Monday, 30 June 2014

Naibu Katibu Mkuu CUF Bara aliyechukua nafasi ya Julius Mtatiro anusurika katika ajali



Naibu Katibu m kuu mpya wa CUF pia Mbunge wa viti Maalum Magdalena Sakaya akimshukuru Mungu baada ya kunusurika katika ajali na Lori kwenye makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere Dar


DIAMOND AFAIDIKA NA MENGI TUZO ZA BET


Photo: Kupata Fursa ya kushare treatment, kunetwork na kubadili ideas na Wasanii ambao ulikuwa ukiwaona tangu mtoto unakua, na tangu unaanza muziki haujui utoke vipi... kiukweli ni jambo ambalo linatia Moyo na nguvu sana ili uzidi kupambana zaidi, kesho na keshokutwa Tasnia yetu nasi ifike kwenye kilele....! das me and my Boy Nelly at the @betawards red carpet... Wenyewe wa uswazi tunamuitaga "Nelly I love you" Mzee wa Plasta������... Cc @bet_intlDIAMOND ANENA HAYA............
Kupata Fursa ya kushare treatment, kunetwork na kubadili ideas na Wasanii ambao ulikuwa ukiwaona tangu mtoto unakua, na tangu unaanza muziki haujui utoke vipi... kiukweli ni jambo ambalo linatia Moyo na nguvu sana ili uzidi kupambana zaidi, kesho na keshokutwa Tasnia yetu nasi ifike kwenye kilele....! das me and my Boy Nelly at the @betawards red carpet... Wenyewe wa uswazi tunamuitaga "Nelly I love you" Mzee wa Plasta������... Cc @bet_intl



Photo: [Interview fupi na Shemeji yetu Karrueche kwenye Red Carpet ya @BETawards jana Mjini Los Angeles California....] Asante sana Sheria Ngowi kwa suti hii uliyonivalisha.....] Jus Me and Our Beautiful inlaw @karrueche at the @betawards red Carpert... Thank you so much @sheriangowi for this classy and Outstanding suit... I really Nailed it... Cc @bet_intl

VUNJA JUNGU GESTI,MUME WA MTU ACHEZEA KICHAPO



Jamaa aliyetajwa kwa jina moja la Lugali  akihusishwa  kuchepuka na mke wa mpangaji wake, akiwa amenaswa kwenye gesti moja maeneo ya Buguruni, Dar.

Vunja jungu! Saa kadhaa kabla ya kuanza kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, jamaa aliyetajwa kwa jina moja la Lugali ameibua sekeseke kwenye nyumba ya kulala wageni (gesti), kisa kikidaiwa ni mchepuko akihusishwa na mke wa mpangaji wake, 


Ndugu wa mume waliyefumania wakimdhibiti baba mwenye nyumba huyo.
mzee huyo alichomolewa kutoka chumbani huku damu zikimvuja baada ya kula kichapo kutoka kwa jamaa na ndugu wa mwanaume aliyedai kuwa jamaa huyo alikuwa anamsumbua mkewe.

Mke aliyekuwa akisumbuliwa, na ndugu wa mume wenye hasira wakizidi kumuadabisha mtuhumiwa.
Kwa mujibu wa mashuhuda, kabla ya jamaa hao kuingia chumbani humo kwanza walivunja mlango wa chumba hicho baada ya kupata idhini kutoka kwa msimamizi wa gesti hiyo kufuatia  baba mwenye nyumba huyo kukahidi kuwafungulia mlango ili wamchukue mke wa ndugu yao aliyedaiwa kuwa ndani na mzee huyo.

Baba mwenye nyumba akizidi kuchezea kichapo.
Walidai kwamba mzee huyo ambaye ni baba mwenye nyumba, alikuwa akimtolea udenda mke huyo wa mpagaji wake ambaye ni jirani yake huku akimsumbua mara kwa mara kwa simu na ujumbe mfupi wa SMS.
Ilidaiwa kwamba kufuatia usumbufu huo, mke huyo alimweleza mumewe lakini mumewe hakuamini kama kweli baba mwenye nyumba alikuwa  akimtaka mke wake kimapenzi.

