Saturday, 28 February 2015

[1.2MB] KUANGALIA VIDEO MPYA ZA BONGO BONYEZA HAPA CHINI==>

 
 

Mtoto Christina Kusale (2) amelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala baada ya kufanyiwa ukatili na mama yake mzazi kwa kumkata sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia maumivu makali.
 
Amesema Ofisa Ustawi wa Jamii wa hospitali hiyo, Dk Rose Temu kuwa mtoto huyo ambaye anaishi Kinondoni alipelekwa na majirani baada ya kusikia akipigwa na mama yake.
Temu alisema waliingia ndani na kumkuta mtoto huyo akilia huku akiwa na majeraha yanayodhaniwa ya kisu na kumsababishia maumivu hayo.
“Mtoto Christina alifikishwa hospitalini hapa Februari 22, mwaka huu akiwa na majeraha mbalimbali kwenye mwili wake ambayo yalikuwa sehemu za usoni, mikononi, kwenye makalio, mapaja na mgongoni,” alisema Temu.
Alisema amelazwa wodi namba mbili akiendelea kupatiwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri.
Alisema mama wa mtoto huyo anashikiliwa na Polisi na uongozi wa hospitali unafanya utaratibu ili aende kwa ajili ya kuchunguzwa kama ana matatizo ya akili.

Wednesday, 25 February 2015

NEW SONG From V_SkillsMusic Hawatoshi

                                         https://www.hulkshare.com/trueboytanzania/v-skillsmusic-hawatoshi

JOYCE KIRIA ADAIWA MILLION 500


Mtangazaji wa Kipindi cha Wanawake Live, Joyce Kiria.
MTANGAZAJI wa Kipindi cha Wanawake Live, Joyce Kiria amepokea samansi ya mashtaka kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Dimani, Zanzibar, Abdallah Sharia Ameir (CCM) ambaye amedai amlipe fidia ya kumdhalilisha sh. Milioni 500 au amuombe radhi kupitia  kipindi chake.
Akiongea, Joyce Kiria alisema kuwa amepokea barua hiyo kwa mikono miwili na anawasubiri wanasheria wake ili waijadili.“Nilimpokea mke wa Mbunge aitwaye Hawa kama mwanamke mwenye matatizo ambaye alifika kutoa sauti yake ili watu wamsaidie mtoto wake mwenye ulemavu.
Baada ya kuongea naye nilimtafuta mheshimiwa ili kumpa nafasi naye aongee ya kwake kama wajibu wangu, lakini cha kushangaza yeye alinikamata na kunipeleka polisi, leo anasema nimemdhalilisha,” alisema Joyce .
Joyce anadaiwa fidia na Mbunge huyo kwa kuitangaza habari ya kumtelekeza mtoto mlemavu ambaye alilepelekwa kwenye kipindi chake na mkewe, Hawa Deusi.  

Shilole na Mchumba Wake Nuh Mziwanda Wachafua Hali ya Hewa Mtandaoni baada ya Kutupia Picha za Uchi


Mwigizaji na mwanamziki,  Zuwena Mohammed ‘Shilole’ ambae ni mama wa watoto wawili wa kike , akiwa na mchumba wake Nuh wamechafua hali ya hewa baada ya kutupia picha yaowakiwa uchi.
  
Nuh Mziwanda ndio alioibandika picha hiyo kwenye ukursa wake kwenye mtandao wa instagram na baada ya kuona watu wengi wanamshabulia aliamua kuibandua. 

Wapo walioona kuwa kitendo  alichokifanya Mziwanda labda ni kutokana na umri wake hivyo hayo ni baadhi ya matokeo ya kuwa na mahusiano  na mtu mtoto.
  
 Lakini pia wapo walioona kuwa wawili hawa wanatafuta KIKI tu ili media za hapa Bongo ziwazungumzie kama Zari na Diamond, ila pia wapo amabo wanaona hii iko poa  na haina tatizo.

KAMA ULIZANI WANAWAKE WAZURI HAWAFAI KUJIUNGA NA POLISI, BASI KAMA ULIKUA HUJUI HAWA NDO ASKARI WAREMBO ZAIDI NCHINI KENYA



Jeniffer Mulwa - Nairobi Area 1



Elizabeth Resa - Parliament buildings



Felista Safari - Wilson Airport



Judy Chemutai - Nairobi Area



Yasmin Abdi - Juja Police Station



Zidi Yusuf - Police Headquarters



Priscah



Priscah
Plus, representing the Kenya Police Band, here's everyone's favourite.





