Saturday, 30 August 2014

PENZI LA MAINDA LAGOMBEWA NA WANAUME KIBAO





Staa  wa  Filamu  za  Kibongo  aliyeamua  kumpokea  Yesu, Ruth Suka  'Mainda'  amesema  amekuwa  akipata  wakati  mgumu  kumjua  mwanaume  wa  kweli  ni  yupi  ambaye  anaweza  kumuoa  na  ndoa  yake  ikawa  na  raha  badala  ya  majuto  kama  ilivyo  kwa  baadhi  ya  wasanii  wenzake....


Mainda  alisema  hakuna  kipindi  kigumu  kama  kujua  yupi  ni  mwanaume  sahihi  wa  kumuoa  na  hili  limekuwa  likiutesa  moyo  wake  japo  sasa  ameamua  kumwachia Mungu  wake  ili  amsaidie  kwani  kwa  akili  zake  ameshindwa...

"Hakuna  wakati  mgumu  kama  kipindi  cha  kumpata  mume  sahihi  kutoka  kwa  mungu, kwani  ukijichanganya  unaweza  kuchukua  mwanaume  ambaye  si  wako  na  kusababisha  kuwe  na  mafarakano  ndani  ya  ndoa  na  hili  ndio  linaumiza  kichwa  changu  kwani  mpaka  sasa  sijajua  ni  yupi  kati  ya  wengi  wanaohitaji  kunioa," alisema  Mainda

Msanii  huyo  alisema  anajifunza  mambo  mengi  kupitia  ndoa  za  watu  waliomtangulia  kwani  nyingi  zimejaa  vurugu  likiwemo  suala  la  kusalitiana  na  kuambukizana  magonjwa  ya  zinaa  kama  vile  Ukimwi  na  menginenyo, hivyo  naye  hatapenda  awe  miongoni  mwa  ndoa  hizo

habari kamili: WATU KUMI WAMEFARIKI DUNIA NA MAJERUHI SABA KATIKA AJALI MBAYA ILIYOTOKEA MBALIZI




Viti vikiwa vimeharibika baada ya ajali kutokea 


Hivi ndivyo ambavyo Daladala hiyo ilivyojibamiza muda mchache uliopita 


Eneo hili la ubavuni ndipo eneo ambalo Daladala hiyo iliingia na Kujigonga 


Gari hilo aina ya Tata likiwa limepaki pembeni Muda mchache baada ya kupata ajali hiyo


Askari wa usalama wa Barabarani akiwa anatazama na kuchunguza zaidi ajali hiyo


Eneo ambalo Daladala hiyo iliyofumuka 





Hivi ndivyo Daladala hiyo iliyokuwa ikitoka Mwanjelwa kuja Mbalizi ilivyo  Haribika Baada ya ajali hiyo.

ALIYELAWITIWA NA MWANAUME MWENZIE BAADA YA KUFUMANIWA AJIUA, MWENYE MKE AKAMATWA NA POLISI




Yule baba aliyelawitiwa bila kinga na jamaa wawili mwenye mke na rafiki baada yakufumaniwa juzi Mwananyamala Jijini Dar akiwa na mke wa jamaa guest...jamaa kwa fedheha yakufanyiwa unyambilisi huo na picha zake kuwa kwenye mitandao amejiua jana na tayari mmoja wa waliomfanyia unyama huo ambaye ni mume wa mke ambaye alifumania amekamatwa na polisi na mwenzake anatafutwa...picha ni chafu sana kuweka hapa.

Friday, 29 August 2014

Nuh Mziwanda wa Shilole alikopi kwa Nick Cannon na Mariah Carey? ( Cannon ana 33, Mariah ana miaka 44)....Sasa amepata fundisho



Mwimbaji wa Bongo Flava, Nuh Mziwanda aliwashitua wengi baada ya kujichora tattoo yenye jina la mpenzi wake ‘Shilole’, tattoo ambayo haifutiki daima. Kitu ambacho kiliwashitua wengi.
 
“Mimi nimefanya hivi kwa kupenda kwangu, sijalazimishwa na mtu. Nimejisikia kufanya hivi kwa sababu nampenda sana Shilole…tukiachana basi lakini mimi nitabaki nayo hadi nitakapoenda kaburini.” Alisema Nuh  Mziwanda
 
Hata hivyo, Shilole alisema kuwa hatajichora kwa kuwa Nuh kafanya hivyo na kwamba anashukuru kwa uamuzi wake kwa kuwa hakulazimishwa na ni ishara ya upendo wa kweli tofauti na aliowahi kukutana nao awali.
 