Ilisemekana kuwa mume huyo alimweleza mkewe ili aamini kweli baba mwenye nyumba alipania kumtaka basi amkubali ili amkute naye gesti amkomeshe kwa tabia hiyo ya baadhi ya wenye nyumba ambao huwataka wake wa wapangaji wake.
“Nilimwambia mke wangu amkubali kwa sababu nilikuwa na nia ya kukomesha tabia yake ya kutongoza wake wa wapangaji wake, akamwita Buguruni ndipo nikawapigia ninyi waandishi wa habari ili mje mchukue ushahidi,” alisema mume huyo.
Baada ya kukutwa gesti humo, mzee huyo aliomba msamaha kwa mpangaji wake huyo na kuahidi kulipa fidia ambapo aliwaandikia cheki feki kisha akakimbilia Kituo cha Polisi cha Buguruni na kufungua shauri kuwa alitekwa, akapigwa kisha akapelekwa gesti.
Shauri hilo ambalo liliandikishwa kwa jalada namba BUG/RB 6182/2014- utekaji. Mzee huyo alidai kutekwa na mpangaji wake huyo na kumpeleka nje ya mji kisha kumpiga ili kuua soo.
Hadi paparazi tunaanua jamvi kituoni hapo, polisi walikuwa wakichunguza ili ukweli ujulikane. 

UDAKU: NDOA YA 3 YA DIDA YAVUNJIKA



Khadija Shaibu ‘Dida’ na Ezden Jumanne wakisikiliza mawaidha ya Bi. Hindu wakati wa harusi yao.

KIMENUKA! Siku chache kabla ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuanza, ndoa ya Mtangazaji wa Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani kupitia Radio Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ na mumewe anayepiga mzigo TV1, Ezden Jumanne inadaiwa kuvunjika.


Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho kililinyaka tukio zima nyumbani kwa mtangazaji huyo Mwananyamala-Manjunju, Dar, ishu hiyo ilijiri wiki iliyopita usiku ambapo majirani walimsikia Dida akilia lakini wakashindwa kutoa msaada kutokana na geti kufungwa.
“Tuligonga sana mlango lakini hakuna chochote ila baada ya muda tulimuona mume wa Dida akitoka nje na begi kisha akaingia kwenye Bajaj  na kuondoka, tukagundua walikuwa kwenye ugomvi,” kilisema chanzo hicho.
TATIZO NI NINI?
Chanzo kingine makini kimepenyeza madai kuwa ugomvi wa wawili hao uliibuka mara baada ya Ezden kuhoji juu ya mapato ya mkewe.
“Jamaa alikuwa anahoji mshahara na fedha ambazo mkewe anazipata katika shughuli za u-MC, alihoji pia kuhusu mwanaye kusoma Shule ya Saint Kayumba (hali ya chini) ndipo mtiti ulipoanzia,” kilisema chanzo hicho.
Bw. Ezden Jumanne akipozi.
EZDEN AENDEWA HEWANI
Baada ya kunyetishiwa ishu nzima, mwanahabari wetu, alimtafuta Ezden kwa njia ya simu na kumsomea madai hayo ambapo hakuwa tayari kufafanua zaidi, alijibu kwa kifupi:
“Elewa tu kwamba tupo kwenye matatizo na mke wangu ila kwa sasa siko tayari kulizungumzia.”
DIDA ANASEMAJE?
Kama ilivyo ada ili kupata uzani wa habari, tulimtafuta Dida, alipopatikana, alifunguka:
“Mimi na mume wangu huwa hatuna mipaka katika simu zetu, kila mtu yuko huru kuchezea simu ya mwenziye. Siku ya tukio jamaa (Ezden) kabla hajaenda kuoga alitengeneza namba za siri (pasword) sasa nilivyotaka kucheza gemu nikamfuata bafuni na kumuuliza mbona simu imefungwa, nikamuomba anifungulie, huwezi amini akaanza kunitukana, nikajiuliza ni simu tu au kuna mengine!”
Khadija Shaibu ‘Dida’.
KIPIGO KINAENDELEA
Akiendelea kusimulia, Dida alisema ghafla, Ezden alichukua mkanda na kuanza kumpiga.
“Nilishangaa sana, nikajiuliza kosa langu ni nini? Alinipiga hadi akanipasua sehemu ya kichwa, sikuamini kama Ezden anaweza kunifanya vile au kama alinichoka angeniambia wakati yeye ndiye mkosaji,” alisema Dida.
EZDEN ATIMKA
Chanzo kilidai kuwa, baada ya Ezden kuona amemuumiza mkewe, alikusanya nguo zake na kukimbia kwa usafiri wa Bajaj kwani Dida alificha funguo zote za magari yake.
“Alijua Dida atakwenda polisi hivyo akaona bora atimke zake,”  kilisema chanzo.
Khadija Shaibu ‘Dida’ na mume wake, Ezden Jumanne.
DIDA ATAKA TALAKA
Katika kuonyesha kuwa amechukizwa na tukio hilo la kupigwa ambalo amedai limekuwa likitokea mara kwa mara pamoja na kukosa imani naye katika masuala ya kuchepuka, Dida amesema kwa kuwa alishindwa kumuomba msamaha siku ileile ya tukio, anachotaka kutoka kwake ni talaka tu.
TUJIKUMBUSHE
Tukio la kuvunjika kwa ndoa hiyo iliyofungwa mwaka jana (siku tano kabla ya Mwezi wa Ramadhani kuanza) likikamilika kwa talaka, Dida atakuwa ametimiza idadi ya ndoa tatu kuvunjika.
Awali aliolewa na Mohamed Mchopanga ‘Mchops’ kisha Gervas Mbwiga ‘G’ na wote walimmwaga kwa talaka.