Friday, 20 February 2015

C-NEWS:MEZ B AFARIKI DUNIA

New AUDIO | Christian Bella - Ukimwona Remix | Download/Listen


MZEE MAJUTO NA WASANII WENZAKE WAMTEMBELEA MAMA ALIYEPOKONYWA MTOTO ALBINO NA KISHA KUUWAWA KIKATILI




BREAKING NEWS: MSANII WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA MEZ B AFARIKI DUNIA HIVI PUNDE


Msanii mez b amefariki dunia leo hii baada ya kuugua wa pneunomia... Taarifa za kuaminika kutoka kwa dada yake anayeitwa Rachel kuwa marehemu mez b amefariki akiwa kwao Dodoma .
Tutawaletea habari zaidi za msiba...

BREAKING NEWS: MFANYAKAZI WA GAZETI LA MWANANCHI APIGWA RISASI


Mfanyakazi wa Kampuni ya Mwananchi Communications, Patrick Pella.
MFANYAKAZI wa Kampuni ya Mwananchi Communications, Patrick Pella amevamiwa na majambazi wenye silaha na kupigawa risasi, kujeruhiwa na kisha kuporwa fedha zake mchana huu maeneo ya Tabata-Relini jijini Dar.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Pella anadaiwa kuporwa kiasi cha Sh. Mil 2 alizokuwa nazo akiwa ametoka kuzichukua kwenye mashine ya kutolea fedha (ATM) Tawi la NMB liliyopo jirani na Azam TV, Barabara ya Mandela.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala, Mary Nzuki.
Mtandao huu ulimtafuta Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala, Mary Nzuki kuelezea zaidi tukio hilo, lakini simu yake iliita bila kupokelewa.

BASI LA KIDIA LAPATA AJALI MBAYA YA KUGONGANA USO KWA USO NA LORI mchana huu dodoma


 Ajali mbaya imetokea mchana huu huko Mbande, Dodoma baada ya basi la Kidia One kugongana uso kwa uso na lori. Basi hilo limeharibika vibaya mno, inasadikika watu wengi wamepoteza maisha.


Oparesheni ya kuwasaka wauaji Morogoro yaanza


Jeshi la polisi mkoa wa Morogoro limeanza kufanya oparesheni ya kuwatafuta  watuhumiwa waliohusika na mauaji ya  watu  watatu  wakiwemo wakulima wawili na mfugaji mmoja,  kufuatia mapigano yaliyozuka kati  ya wakulima na wafugaji  katika bonde la matembele linalounganisha kijiji cha Mabwegere na Mbigiri wilayani kilosa mkoani Morogoro.
  
Mkuu wa wilaya ya Kilosa Elis Tarimo akizungumzia  tukio hilo wakati alipotembelea majeruhi  katika  hospitali  ya mission St Joseph  Dumila  amesema  mauaji hayo hayatavumilika na jeshi la polisi litahakikisha linawakamata waliohusika na tukio hilo.
  
Tarimo amewataja waliofariki dunia  kuwa ni Joseph Peter (26) mkulima, Rajabu Selemani (55) mkulima na Kaduru Kashu (30) mfugaji na wengine wamelazwa hospitalini hapo huku mmoja  akihamishiwa katika hospital ya mkoa wa Morogoro. 
  
Kufuatia tukio hilo mkuu wa wilaya ya Kilosa Elias Tarimo ametupia lawama  Wizara ya  Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuchelewa  kuleta wasuluhishi wa mgogoro huo kama serikali ilivyoahidi kwa lengo  la kuhakiki upya  mipaka ya vijiji  ili kuondoa migogoro ya wakulima na wafugaji, iliyodumu kwa muda mrefu. 
  
Nao majeruhi waliolazwa  katika hospitali ya Mission  Joseph  Dumila  wamelalamikia  serikali kushindwa kumaliza tatizo la migogoro ya wakulima na wafugaji.Nae muuguzi wa zamu  Melania Shayo amesema wakulima wawili walifariki dunia wakati wakipatiwa matibu  na  kukiri kupokea maiti moja ya mfugaji  aliyeuwawa wakati wa mapigano hayo.
  