“Siwezi kusema ntafanya hivyo sijui na nini basi ni mapenzi tu na mimi siku nikiamua kufanya ntafanya kama ambavyo amefanya yeye. Kiukweli ana love ya ukweli kabisa tofauti na wanaume ambao nilikuwa nao, watu walikuwa wanapenda tu wasikie wanatoka na ShiShi kwa kutaka kutafuta kick na lakini Nuh kama Nuh ana upendo wa peke yake kabisa. Yaani hadi inafikia hatua nasema alikuwa wapi. Wanasema Mungu akitaka kukupa kitu hakuandikii barua.”-Shilole

Uamuzi wa Nuh Mziwanda unaendana na uamuzi alioufanya Nick Cannon na Mariah Carey mwaka 2008 walipojichora tattoo za kudumu kwenye miili yao baada ya kufunga ndoa. 
Nick aliandika mgongoni ‘Mariah’, na Mariah alijichora kipepeo chini ya mgongo na kuandika maandishi madogo ‘Mrs Cannon’.
 
“Kwangu mimi pete ni maalum na zinavutia, lakini tattoo zinamaana zaidi  ya kitu chochote. Ni za milele na milele…” Alisema Mariah Carey.

Hivi sasa Mariah na Nick Cannon wametengana na kwa mujibu wa vyanzo vya uhakika wanasubiri talaka tu.
 
Lakini wamebaki na alama za tattoo kwenye maisha yao ambazo hazitafutika daima hata watakapokuwa na wapenzi wengine.
 
Hata hivyo, tattoo inaweza isiwe kitu kama watoto wao mapacha ambapo pia ni kiunganishi kikubwa katika maisha yao.

Je, Nuh Mziwanda na Shilole wao watafikia hatua ipi? Je, watadumu kama tattoo ya Nuh Mziwanda au watayeyuka

BREAKING NEWS: WATU 10 WAFARIKI DUNIA KATIKA AJALI HUKO MBEYA!


Watu kumi wakiwemo watoto wawili, 
wamefariki dunia papo hapo na wengine 
saba wamejeruhiwa vibaya katika ajali 
iliyohusisha magari mawili.

Ajali hiyo imehusisha gari ndogo ya abiria 
maarufu daladala lenye namba za usajili T 
237 BFB aina Toyota Hiace na gari kubwa 
aina ya Fuso lenye namba za usajili T 158 
CSV.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo 
wamemwambia paparazihuru kuwa ajali hiyo imetokea maeneo ya Mbalizi baada ya Hiace iliyokuwa ikitokea 
Mbeya mjini kuelekea Mbalizi kulivaa Fuso 
ilikuwa ikiingia barabarani.
Hata hivyo majina ya majeruhi na marehemu 
hayajaweza kupatikana mara moja kutokana 
na kuwa katika hali mbaya ambapo Dereva 
wa Fuso akitokomea mara baada ya tukio.
R.I.P All na pole sana kwa familia

MTANGAZAJI LA CLOUDS FM (LOVENESS DIVA) AVUJISHA MESSAGE ZA ZITTO KABWE AKIMTONGOZA: HIZI HAPA


Ukishangaa ya musa utayaona ya firauni, hivi karibuni baada ya zitto kumkana Diva mtangazaji wa alla za roho wa clouds FM, Kuwa hajawahi kuwa naye kimapenzi na Diva amekuwa akijitangaza sana amekuwa naye kimapenzi, sasa Diva kamuanika hadarani ona hapo chini, ila duu huyu mwanamke ni kiboko,salaleeeeee


Kijana Avua Nguo baada ya Kufika Kilele cha Mlima Kilimanjaro



KIJANA Ben Boleyn aliamua kuvua nguo baada ya kufika kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro nchini chenye joto la kati ya sentigrade 10 hadi 12.

Ben alifanya hivyo baada ya kuwekeana dau la shilingi 500 na mwenzake miongoni mwa aliopanda nao mlima huo.

Kijana huyo mwenye miaka 18 alipanda mlima huo katika kuchangisha fedha kusaidia watoto wa kituo cha kulea watoto cha Acorns Children's Hospice kilichopo jijini Worcester nchini England.
Kwa kupanda mlima huo, Ben alikusanya pauni 600 ila baada ya kuvua nguo zake na kuweka picha yake mitandaoni alichangisha fedha nyingi zaidi.

