Mashabiki
wawashambulia Masanja na Diamond kwa kushindwa ‘hata’ kutoa pole kwa
misiba 3 YA Bongo Movie.WAO WANAPOST TU picha za bataNI NCHINI
Marekani..MASANJA AJIBU TUHUMA KWA KUMWAGA MATUSI.."fyokofyokomsibani"
Instagram leo utakutana na post nyingi za R.I.P George Tyson katika
akaunti za wasanii wengi wa bongo movie na wa muziki, pamoja na wadau
mbalimbali wa burudani, ingawa hakuna dalili za huzuni katika akaunti ya
Diamond na Masanja zaidi ya picha za bata nchini Marekani.
Mashabiki
wa muigizaji wa Ze comedy, Masanja Mkandamizaji pamoja mashabiki wa
msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz wameshindwa kuvumilia kuona
hawajihusishi hata kwa kutoa pole katika kipindi cha majonzi ya misiba
mitatu iliyoongozana wiki mbili zilizopita katika akaunti zao za
mitandao ya kijamii.
Ndani
ya wiki mbili zilizopita tasnia ya burudani Tanzania imepoteza watu
watatu muhimu upande wa bongo movie, ambao ni muongozaji wa filamu Adam
Kuambiana aliyefariki May 17, ukafuatia msiba wa muigizaji Rachel
Haule aliyefariki May 26, na muongozaji wa filamu George Tyson
aliyefariki jana May 30 kwa ajali ya gari.
Chanzo
cha mashabiki hao kuwashambulia Diamond na Masanja ambao wote wako
Marekani kwa sasa kutokana na jinsi ambavyo wamekuwa wakipost picha za
kula bata zaidi hata wakati ambao watu wana huzuni ukizingatia wao ni
watu maarufu, pia ni wasanii na wanafuatiliwa na watu wengi kama kioo,
pia misiba iliyotokea inawahusu pia sababu waliofariki ni wasanii
wenzao.
Katika
akaunti za Instagram za Masanja na Diamond ndani ya wiki mbili hadi
leo hakuna yeyote kati yao aliyepost kitu chochote kuhusu msiba wa Adam,
Rachel wala Tyson, huenda ndio kilichowaudhi na kuamua kuwapa makavu
live.
Masaa
11 yaliyopita Masanja amepost picha akiwa anataka kupanda ndege
kuelekea North Carolina, na masaa 5 yaliyopita amepost picha akiwa
amefika na kuandika ‘Asante Mungu North Carolina’s Safe!’
Hizi ni baadhi ya comments za mashabiki wa Masanja:
angiellyicious
– Hvii wewe unajua kama wasanii wenzako huku wana misiba au unakula
raha tuu huko huna habari tena na kwenu!?? @mkandamizaji si uonyeshe
japo kwa ku fake kuwa unahuzunika we ni mipicha ya raha tuuuu!!! 3h
sikudhanimtambo – Yaani huyu yeye ni mipicha ya batani tu,,,kasahau hata kuna kufa,,,wenzio wako misibani
rewardmassawe
– Mimi Kila cku nawaambia Masanja ni POPOMPO kaz yake kupost pic zake
za bata tu wenzako huku ni misiba tu bwege wewe au unazani wewe hutokufa
bintijuma11 – ila kweli jamani utasema askii taarifa za misiba hata pole za uongo huna kaka
bintijuma11-
@dalila022 tatizo sio kupost picha za marehem we jiulize ndani ya hz wk
mbili imetokea misiba mingapi na yeye muda wote anapost yuko happy tu
hata kama aimuumi inabd awe soni kwa pindi mpendwa so kuturushia vipicha
vyake vya bata
sikudhanimtambo- Tunampenda but hata kama hajali mambo ya misiba azuge tu kuhuzunika,,,,au ye ataish milele mwenzetu
Baada ya Diamond kupost picha hii alfajiri ya leo na kuandika ‘Crazy Hunh…?’ hizi ni baadhi ya comment za mashabiki:
Kimatire- Ww dogo ulizaga kwanza hbr za nymbn cyo unatupia ma uchafu yako wkt wenzio wapo kwny maombolezo..punguza sifa
misspopote – Hivi huinag misiba au kwa vle n bongomovie nawe n bongofleva…..??inamaana wote hawakugusi @diamondplatnumz
kimatire
– Hata mkimtetea lzm aambiwe”’sifa hazijengi’ huo muda wa kupost huo
‘uchafu”’angeutumia kutoa pole’kwa hli nitukaneni matusi yote”’jpo
shabiki wake lkn muhmu kumwambia ukwel
hawamafixhbaby
-Una habar na misiba unafany yko2 ujui kexho itakuaje platnumz ss
2nakupend lakin misiba unaipotezea cijaona hta pich yk moj una andik
kuhus misiba pexa za kwak2 unasiaxh hp hp ndug watasi2mia kuwa na huruma
kk nyang???????????