Mapigano haya yamekuja siku chache baada ya nyumba 41  kuchomwa moto zikiwemo za  wakulima na wafugaji kufutia mgogoro wa ardhi katika kijiji cha mabwegere wilayani kilosa, ambapo mkuu wa wilaya aliwakutanisha wakulima na wafugaji kwa lengo la kumaliza mgogoro huo lakini hata hivyo mkutano huo  uligubigwa na mivutano  na wafugaji kuondoka kabla ya mkutano kumalizika..

Mwanamke Amuua Mwanamke Mwenzake kwa Kummwagia Mafuta ya taa na Kumchoma Moto baada ya Kumfumania na Mumewe



Mkazi wa kijiji cha Ibosa, kata ya Nyakato, Bukoba Vijijini, Amelia Richard (50) anatuhumiwa kumuua mwanamke mwenzake kwa kummwagia mafuta ya taa na kumchoma moto baada ya kumfumania na mumewe.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera,  Henry Mwaibambe  alitaja tukio hilo ni  la Februari 15, mwaka huu saa 3 usiku katika kijiji cha Ibosa kata ya Nyakata Bukoba vijijini.
  Alimtaja aliyeuawa ni  Pelagia Martin (46) aliyeunguzwa mwili mzima. Kamanda alisema mwanamke huyo alicheleweshwa kufikishwa Hospitali ya Mkoa hadi kesho yake; Februari 16 baada ya wanafamilia kuomba wayamalize bila kwenda Polisi.
  Makubaliano ya wanafamilia hao yalitokana na kile kilichoonekana kwamba  Amelia alimfumania Pelagia akiwa na mumewe,  Richard Bulebo (57) ndani ya nyumba yao.
  Kwa mujibu wa Kamanda, Februari 16 walipoona hali ya majeruhi inazidi kuwa mbaya, ndipo walifika katika Kituo cha Polisi mjini Kati wakiomba msaada.
  Polisi walimpeleka majeruhi huyo Hospitali ya Mkoa lakini alifariki kabla ya kupatiwa matibabu. Polisi inamshikilia Amelia na Bulebo kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo.

JKT Yawasuta Wahitimu Wanaotaka Kuandamana kudai Ajira



Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limewataka vijana waliomaliza katika jeshi hilo, kutambua kuwa walikula kiapo cha utii wakati wa kuhitimu mafunzo, hivyo suala la kuandamana ni kinyume na kiapo chao.