Ben ambaye hujitolea katika kituo hicho alipanda futi 19,341 za Mlima Kilimanjaro kwa siku 9 akiwa na wenzake 7.
 
Ben ambaye ni mwenyeji wa Kingswinford, England alisema: "Kila mtu alifurahia kitendo nilichokifanya katika kilele cha Mlima Kilimanjaro na kuchukua picha zangu.
 
"Wazazi wangu walipigwa na mshangao mwanzoni, ila walipoona watu wanazidi kuchangia kwa wingi walinielewa maana nilifanya kitu tofauti."

Utata kuhusu gari la ulinzi wa Rais kuibiwa Kenya


Msemaji wa serikali amekanusha madai kuwa gari lililoibiwa lilikuwa la ulinzi wa Rais Taarifa za kutatanisha za kuibiwa kwa gari la ulinzi wa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta zimeibuka nchini humo.


Taarifa hii ilitolewa na baadhi ya vyombo vya habari ingawa msemaji wa Rais Kenyatta ameikanusha taarifa hiyo akisema kuwa gari lililoibiwa lilikuwa la idara ya polisi likiendeshwa na inspekta mkuu wa polisi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa Daily Nation ikimnukuu mtu anayesemekana kuwa dereva wa gari hilo la kifahari alilazimishwa kuvua nguo zake kabla ya kupokonywa gari hillo.Gari hilo lililokuwa lisemekana kuwa na uwezo wa kuhimili risasi, liliibiwa usiku wa Jumatano na kwamba aliyekuwa analiendesha gari hilo alikuwa afisa wa polisi.
Gari lenyewe lilikuwa na nambari ya usajili ya kibinafsi.
Ni gari la polisi au la Rais?
Kwa mujibu wa msemaji wa Rais, gari hilo aina ya BMW 735 la mwaka 2000, lilikuwa linaendeshwa na inspekta wa polisi alipovamiwa na wanaume wanne waliokuwa wamejihami karibu na eneo la Ruai viungani mwa mji mkuu Nairobi.
Msemaji wa Rais Manoah Esipisu amekanusha madai kwamba gari hilo lilikuwa moja ya magari ya ulinzi wa Rais Uhuru Kenyatta kama ilivyokuwa imenukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari
Bwana Manoah amesema kuwa Inspekta aliyekuwa anaendesha gari hilo aliporwa dola miasaba na simu yake gari hilo lilipoibiwa saa tatu usiku. Alitekwa na majambazi hao kwa karibu saa tano kabla ya kumwachilia usiku wa manane.
Alisema kuwa wezi hao walitoweka na gari hilo ambalo alisema hutumiwa kwa shughuli za polisi na kwamba tayari msako umeanzishwa ingawa gari hilo bado halijapatikana.
Kadhalika alikanusha kuwa gari hilo lilikuwa la ulinzi wa Rais na kwamba lenyewe lilikuwa na uwezo wa kuhimili risasi.
Visa vya wizi wa magari na utekaji wa madereva sio jambo geni nchini Kenya ila kilichowashangaza wengi ni kwamba je viopi gari la ulinzi wa Rais liibiwe?
Bwana Manoah amesema takwimu zinaonyesha visa vya uhalifu vimepungua hasa katika jiji kuu Nairobi katika miezi ya hivi karibuni na kwamba ulinzi unaendelea kuimarishwa.

chanzo:bbc

Zitto Kabwe Afunguka kuhusu Uhusiano wake wa Kimapenzi na Loveness Diva wa Clouds Fm



Kwa mara ya kwanza Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Zuberi Kabwe ameibuka na kuzungumzia uhusiano wake na mtangazaji wa Clouds FM, Loveness Malinzi ‘Diva’ na kufuta uvumi mzito uliokuwa ukizagaa kuwa wawili hao ni wapenzi.

Zitto alifunguka hayo juzi kupitia kipindi cha Mkasi kinachorushwa na Televesheni ya East Africa ambapo alikanusha kuwa hana uhusiano wowote wa mapenzi licha ya kudaiwa kutungiwa wimbo na mtangazaji huyo kama ishara ya penzi lao.“Mh! Kama yeye amenitungia wimbo sijui lakini mimi sina uhusiano naye wowote wa kimapenzi,” alisema Zitto.
 
