Mtangazaji wa Kipindi cha Wanawake Live, Joyce Kiria.
MTANGAZAJI wa
Kipindi cha Wanawake Live, Joyce Kiria amepokea samansi ya mashtaka
kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Dimani, Zanzibar, Abdallah Sharia Ameir
(CCM) ambaye amedai amlipe fidia ya kumdhalilisha sh. Milioni 500 au
amuombe radhi kupitia kipindi chake.
Akiongea,
Joyce Kiria alisema kuwa amepokea barua hiyo kwa mikono miwili na
anawasubiri wanasheria wake ili waijadili.“Nilimpokea mke wa Mbunge
aitwaye Hawa kama mwanamke mwenye matatizo ambaye alifika kutoa sauti
yake ili watu wamsaidie mtoto wake mwenye ulemavu.
Baada
ya kuongea naye nilimtafuta mheshimiwa ili kumpa nafasi naye aongee ya
kwake kama wajibu wangu, lakini cha kushangaza yeye alinikamata na
kunipeleka polisi, leo anasema nimemdhalilisha,” alisema Joyce .
Joyce
anadaiwa fidia na Mbunge huyo kwa kuitangaza habari ya kumtelekeza
mtoto mlemavu ambaye alilepelekwa kwenye kipindi chake na mkewe, Hawa
Deusi.
No comments:
Post a Comment