UNJAMJUNGU KWA AUNT, WEMA NA KAJALA LIVE,WALA SAHANI MOJA WAKATA MAUNO YA KUFA MTU



Manguli wawili wa Bongo Movies waliokuwa mahasimu wakubwa Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ na Kajala Masanja ‘K’ wakikata mauno.

Hatimaye! Manguli wawili wa Bongo Movies waliokuwa mahasimu wakubwa na kusababisha tafrani kubwa, Wema Isaac Sepetu ‘Beautful Onyinye’ na Kajala Masanja ‘K’ hatimaye wamekutana uso kwa uso (live) na kumaliza bifu lao saa chache kabla ya kuanza kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani,

NI KWENYE VUNJA JUNGU

Tukio hilo la heshima lilijiri wikiendi iliyopita nyumbani kwa staa mwenzao wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson, Mwananyamala jijini Dar ambapo baadhi ya mastaa walikuwa wakivunja jungu katika sherehe ya kumpongeza rafiki yao almaarufu kwa jina la Wise Ime aliyejifungua mtoto wa kike hivi karibuni.
...Wema na Kajala katika pozi.
KWA MARA YA KWANZA TANGU WAGOMBANE
Katika tukio hilo, mastaa wenzao walipigwa na butwaa kuwaona wawili hao wakiwa pamoja kwa mara ya kwanza tangu wagombane. miezi kadhaa iliyopita.
WALA UJANA KAMA ZAMANI
Mastaa hao walinaswa pamoja wakiwa kama kumbikumbi wakila ujana kama zamani, kitendo kilichowafurahisha marafiki zao wengine waliofika nyumbani hapo wakimpongeza Aunt kwa kuwaweka pamoja kwani tangu wapatanishwe hawakuwahi kukaa pamoja wala kula sahani moja kama walivyofanya siku hiyo.
“Ukweli sisi tumefurahishwa na ukaribu wa hawa mashosti tuliwamisi sana kuwaona hasa kwenye shughuli kama hizi za kibao kata, leo wameshirikiana kama zamani, wamezungumza, wamecheka na kukata mauno pamoja,” alisikika mmoja wa mastaa aliyehudhuria katika shughuli hiyo.
MAUNO MWANZO-MWISHO
Kwenye shughuli hiyo kulipambwa na mauno mwanzo-mwisho yaliyoongozwa na wapiga ngoma ya Kibao Kata ambapo kila mmoja aliinuka na kuonesha ustadi wake wa kukata mauno.
Aunt Ezekiel na Vanita wakikata nyonga.
HADI MAJOGOO
Shughuli hiyo iliendelea hadi majogoo kwani baada ya Kibao Kata, mastaa hao walifunguliwa disko lililokuwa likiongozwa na madj maalum wa Pro24djs huku MC akiwa ni Maimartha  Jesse.
WEMA, KAJALA, AUNT WAPAGAWISHA
Katika shughuli hiyo, Wema, Kajala na Aunt walipagawishwa na wimbo wa mpya wa mpenzi wa Wema, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ wa Mdogomdogo ambapo waliingia kati na kuachia mauno hadharani.