Katika mahojiano hayo, mheshimiwa huyo alifungukia skendo nyingine inayomhusisha kutembea na staa wa Bongo Fleva, Mwasiti Almasi na kudai hakuna ukweli wowote juu ya ishu hiyo.

Alisema anaumia zaidi kusikia watu wanavyomhusisha kutembea na Mwasiti kupitia mitandao ya kijamii wakati hakuna ukweli wowote ambapo msanii huyo wanaheshimiana na kufanya naye kazi kwa karibu ili kumsaidia katika harakati zake za muziki.
 
“Naumia sana kusikia wakinisema na Mwasiti wakati yule ni dada yangu na mbaya zaidi ni mtu ambaye mara kwa mara nimekuwa nikimsaidia katika shughuli zake za muziki, hakuna kitu kingine zaidi ya ukaka na udada,” alisema Zitto.
 
Aidha, mheshimiwa huyo mbali na kungumzia mikakati yake ya kisiasa katika kipindi hicho, aliweka bayana kuwa ni baba wa mtoto mmoja kwa mkewe aliyemtaja kwa jina moja la Jack, wanamlea mtoto wao vizuri lakini suala la ndoa bado halijatimia.

Video Mpya: Prokoto- Victoria Kimani Feat. Diamond & Ommy Dimpoz



Victoria Kimani ameachia video ya ‘Prokoto’ akiwa na wakali wa Bongo Flava, Diamond Platinumz na Ommy Dimpoz. Imeongozwa na Kevin Bosco Jnr.
Itazame  hapo  chini

SMS za Usagaji za Aunt Lulu Zanaswa.....Zilikuwa zinaenda kwa binti wa kidato cha pili, Ukiziona hutaamini



Mama mmoja mkazi wa Sinza jijini Dar es Salaam, aliyejitambulisha kwa jina la Mama Zahara, ameibuka na madai mazito akimtuhumu msanii wa filamu ambaye pia ni mjasiriamali, Lulu Mathias Semagongo ‘Anti Lulu’ kumtumia ‘SMS’ za usagaji mwanaye aitwaye Zahara  ambaye ni denti wa kidato cha pili.

MSIKIE MAMA MWENYEWE
Akizungumza kwa hasira, Mama Zahara aliwaka: “Mimi nina mtoto huyu tu wa kike, anasoma boarding huko Tanga lakini hivi karibuni alirejea akidai wamepewa likizo ya wiki moja.
 
“Tangu huyu mtoto amekwenda boarding, nimebaini amebadilika sana, amekuwa na vijitabia ambavyo sivielewi hivyo nikawa namchunguza sana.
 
“Leo (Jumanne wiki hii) wakati niko jikoni nikasikia anaongea na mtu akiwa chumbani kwake, mazungumzo yale yalinitia shaka kwani kuna muda nikamsikia ‘akimkisi’ aliyekuwa anazungumza naye.
 
“Nilihisi kitu f’lani lakini nikasema nitamvizia nichukue simu yake nikiamini kama kuna kinachoendelea nitagundua, na kweli, alipotoka kwenda bafuni nikaichukua simu yake na kukutana na mambo ya ajabu.
 
“Nilinasa hizi sms ambazo zilinionesha waziwazi kwamba mwanangu anafanya vitendo vya kisagaji. Niliumia sana hasa ukichukulia kwamba nina binti huyo tu.

“Nilipoichukua ile namba, nikataka kujua kama kweli alikuwa anachati na msichana mwenzake au mwanaume, ikabidi nifanye kama nataka kumtumia pesa kwenye simu yake na hapo ndipo likaja jina la Lulu Semagongo.

“Nilishtuka kwani namjua huyu msanii tangu alipokuwa mtangazaji. Nilipompigia akanijibu kwa kifupi tu kwamba nimlee vizuri mwanangu na yeye hawezi kumfanyia vitendo hivyo, nikaona bora nije kwenu mtanisaidia.”
 
MESEJI ZENYEWE ZIKOJE?
Zahara: Natamani kufanya kale kamchezo, unaweza kunisaidia?
Anti Lulu: Nitumie pesa!
Zahara: Kiasi gani cha pesa? Pesa siyo tatizo, umenielewa lakini? Nataka tu…(kitendo kichafu).
 
Anti Lulu: Nitumie hiyohiyo, kwa muda huu nitumie 30,000.
Zahara: Sawa halafu tunaonana vipi?
 
