Afande Sele: Daz Baba havuti unga, anakunywa pombe kupita kiasi ndio maana kakonda na kuchakaa

Afande
Sele amedai kuwa Daz Baba havuti unga kama watu wengi wanavyodhani bali
amekuwa akinywa pombe bila kuzingatia kula hali inayomfanya akonde.
Akiongea na paparazi, Afande
amesema huu ni wakati wa wasanii na wadau wa muziki nchini kuonyesha
juhudi za kumuokoa katika hali hiyo ili kunusuru maisha yake.
“Tatizo sisi wabongo tunapenda kusema vitu vya unafiki hasa hasa sisi
wasanii,” amesema Afande. “Tunashindwa kusema vitu vya ukweli mwisho
wake tunaathirika zaidi.
Mbona wasanii wengine wa nje wakifilisika wanasema wamefilisika ili waweze kuishi maisha ya kawaida?” amehoji Afande.
“Tatizo watu wanajikweza wakati hawana kitu. Kusema kweli hali halisi ya Daz Baba ni mtu ambaye kama kachanganikiwa hivi.
Daz
Baba havuti unga. Wasanii acheni kuongea huu ndio wakati wa kumsaidia.
Daz Baba akinywa pombe hata bia mbili tu anabadilika kabisa na tatizo
lake Daz akinywa pombe hawezi kula, kwahiyo mara nyingi anakesha
anakunywa pombe, hachagui pombe. Kusema kweli Daz Baba ni mtu ambaye
kachakaa.
Mimi naapa Daz havuti unga ila ni mlevi kupita kiasi. Hana muda wa
kulala. Ukikutana naye sehemu unamwomba msamaha wewe kwa sababu bila
hivyo atakusumbua na haelewi anachoongea, kama vile chizi tu.
Wapo
wadau ambao wanajua Daz katoka wapi. Mimi mwenyewe binafsi
nimeshahangaika na Daz na kwa namna ya pekee lakini watu wengine
hawafikirii kama hili jambo ni la serious.”
“Toka naanza kubadilika mimi najaribu kumweka sawa. Kwasababu kama hali ngumu hata sisi hali ngumu tunahangaika tu.
Watu
wengi wanasubiria mtu amekufa halafu waanze kutoa magari na michango.
Kwanini kama mnaweza kufanya juhudi hizo msifanye sasa hivi? Kwenye
mazishi watu wanajifanya kukodi magari kwenda kuzika, mtu kama Daz
kipindi hiki ndio cha kumsaidia. Wapo marafiki wa Daz, wasanii wadau
wanaweza kumsaidia sasa hivi.”
No comments:
Post a Comment