...Aunt Ezekiel na mashosti zake wakizidi kuonyesha machejo.
Kuna wakati Kajala na Wema waliachiwa nafasi ambapo walitoana jasho kwa kukata mauno huku wakifuatisha vizuri wimbo huo utadhani walikuwa wamefanya ‘riheso’.
ASANTE DJ
Baada ya kuserebuka kwa muda mrefu hadi wakatoka jasho, wawili hao walisikika wakisema kuwa Dj alikuwa amewakuna mno kwani kila muziki aliokuwa akiwawekea alikuwa akiwalenga na kuwafanya wachangamke zaidi hadi shughuli ilipokwisha kila mtu akarudi kwake.
NENO LA WEMA
“Sasa hivi tupo vizuri sana. Yes tupo bega kwa bega ukizingatia ndiyo tunaingia kwenye mwezi mtukufu. Nimefurahi sana kushea naiti na Kajala,” alisema Wema.
NAYE KAJALA
“Kwani kuna tatizo? Hakuna tatizo. Sisi tupo vizuri kama alivyosema Wema tumeinjoi sana,” alifunguka Kajala.
Mahasimu hao wawili wakiwa kwenye picha ya pamoja na mashosti wenzao.
TUMEFIKAJE HAPA
Miezi kadhaa Wema na Kajala waliingia kwenye gogoro kubwa na kusababisha kuibuka kwa pande mbili za Team Wema na Team Kajala zilizokuwa zinachochea ugomvi huku Kajala akitakiwa kurejesha zile Sh. Milioni 13 alizolipiwa na Wema asiende jela miaka 7.

BABY MADAHA: SIOLEWI KWA KUFUATA MKUMBO



‘Baby Madaha’ akiwa kwenye pozi.

STAA wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’ amesema anaishi katika staili ya kivyake hivyo kamwe hawezi kuolewa kwa kufuata mkumbo kama ilivyo kwa wasanii wengine.

Staa wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’
Akipiga stori na paparazi, Baby Madaha alikiri kuwa ana mchumba ambaye ni Joh Kairuki, anampenda sana ila katika suala la kufunga ndoa bado yupoyupo sana kwa sababu haolewi kwa kufuata mkumbo kwani amejifunza kupitia kwa walioolewa na kuachika.
“Nitaolewa nitakapokuwa tayari siyo kwa kufuata mkumbo vinginevyo bora nibakie hivihivi kwa sababu pesa kwangu ndiyo kila kitu, mambo mengine yanafuata,” alisema.

RED CARPET YA TUZO ZA BET 2014




Diamond Platnumz akihojiwa na Karrueche Tran ambaye ni mpenzi wa Chris Brown kwenye Red Carpet.
Amber Rose.
T.I.
Gabrielle Union.
Ne-Yo akipozi kwenye Red Carpet.
Ashanti.
Nelly.
Claudia Jordan.
John Legend.
Eva Marcille.
Lionel Richie.
Jennifer Freeman.