Anti Lulu: Nitumie pesa muda huu, Jumamosi.
Zahara: Mbona mbali sana mpenzi, leo haiwezekani au hata kesho, pesa siyo tatizo.
 
Anti Lulu: Nitumie pesa basi.
Zahara: Subiri kidogo baby, simu yenye pesa iko kwenye chaji, usijali, nashukuru kwa kunionea huruma.
Anti Lulu: (kimya).
 
KESHO YAKE
Anti Lulu: Umeona ishu kunidanganya siyo?
Zahara: Siwezi kukudanganya mpenzi, ndiyo naamka nitakutumia ila usije ukanidanganya maana nina..., hiyo Jumamosi tunaonana wapi?
 
Anti Lulu: Tuta-meet (kukutana) Bondeni Hotel (ipo Magomeni, Dar), basi nitumie hiyo pesa.
Zahara: Nikutumie kwenye namba hii, vipi tutatumia vifaa?
 
Anti Lulu: Nitumie kwenye namba hii.
Zahara: Nijibu basi kama tutatumia vifaa au hivihivi…
 
Anti Lulu: Hakuna haja ya vifaa, mimi natosha…
Zahara: Haya natuma, nitafurahi sana.
 
Baada ya maelezo ya mama huyo kisha kuziona sms hizo, kweli zilionesha Zahara ndiye aliyekuwa akimshawishi Anti Lulu amfanyie kamchezo hako huku msanii huyo naye akionesha kuujua na kutaka apewe kwanza Sh. 30,000, Ijumaa lilimsaka Anti Lulu ili kupata maelezo yake ambapo alikuwa na haya ya kusema:
 
HUYU HAPA ANTI LULU
“Kusema ukweli huyo binti ndiye aliyekuwa akinisumbua kwa kunitumia sms za kunitaka.
 
“Alionekana kuuzoea na kuupenda sana sana huo mchezo, mimi sijawahi, ni two different things (vitu viwili tofauti).
 
“Inavyoonekana alitaka kunichafua kwani alinilazimisha sana, sijawahi kufanya huo mchezo na wala sifikirii hasa kwa binti kama mimi ambaye naamini wapo wanaume wanaonipenda, niingie kwenye usagaji natafuta nini?

“Huyo binti mwambieni anikome kabisa.”
 
Chanzo: Gazeti la Ijumaa/gpl

Pochi Yamuokoa Kajala Masanja kukaa nusu Uchi ili utamu wake usionekane



Msanii wa filamu, Kajala Masanja, hivi karibuni alijikuta akiwa kwenye wakati mgumu baada ya kukaa kwenye kiti na kuachia sehemu zake nyeti kiasi cha kuwatoa udenda baadhi ya wanaume.

Tukio hilo lilijiri mkoani Tanga wakati msanii huyo alipokwenda kwenye Tamasha la Fiesta, alipokaa kwenye kiti alijikuta akikaa vibaya mazingira yaliyomfanya ahangaike ili kuziba maeneo yake muhimu.
 
Kutokana na hali hiyo, alichukuwa pochi yake na kuiweka mapajani na kufanikiwa kujiziba, lakini licha kufanya hivyo alikosa raha.

Mbowe: Mimi ni Kisiki cha CHADEMA.....Ajitosa rasmi kugombea Uenyekiti wa chama hicho




Mbowe: Mimi ni Kisiki cha CHADEMA.....Ajitosa rasmi kugombea Uenyekiti wa chama hicho
[Image: 2.jpg]

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe jana alikabidhiwa fomu na makada wa chama hicho na kumtaka awanie tena kiti hicho, ombi ambalo alilikubali na kufungua milango kwa wanachama wengine ‘kupimana naye kifua’.

“Nafasi bado ipo, anayetaka kupima kifua na mimi ajitokeze. Tena nawaomba viongozi wangu msizuie fomu kwa anayetaka,” alisema Mbowe ambaye ameongoza chama hicho kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano.

Makada wa chama hicho kutoka maeneo mbalimbali nchini wakiongozwa na kada maarufu, Athuman Mzigo (Mapigo Saba) kutoka Kigoma, walikutana na Mbowe na kuwasilisha maombi yao ya kumtaka awanie tena nafasi hiyo.