Vijana hao waliotumikia Jeshi la Kujenga Taifa Operesheni za nyuma na kumaliza mkataba wa miaka miwili,  wameambiwa shinikizo lao la kulazimisha ajira kwa kuandamana ni kinyume cha sheria za nchi.
Taarifa kwa vyombo vya habari, iliyotolewa na Makao Makuu ya  jeshi hilo, jijini Dar es Salaam jana, ilisema kipengele kimoja cha masharti ya kujiunga na JKT kinasema baada ya mkataba, wanapaswa kurejea nyumbani na hawapaswi kudai jeshi liwatafutie ajira.
Ilieleza kwamba masharti ya jeshi hilo, huwekwa bayana kwa vijana wanapojiunga na JKT. Vijana hao wanatakiwa  kujua masharti  hayo na taratibu  za  JKT na kuelewa kuwa JKT halitoi ajira.
Taarifa hiyo ilinukuu kipengele kimojawapo cha masharti, kinachosema“Kwa kipindi chote nitakachokuwa ndani ya Jeshi la Kujenga Taifa nitakuwa nafanya mafunzo ya kijeshi na ya stadi za kazi na maisha, na baada ya mkataba nitarejea nyumbani. Hivyo sitalidai Jeshi la Kujenga Taifa ajira, wala kulitaka linitafutie ajira/kazi”.
Ufafanuzi huo ulitolewa, kutokana na vijana zaidi ya 200 waliohitimu mafunzo ya JKT kuanzia mwaka 2000 hadi mwaka 2013, kutangaza hivi karibuni kuwa wataandamana wiki ijayo kwenda kwa Rais Jakaya Kikwete, kumweleza shida zao, ikiwemo kutokuwa na ajira tangu wamalize mafunzo.
Jeshi hilo lilisema ni vema vijana hao, wakatambua kuwa tatizo la ajira siyo kwao peke yao, ni tatizo la ulimwengu mzima Tanzania, ikiwemo hivyo wanashauriwa kutumia stadi za kazi kujiajiri wenyewe.
“Kutokana na dhumuni la kuundwa JKT  Taifa, halina dhamana ya kuajiri bali kufunza vijana wa taifa hili umoja, stadi za kazi na uzalendo baada ya hapo wawe wenye sifa za kuajiriwa hupata ajira katika taasisi mbalimbali za serikari na binafsi,” ilisema taarifa hiyo.
Hata hivyo, jeshi hilo limesema tangu  mwaka 2003 hadi 2014,  vijana 24,708 wameajiriwa katika vyombo  vya ulinzi na usalama. Kati ya hao, vijana 21,977 wakiwemo wavulana 17,307 na wasichana 4,670,  wameajiriwa na Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Kwa upande wa  Polisi,  vijana 3,965  wameajiriwa ambao kati yao, wavulana ni 2,943;  Magereza  wameajiriwa 2,139 kati yao wavulana ni 2,044; Zimamoto vijana 100 wavulana wakiwa  78 na taasisi zingine wameajiriwa vijana 592
Aidha, alisema vijana 1,622 wameajiriwa katika taasisi mbalimbali kamavile  migodi ya dhahabu ya Geita, Mamlaka ya Bandari na Shirika la Hifadhi la Taifa (Tanapa).
 Taarifa hiyo ilisema JKT  ilianzishwa Julai 10, 1963 kwa lengo la kuwaweka pamoja vijana na kuwapa malezi, kuhusu uzalendo na umoja ili kuondoa dalili za matabaka, zilizoanza kujitokeza katika jamii baada ya uhuru.
Serikali ilirejesha mafunzo ya jeshi hilo kwa vijana wa kujitolea mwaka 2001 baada ya kusitishwa mwaka 1994.
Alisema  masharti ya kujiunga na jeshi hilo kwa vijana wa kujitolea ni kuhakikisha wahusika wanafahamu masharti na  taratibu, ikiwemo kuelewa kwamba  JKT haitoi ajira.
Takwimu zinaonesha kuwa tangu kurejeshwa kwa mafunzo ya JKT mwaka 2001 hadi mwaka jana, vijana 104,594 wamejiunga na JKT wakiwemo wavulana 76,832 na wasichana 27,762.

Watu Wawili Wafariki Dunia Wakiiba Mafuta Kwenye Lori Lililopinduka jijini Mbeya...18 Wamejeruhiwa Vibaya



Takribani miaka 15 imepita tangu ilipotokea ajali  katika kijiji cha Idweli wilayani Rungwe mkoa wa Mbeya, iliyosababisha vifo vya watu walioungua wakichota petroli  kwenye gari lililopinduka.


Hata hivyo, tukio la namna hiyo limejirudia tena kijijini hapo na safari hii watu wawili, wamekufa na wengine 18 kujeruhiwa wakati wakichota mafuta  kwenye gari lililopinduka.
Lori hilo lilikuwa likisafirisha mafuta kutoka Dar es Salaam kwenda Malawi. Lilipinduka kijijini hapo juzi. 
Vifo hivyo viwili vya wakazi wa kijiji hicho, Maria Pajela (18) na Wiliam Pascal (38), vimetonesha makovu ya huzuni ya ndugu na jamaa wapatao 40 waliopoteza maisha na kulazimu miili  yao kuzikwa kaburi moja, kutokana na kuharibika zaidi na kushindwa kutambuliwa.
  
Akitoa taarifa juu ya ajali ya juzi  saa 3 usiku, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi  alisema waliofariki na waliojeruhiwa, walikuwa katika harakati za kuiba mafuta kutoka katika gari aina ya Scania  lenye namba za usajili T 891 AQZ likiwa na tela lenye namba T 821 ARF.
Alisema gari hilo mali ya Ailis Sanga, lilipakia petroli yenye ujazo wa lita 41,000, likitoka Dar es Salaam  kwenda Malawi. 
Lilikuwa likiendeshwa na Zawadi Nyato (46) mkazi wa Sae  jijini Mbeya akiwa na utingo wake, Frank Yohana (24) mkazi wa Mbozi.
Baada ya kufika kijijini hapo, liliacha njia na kupinduka. Dereva na utingo  waliokolewa na kupelekwa kituo cha Polisi Kiwira  kupata fomu namba tatu ya kwa ajili ya matibabu.
Kamanda alisema baadhi ya wakazi, walivamia lori hilo na kutoboa tangi la mafuta, hali iliyosababisha mafuta kuanza kumwagika na kusambaa maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye makazi ya watu.
  
