JAMBO limezua
jambo! Katika hali ya kushangaza, mgeni rasmi katika shughuli ya
kumbukumbu cha kifo cha aliyekuwa staa wa muziki wa Hip Hop Bongo,
Albert Mangwea ‘Ngwea’ amejikuta akichafua hali ya hewa.
Katibu
wa Mbunge wa Jimbo la Morogoro, Mourice Masala anayedaiwa kuchafua hali
ya hewa katika kumbukumbu ya marehemu Albert Mangwea ‘Ngwea’.Tukio
hilo lililoibua minong’ono ya aina yake lilitokea Mei 28, mwaka huu
katika Ukumbi wa Samakisamaki mjini hapa ambapo awali mgeni rasmi
alipangwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Aziz Abood.
Ilielezwa
kuwa, Abood aliyekuwa na majukumu mengine, alishindwa kufika hivyo
kumtuma katibu wake, Mourice Masala ambaye alichafua hali ya hewa kwa
kusema wasanii wasikubali kutumiwa na wanasiasa wala wasikubali
kubebeshwa mizigo na matajiri.
Marehemu Albert Mangwea ‘Ngwea’ enzi ya uhai wake.Mbali
na kauli hiyo, mwakilishi huyo akaenda mbele zaidi kwa kuwataka wasanii
waachane na skendo mbaya kwani kila kukicha jamii imekuwa ikisikia
mabaya yao. Hapo ndipo umati uliokuwemo ukumbini humo sanjari na ndugu
wa marehemu ukaibua miguno ya mshangao wengine wakihoji mgeni huyo
alikuwa akimaanisha nini kusema hivyo? au katumwa nini?
“Mh!
Sasa huyu mgeni inakuwaje anaanza kuwananga wasanii wasikubali kuwa
punda? Kwani nani alikuwa punda? Anataka kutwambia marehemu (Ngwea)
alikuwa punda? Anatuzingua huyu naye,” alisikika mmoja wa waalikwa.
Punda ni mtu anayebebeshwa mzigo wa madawa ya kulevya ‘unga’ kwenda kuuza kwingine.
Minong’ono hiyo ilidumu kwa muda kisha baadaye hali ikakaa sawa na mgeni huyo akaendelea kuhutubia licha ya watu kumshangaa.
Ngwea aliyefariki dunia nchini Afrika Kusini, Mei 28, mwaka jana, Jumatato iliyopita alitimiza mwaka mmoja tangu kifo chake.
Hadi
sasa hati ya kifo chake haijatolewa hadharani licha ya familia ya
msanii huyo kufanya juhudi za kuisaka kwa wahusika bila mafanikio.