“Kutokana na sifa za mwenyekiti wetu, tumechangishana Sh200 kila mmoja hadi zikafika Sh50,000,” alisema Mapigo Saba huku akishangiliwa na makada wenzake alioambatana nao na kuongeza:

“Tumemwomba mwenyekiti agombee nafasi hiyo kwa kuzingatia sifa; kwanza anaijua vizuri idadi ya Watanzania na matatizo yao, pili anaungwa mkono na watu wengi na amekisaidia chama kukua. Tulikuwa na madiwani 40 leo wamefika 500, wabunge watano leo 48. Halafu hana ubaguzi ndiyo maana ameunganisha vyama vya upinzani na kuunda Ukawa (Umoja wa Katiba ya Wananchi).”

Huku akichomekea maneno ya lugha ya Kiha, Mapigo Saba alisema kuwa maombi ya kumtaka Mbowe agombee pia yametolewa katika mikoa ya Rukwa, Manyara, Iringa, Njombe, Jimbo la Same Magharibi, Zanzibar, Mwanza na Kilimanjaro.

Hotuba ya Mapigo Saba ilifuatiwa na salamu kutoka kwa wazee wa wilaya za Kinondoni, Ilala na Temeke, Baraza la Wanawake (Bawacha) na Baraza la Vijana (Bavicha).

Akitoa salamu za Bavicha, mwenyekiti wa baraza hilo Njombe, Emmanuel Masonga alisema Mbowe ni sawa na Joshua aliyemalizia kuwaongoza wana wa Israel kuingia nchi ya Kanaani:

“Sisi Wakristo tunajua kuwa Mussa alianzisha safari ya Waisrael kwenda Kanaani, ila hakuwafikisha. Kina Mtei (Edwin), Kimesera (Victor), Bob Makani na wengineo walianzisha safari ya kwenda Ikulu, ila hawakutufikisha. Mbowe ni sawa na Joshua atakayetufikisha Ikulu,” alisema Masonga.

Mwenyekiti wa Bawacha Taifa, Susan Lymo alimsifu Mbowe akisema ameongeza hamasa ya wanawake kushiriki siasa katika chama hicho.

“Mwaka 2000, kulikuwa na mwanamke mmoja katika viti maalumu, mwaka 2005 waliongezeka na kufikia sita na mwaka 2010 wamefikia 26. Mwenyekiti pia ameufanya mwaka huu kuwa wa wanawake kitaifa na ameongeza hamasa ya wanawake kushiriki siasa,” alisema Lymo.

Mbali na viongozi wa chama, alikuwapo pia Sheikh Rajab Katimba kutoka Jumuiya na Taasisi za Kiislamu ambaye alimsifu Mbowe na kuomba agombee tena nafasi hiyo.

Mbowe akubali
Baada ya Mratibu wa Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), Nickson Tugara kummwagia sifa Mbowe, Mapigo Saba alimkabidhi fomu, huku makada wakiimba, ‘Jembe, jembe, jembe…”

Mbowe aliishukuru Kamati Kuu ya chama hicho kwa kupanga uchaguzi Septemba 14, mwaka huu ambayo ni siku yake ya kuzaliwa huku akiahidi kujenga chama imara.

“Mtaiona Chadema mpya ifikapo Septemba 14. Hiki chama hakitakufa na hatutamvumilia mtu yeyote wa kabila lolote atakayekivuruga,” alisema.

Mbowe alisema hajawahi kuomba kugombea uenyekiti wa chama hicho tangu aliponza mwaka 2000...

“Napata wakati mgumu ninapofikia wakati huu. Chadema ina watu mbalimbali wenye taaluma na uzoefu, kwa nini mimi? Makundi haya yaliyojitokeza kunichukulia fomu yanaweza kutafsiriwa na wapenda majungu kuwa nimepanga mimi.

“Leo ni mara ya tatu naombwa kugombea uenyekiti, sijawahi kuomba. Mwaka 2004, Mzee Makani aliniomba nikamkatalia, lakini akaunda kikundi cha wazee walionichukulia fomu.

"Mwaka 2005, chama hakikuwa na mgombea urais, awali alijitokeza Profesa Mwesiga Baregu lakini akajitoa, nikaambiwa nibebe mzigo. Mwaka 2009 nikaombwa tena kugombea.”

Alisema amedhamiria kujenga chama kimtandao na kimfumo ili kuondokana na mfumo wa kienyeji... “Huko nyuma wakati wa uchaguzi watu walipeana tu nyadhifa kiundugu tukadhani chama kimeongezeka. Lakini wakati huu uchaguzi umefanyika kwa miezi tisa.