Hata hivyo baada ya madongo hayo, Diamond aliamua kuwa mwerevu kwa kufanya kile mashabiki wake walimtaka afanye kwa kuandika:
Najua
tumekuwa tukipitia kipindi kigumu sana hivi karibuni.. kuondokewa na
ndugu zetu ambao tunawapenda na kuwategemea kwenye sanaa na mambo
mbalimbali.. kiukweli ni pigo na Pengo kubwa kwa Taifa… lakini skuzote
tunaamini Sisi tuliwapenda ila Mwenyez mungu aliwapenda zaidi… Maombi
yetu ndio yatakayo wasaidi walipo wapumzike kwa Amani….Mwenyez mungu
azilaze roho zao mahala pema peponi Amin
Naye Masanja Mkandamizaji amejibu tuhuma hizo kwa kuandika:
Naona kuna watu wanahoji mbona siweki picha ya Misiba Inayotokea. JIBU
MAISHA NI MIPANGO NA MAAMUZI NILIAMUA SITAWEKA PICHA YA MSIBA WOWOTE
ISTAGRAM KWA MAANA HAISAIDII CHOCHOTE, NILIFIWA NA DADA YANGU NA MDOGO
WANGU WA MWISHO NA SIJAWAHI WEKA INSTA. NACHOJUA NI KWAMBA YANAPOTOKEA
HAYA NI KUMSHUKURU MUNGU KWA KILA JAMBO,TENA SIO KUMSHUKURIA INSTA
UNAMSHUKURU MOYONI WAKO. SO NIWAOMBE MLIOKUWA MNASUBIRI NIPOST SITAPOST
NG’O!! NA KWA TAARIFA MSIBA WA ADAM NILIKUWEPO LIDAZ NA MCHANGO NIKATOA
LKN SIKUWEKA PICHA ISTAGRAM. SO HUWA SIONGOZWI NA WATU KUFANYA KITU.
NA NILIACHAGA BAADA YA KWENDA KWENDA KWENYE MSIBA WA NGWEA MORO NIKAWEKA
PICHA RAIA WAKAANZA OOOOH UNAUZA SURA. MALA MBONA SURA HAINA MAJONZI
HEE SA MNATAKA NIJIUMBE MWENYE SURA YA MAJONZI ILI NIMKOSOE MUNGU
ALIYENIUMBA HANDSOME JAMANI??? NEVER SITAWEKA PICHA ZA HIVYOOO INSTA.
HAPA NI MACHAPIII YA UNAITEDI MPAKA NAVYORUDI NIKAWAPE POLE WAFIWA.
NADHANI KAMA ULINIFOLOOOOOO KUPATA UPDATE ZA MISIBA. U BETTER GO TO
HELL. ETI KIOO CHA JAMIII(kwa ku bana pua moja na kidole) KIOO CHA JAMII
CHA BABAKOOO. … #ChekilihotubaKamaLaMheshimiwaRais#
#HarafuNimeliwekaKwaHerufiKubwaa#
#UsichezeNaMimiKwenyeExplanesheniiiii#
#HahahahaaaNaonagaCommentZaPichaZaMisibaUtasikiaSaAmewekajeKopeMsibaniAmevaajeMiwaniAmefyokofyokomsibaniYaanWaliofeliLifeWanashidaaaaa#
#KumbukaNaongozwaNaRoho#
#Over#
No comments:
Post a Comment