kunusuru maisha yake.


“Tatizo sisi wabongo tunapenda kusema vitu vya unafiki hasa hasa sisi
wasanii,” amesema Afande. “Tunashindwa kusema vitu vya ukweli mwisho
wake tunaathirika zaidi. 

Mbona wasanii wengine wa nje wakifilisika wanasema wamefilisika ili waweze kuishi maisha ya kawaida?” amehoji Afande.

“Tatizo watu wanajikweza wakati hawana kitu. Kusema kweli hali halisi ya Daz Baba ni mtu ambaye kama kachanganikiwa hivi. 

Daz
Baba havuti unga. Wasanii acheni kuongea huu ndio wakati wa kumsaidia.
Daz Baba akinywa pombe hata bia mbili tu anabadilika kabisa na tatizo
lake Daz akinywa pombe hawezi kula, kwahiyo mara nyingi anakesha
anakunywa pombe, hachagui pombe. Kusema kweli Daz Baba ni mtu ambaye
kachakaa.


Mimi naapa Daz havuti unga ila ni mlevi kupita kiasi. Hana muda wa
kulala. Ukikutana naye sehemu unamwomba msamaha wewe kwa sababu bila
hivyo atakusumbua na haelewi anachoongea, kama vile chizi tu.

Wapo
wadau ambao wanajua Daz katoka wapi. Mimi mwenyewe binafsi
nimeshahangaika na Daz na kwa namna ya pekee lakini watu wengine
hawafikirii kama hili jambo ni la serious.”

“Toka naanza kubadilika mimi najaribu kumweka sawa. Kwasababu kama hali ngumu hata sisi hali ngumu tunahangaika tu. 

Watu
wengi wanasubiria mtu amekufa halafu waanze kutoa magari na michango.
Kwanini kama mnaweza kufanya juhudi hizo msifanye sasa hivi? Kwenye
mazishi watu wanajifanya kukodi magari kwenda kuzika, mtu kama Daz
kipindi hiki ndio cha kumsaidia. Wapo marafiki wa Daz, wasanii wadau
wanaweza kumsaidia sasa hivi.”

Penzi Kinyume na Maumbile Lamtesa Lungi









Msanii wa filamu za Kibongo, Lungi Maulanga, amesema kuwa mpenzi wake
amekuwa akimsaliti kila kukicha huku akihisi kuwa, huenda wanawake
anaowafuata huko nje wanampa mapenzi kinyume na maumbile.

 
Akizungumza Gpl Lungi alisema kuwa siku chache
zilizopita alilia sana kutokana na usaliti aliofanyiwa na mpenzi wake
aliyemhifadhi kwa jina, akasema aliamua kumsamehe kwa kuwa anampenda. 


 

“Naumia sana na nalia kila ninapokumbuka namna mpenzi wangu
anavyonisaliti, sielewi ni kwa nini wakati mimi ni mrembo na nina umbo
zuri ambalo kila mwanaume akiniona lazima anitamani.
 
“Nashangaa
mwenzangu anavyochepuka, sijui huko nje anawafuata wale wanaotoa
‘mtandao’?”
alihoji Lungi na kuongeza: “Mimi siwezi kumsaliti hata
iweje, najua huko nje magonjwa ni mengi.”


Baada ya Kupiga Show ya Nguvu Nigeria usiku wa leo, Diamond kasema haamini Macho yake



Staa Afrika Mashariki, Nasibu Abdul ‘Diamond’, amefunguka kwamba haamini kama kweli amepata nafasi ya kutumbuiza kwenye sherehe za utoaji tuzo za wanamichezo bora zilizoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ambazo zimefanyika usiku wa kuamkia leo jijini, Lagos, Nigeria.
  
Akizungumza na Paparazi, Diamond amesema amefurahi kupata nafasi ya pekee ambayo mara nyingi hutolewa kwa wasanii wakubwa Marekani na kuamini kwamba muziki wa Tanzania unathaminika kila kona.
  
“Nimefurahi maana hii inaonyesha jinsi gani muziki wetu umekuwa hadi kufikia Afrika kuwa moja ya kionjo hasa kwenye tamasha kubwa kama hilo, kiukweli sikuwahi kufikiria hapo mwanzo,” alisema Diamond.