LIST YOTE YA WASHINDI YA TUZO ZA BET 2014 HII HAPA, BEYONCE AKOMBA 3, PHARRELL, AUGUST, LUPITA WAPATA 2 KILA MMOJA,DOVIDO ANYAKUA YAKE, DIAMOND AANGUKIA PUA


Pharrell Williams na Missy Elliot wakifungua shoo ya utoaji tuzo za BET usiku wa kuamkia leo jijini Los Angeles.


Chris Brown akifanya makamuzi wakati wa utoaji tuzo za BET.

WASHINDI WA TUZO HIZO NI KAMA IFUATAVYO:
Best Female R&B/Pop Artist
Beyoncé (WINNER)
Janelle Monáe
Jhené Aiko
K. Michelle
Rihanna
Tamar Braxton

Best Male R&B/Pop Artist
Pharrell Williams (WINNER)
August Alsina
Chris Brown
John Legend
Justin Timberlake

Best Collaboration
Beyoncé f/ JAY Z – "Drunk In Love" (WINNER)
August Alsina f/ Trinidad Jame$ – "I Luv This"
Drake f/ Majid Jordan – "Hold On (We're Going Home)"
JAY Z f/ Justin Timberlake – "Holy Grail"
Robin Thicke f/ T.I. & Pharrell Williams – "Blurred Lines"
YG f/ Jeezy & Rich Homie Quan – "My Hitta"

Best Movie
12 Years a Slave (WINNER)
The Best Man Holiday
Fruitvale Station
Kevin Hart: Let Me Explain
Lee Daniels' The Butler

Best Actress
Lupita Nyong’o (WINNER)
Angela Bassett
Gabrielle Union
Kerry Washington
Oprah Winfrey

Best Actor
Chiwetel Ejiofor (WINNER)
Forest Whitaker
Idris Elba
Kevin Hart
Michael B. Jordan

Video of the Year
Pharrell Williams – "Happy" (WINNER)
Beyoncé – "Partition"
Beyoncé f/ JAY Z – "Drunk In Love"
Chris Brown – "Fine China"
Drake – "Worst Behavior"

Best Male Hip Hop Artist
Drake (WINNER)
Future
J. Cole
JAY Z
Kendrick Lamar

Best Female Hip Hop Artist
Nicki Minaj (WINNER)
Angel Haze
Charli Baltimore
Eve
Iggy Azalea

Best Group
Young Money (WINNER)
A$AP Mob
Daft Punk
Macklemore & Ryan Lewis
TGT

Subway Sportsman of the Year
Kevin Durant (WINNER)
Floyd Mayweather Jr.
Carmelo Anthony
Blake Griffin
LeBron James

Subway Sportswoman of the Year
Serena Williams (WINNER)
Brittney Griner
Lolo Jones
Skylar Diggins
Venus Williams

Best Gospel Artist
Tamela Mann (WINNER)
Donnie McClurkin
Erica Campbell
Hezekiah Walker
Tye Tribbett

Best New Artist
August Alsina (WINNER)
Ariana Grande
Mack Wilds
Rich Homie Quan
ScHoolboy Q    

YoungStars Award
KeKe Palmer (WINNER)
Gabrielle Douglas
Jacob Latimore
Jaden Smith
Zendaya

Centric Award
Jhené Aiko – "The Worst" (WINNER)
Aloe Blacc – "The Man"
Jennifer Hudson f/ T.I. – "I Can't Describe (The Way I Feel)"
LiV Warfield – "Why Do You Lie?"
Wale f/ Sam Dew – "LoveHate Thing"

Best International Act: UK
Krept & Konan (WINNER)
Dizzee Rascal
Ghetts
Laura Mvula
Rita Ora
Tinie Tempah

Video Director of the Year
Hype Williams (WINNER)
Benny Boom
Chris Brown
Colin Tilley
Director X

Best International Act: Africa
Davido (Nigeria) (WINNER)
Diamond Platnumz (Tanzania)
Mafikizolo (South Africa)
Sarkodie (Ghana)
Tiwa Savage (Nigeria)
Toofan (Togo)


PHARRELL, AUGUST, LUPITA WAPATA 2 KILA MMOJA

TIMBWILI LA KUSHIKANA UCHAWI LATIKISA



Mzee Kikongwe aliyefahamika kwa jina moja la Siberi anayetuhumiwa kwa ulozi.