Kwa mujibu wa kamanda, watu hao hawakujali hatari iliyokuwa ikiwakaribia, badala yake waliendelea kukinga mafuta kwa kutumia vyombo vyao zikiwemo ndoo, madishi, karai na madumu.
“Wakati wakiendelea na harakati za wizi huo,wakazi hao walijikuta wakiwa katika moto mkubwa baada ya lori hilo kulipuka na hapo ndipo wawili kati yao wakapoteza maisha na waliosalia kujeruhiwa vibaya,” alisema Kamanda.
Alitaja  majeruhi katika ajali hiyo,  ambapo wanaume ni 13 na wanawake watano ni Shukuru Kanzale (21), Nuru George (30), Asante Boniface (38), Joseph Jamson (18), Joseph Paschal (30), Siza Kanesa (22),Alex  Daud (35), Oscar Yosia (23), Traiphon Moasi (37) na Samson Mbwila (29).
  
Majeruhi wengine ni Veronica Elia (30), Dora Michael(35), Rabsen Ayub (26), Wasiwasi Spika (32), Asia Anon (20), Bahati Kyando (23),Christopher Erasto(32) na Melisa Sanane (50) wote wakazi wa kijiji cha Idweli.
Kati  ya majeruhi hao, 16 wamelazwa katika Hospitali ya Misheni  Igogwe na  wawili wamelazwa Hospitali ya Serikali Makandana, Tukuyu na hali zao zinaendelea vizuri.
Katika tukio  la mwaka 2000 katika kijiji hicho cha Idweli,  gari lililohusika  lilikuwa likitoka Dar es Salaam kwenda Malawi. Lilianguka kijijini hapo, kutokana na  utelezi katika mteremko unaoishia kwenye kijiji hicho.
Tukio lingine la watu kuungua moto nchini, kutokana na kutaka kujipatia mafuta ya bure, lilitokea  mwaka jana katika eneo la Mbagala Rangi Tatu, jijini Dar es Salaam la mwaka 2014.
  
Watu wanne  walipoteza maisha na wengine 21 kujeruhiwa vibaya baada ya kwenda kuchota mafuta yaliyokuwa yanamwagika wakiwa na ndoo, vidumu vya lita tano na vyombo vingine bila kuchukua hadhari.

Huddah the boss chick aonyesha kadi ya gari,ushahidi kuwa anamiliki Range Rover anayoendesha


Huddah-Range

Huddah The Boss lady wa Kenya aliyewahi kushiriki BBA amewanyamazisha wale walioponda kuwa gari amepewa tu atembele ni kwamba sio yake kwa kuweka wazi kadi ya gari yenye jina lake.
huddah-M
hudda 82

New AUDIO | Diamond Platnumz Ft. P - Square - NAKUPENDA | Download/Listen


Picha: Huddah Monroe achefua tena, atupia picha akiwa uc*i kitandani! (18+)


10982337_501544039986956_8689538412124604069_nHuddah Monroe ameshajikubali kuwa ni ‘good girl gone bad’ na ndio maana haoni tatizo kuweka picha akiwa kitandani kama alivyozaliwa.


Mrembo huyo wa Kenya amepost picha kwenye akaunti yake ya Facebook akiwa kitandani huku akiwa amejifunika na shuka sehemu ndogo tu ya mwili wake kuficha sehemu ny*ti.
Mashabiki wake hawakusita kumchana.

“Dnt you fear God?oh I like your beauty and en everything mash Allah but this idea of being naked subhanallah stop it.You are a good girl hudda you can change if you want,” aliandika Shankaroon A. Mohammed.

“Wajameni u mean ur whoring for real?? Oh my… please stop proving ppl right n be decent now that uv achieved what u wanted… n be quiet, if not for anything else then respect your clientèle. This is wrong,” ameandika Brenskie La’femme.

WAKUBWA TU...BOFYA PICHA HAPA CHINI AKIWA AMEPANU

New AUDIO | G NAKO Ft. JOH MAKINI - JUMA IKANGAA | Download/Listen


New AUDIO | YOUNG DEE & YOUNG KILLER MSODOKI - TUSAMEHE | Download/Listen




New AUDIO | Jux - NIKUITE NANI | Download/Listen


Official AUDIO | Nakupenda [i Love You] Iyanya X Diamond Platnumz | Download/Listen