"Tulisema hatuwezi kufanya uchaguzi wa Taifa bila kupata viongozi wa mkoa, wilaya, kata, kijiji na mtaa, kitongoji na shina.

Tumefanya uchaguzi, watu wamepima na kuona mambo magumu, mara unasikia wanakimbia wakisema wameacha uenyekiti, uache wakati chama kinakua?”

Aliyehisiwa kufa kwa ebola azua mjadala Geita....Alikuwa anatapika na kuhara damu, Mwili wazikwa na Serikali



Utata umegubika kifo cha Bertha Boniface (25) ambaye amefia Hospitali ya Wilaya Geita, kutokana na uvumi kuwa kifo chake kinatokana na ugonjwa wa ebola. Hata hivyo, madai hayo yamekanushwa na uongozi wa wilaya hiyo. 
 
Viongozi hao wamedai hakuna mgonjwa aliyekufa kwa maradhi hayo na wala ugonjwa huo haupo. Umesema Bertha alikuwa akihisiwa kuwa na dalili za ebola.
 
Akizungumzia uvumi huo, mganga mfawidhi wa Wilaya ya Geita, Dk Adam Sijaona alisema siku kumi zilizopita walimpokea mgonjwa kutoka mji mdogo wa Katoro ambaye alikuwa akitapika, kuharisha damu na kutokwa damu mdomoni na puani.
 
“Kutokana na hali hiyo, tuliamua kuchukua tahadhari. Tulimlaza kwenye chumba maalumu ili kumfanyia uchunguzi wa kina,” alisema Dk Sijaona.
 
“Tayari tumetuma sampuli Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa uchunguzi zaidi, kwa sababu hospitali yetu haina vifaa vya kupima ebola. Tumekaa na mgonjwa huyo lakini kwa bahati mbaya alifariki dunia Jumatano. Tunasubiri majibu ya mwisho, lakini uchunguzi wa awali unaonyesha inaweza isiwe ebola, hivyo watu wasiwe na hofu. Ugonjwa huo haujaingia mkoani kwetu.”
 
Hata hivyo, uongozi wa hospitali hiyo ulikataa kukabidhi mwili wa marehemu kwa familia kwa ajili ya maziko na badala yake ulizikwa na Serikali.
 
Dk Sijaona alitetea uamuzi huo wa Serikali kusika akisema ulitokana na kutojua sababu za kifo chake.
 
Mganga mkuu wa Wilaya ya Geita, Dk Noel Makuza alisema Bertha awali alikuwa akisumbuliwa na malaria, lakini siku tatu baadaye alianza kuharisha na kutapika damu nyingi.
 
“Inawezekana pia alikuwa na vidonda vya tumbo, hata hivyo katika vipimo tulibaini pia alikuwa na homa kali ambayo kitaalamu inajulikana kama haemorge fever inayoendana na ile ya dengue au ya bonde la ufa,” alisema.
 
“Lakini pia tulipokuwa tukimchoma sindano, damu ilikuwa inaganda na eneo husika linakuwa jeusi. Kwa sababu ya utata huo tuliamua kupeleka sampuli wizarani kwa ajili ya vipimo. Nina imani kuwa wiki hii majibu yatapatikana.”
 
Alisema kitaalamu iwapo ugonjwa huo ni ebola, ndugu wa Bertha waliokuwa wakimhudumia wataanza kuumwa au kuonyesha dalili baada ya siku nane.
 
Jumatano wiki hii ndugu wa Bertha walikwenda Hospitali ya Wilaya ya Geita wakitaka kuchukua maiti kwa ajili ya maziko, lakini uongozi wa hospitali ulikataa kwa sababu za kiafya.

Waliomba tena waruhusiwe hata kutoa heshima za mwisho, pia walikataliwa.


Walitaka kuelezwa sababu na chanzo cha kifo hicho, lakini walikataliwa hali ambayo imeendelea kuzua maswali kwa wakazi wilayani hapa.
 
Dk Makuza alisema mwili ulizikwa na maofisa afya ambao walikuwa na vifaa vya tahadhari, lakini waliruhusu ndugu watatu kushuhudia. mahali alipozikwa Bertha.

Ajinyonga shambani na kuacha ujumbe; “Nawaachia dunia yenu muishi miaka 110”



Mtu mmoja ambaye hakujulikana jina, amekutwa akiwa amejinyonga ndani ya kibanda shambani huku akiwa na karatasi iliyoandikwa ujumbe “Nawaachia dunia yenu muishi miaka 110”. 
 
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kibiki, Ally Hussein alisema kijana huyo mwanamume amekutwa saa mbili usiku akiwa amefariki na hivyo kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi Chalinze.
 
Alisema askari walifika na kuukuta mwili wa marehemu ukiwa umefungwa kamba ya katani na alipopekuliwa alikutwa mfukoni na karatasi yenye maandishi hayo.
 
Kaimu Kamanda wa Polisi Pwani, Mrakibu msaidizi, Athumani Mwambalaswa amethibitisha tukio hilo na kusema mwili wa marehemu ulichukuliwa na kuifadhiwa Kituo cha Afya Chalinze kusubiri uchunguzi wa daktari.
 
Hata hivyo, alisema bado haijafahamika mtu huyo ni mwenyeji wa kijiji kipi kwani hapo Kibiki hakuweza kutambulika na jitihada za kutafuta ndugu zake katika vijiji vya jirani zinafanyika. Chanzo cha kujinyonga bado hakijajulikana.

Polisi amgonga mtoto, Atoka nduki na kutelekeza gari



Polisi mmoja ambaye hakufahamika jina lake mara moja, aliyekuwa akiendesha gari kwa mwendo wa kasi, Jumapili iliyopita alimgonga mtoto wa kike, Zahara Almeda katika barabara ya Mji Mpya  mkoani  Morogoro.

Katika tukio ambalo mwandishi wa habari hizi alilishuhudia, mara tu baada ya kumgonga mtoto aliyekuwa akitoka sokoni kununua magimbi na mihogo, askari huyo aliteremka na kukimbia akiliacha nyuma gari lake lililokuwa bado halijazimwa, ambalo ndani yake kulikuwa na kofia yake.

Wananchi waliojawa na hasira baada ya tukio hilo walilizingira gari hilo na kutaka kulichoma moto, lakini busara za baadhi yao ziliwezesha kitendo hicho kutofanyika na baadaye trafiki alifika kudili na tatizo hilo
 
Mmoja wa watu walioshuhudia ajali hiyo iliyolihusu gari aina ya Toyota Baloon lenye namba za usajili T 5** AUE, alisema mtoto aliyegongwa alikuwa akitokea sokoni Mji Mpya, akiwa amebeba kikapu kichwani.
 
Mtu huyo aliyejitambulisha kwa jina la Sudi Kiwamba, alisema binti huyo alikuwa ameshavuka barabara, lakini wakati akijiandaa kuvuka msingi wa pembeni gari hilo lilimfuata katika jitihada za kumkwepa mwendesha pikipiki.

Hata hivyo, siku moja baada ya tukio hilo, mwandishi wetu alizungumza na baba mzazi wa mtoto huyo alisema mwanaye anaendelea vizuri na mtu aliyemgonga alikwenda hospitalini kumjulia hali kwani aliamini alikuwa amefariki.

MSANII AKOMBA VITU KWA BWANA’KE


Fatma Leonard 'akila kona'.
MSANII wa filamu Bongo, Fatma Leonard wiki iliyopita alinaswa na paparazi wetu akihamisha vitu vya ndani nyumbani kwa mpenzi wake huko Ubungo Makuburi jijini Dar es Salaam akidai kuchoshwa na maisha bila ndoa. Hata hivyo, paparazi lilikuta tayari mzigo wa fenicha umeshaondoka.
Msanii wa filamu Bongo, Fatma Leonard akifungasha virago kuianza safari.
“Nimemvumilia kwa muda mrefu sana, kila siku namkumbusha, sasa inaonekana kama ninalazimisha, nimeamua kuchukua vyangu kwa sababu nimempata mtu mwenye mapenzi ya kweli ambaye yupo tayari kunioa,” alisema Fatma akikataa kulitaja jina la mpenzi wake huyo anayempotezea muda.
Baba mwenye nyumba hiyo alimpigia simu mpangaji wake kumfahamisha kuhusu kuondolewa kwa mizigo hiyo, lakini alimtaka amuache achukue anachotaka, kitu kinachoonyesha aliridhia kitendo hicho kilichowavutia majirani wengi waliojazana kushuhudia.