Katika hali ya kushangaza, mama aliyetajwa kwa jina la Khadija Omari amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kushikana uchawi na kikongwe anayefahamika kwa jina moja la Siberi akiwa na mganga wake, Rashid na kuibua timbwili lililotikisa, akimtuhumu kikongwe huyo kumchukua mwanaye kimazingara ‘msukule’.
Tukio hilo lilitokea wikiendi iliyopita maeneo ya Mgeni-Nani, Mbagala jijini Dar na kusababisha sekeseke kubwa lililofunga mtaa kufuatia mvutano ulioibuka baina ya wakazi wa mtaa huo huku baadhi wakiamini ushirikina wakimhusisha kikongwe huyo.
Mama aliyetajwa kwa jina la Khadija Omari anayemtuhumu mzee huyo.
Kwa mujibu wa Khadija ambaye ni mama mzazi wa mtoto anayedaiwa kuchukuliwa msukule aitwaye Tausi, mwanaye huyo alifariki dunia Agosti, mwaka jana katika mazingira ya kutatanisha.
Alisema kifo cha mwanaye kilimtatiza hivyo alikwenda kwa waganga wa jadi ‘kuchungulia’ kama alifariki dunia kweli au ni mauzauza ndipo akabaini kuwa kikongwe huyo ambaye alikuwa mwenye nyumba wake anahusika.
Mganga akijaribu kutoa dawa ya kurejesha mtoto.
Kufuatia hali hiyo, Khadija aliamua kuondoka kwenye nyumba ya kikongwe huyo kwani alikuwa akikutana na mauzauza kila kukicha na kutimkia mkoani Mwanza huku akijipanga kutafuta mtaalam wa kumtoa mwanaye alipowekwa msukule.
Alisema hivi karibuni alirejea Dar na kutinga kwa kikongwe huyo akiwa na waganga wa jadi ili kumpata mwanaye.
Baadhi ya mashuhuda waliofika kushuhudia sekeseke hilo.
Hata hivyo, zoezi hilo halikufanikiwa baada ya ndugu wa kikongwe huyo kuingilia kati na kuanzisha timbwili la aina yake wakimtetea kwa madai hawana imani kama anajihusisha na vitendo vya aina hiyo.

Diamond Platnumz AANGUKIA PUA TENA,Davido ACHUKUA TUZO, Baada Ya Kutofanikiwa Kupata Tuzo Ya BET Diamond Asema Haya!!!


Imani yangu ni kwamba umekuwa mfuatiliaji mzuri wa habari tofauti kuhusu muziki wa Tanzania  na unafahamu kuhusu tuzo kubwa aliyokuwa akiwania msanii Diamond katika tuzo za Bet Nchini Marekani.


 Taarifa mpya ni kuwa Tuzo zimefanyika na Tuzo aliyowania Diamond ya Best Africa Act imekwenda kwa msanii mwenzake Davido kutoka Nigeria.

Kwenye instagram Ya Diamond Kuna Huu Ujumbe kuhusu Matokeo Hayo.

” Tusipopenda kukubali Matokeo na Ushindi wa Wenzetu basi Daima Hatutaweza kuwa Washindani….Muhimu ni kujua wapi tulipotoka na Wapi tulipo Leo… 

Katika Nchi zaidi ya 20 zenye wasanii zaidi ya Million 40, kuchaguliwa Tanzania ni fursa, Heshima na Hatua kubwa… Cha Muhimu ni kuitumia vyema Fursa Hii na Kuhakikisha Mwakani tunapiga Hatua Zaidi!….

 Asante sana kwa wote wanaozidi kuni support kwa hali na Mali, Mapambano ndio kwaaaanza yanaanza sasa…..!!!!!! @wcb_wasafi For Life Baby
d

dd 7


Msanii wa Nigeria, Davido ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya Best African Act, katika BET Awards 2014 zinazofanyika usiku huu Los Angeles, Marekani.

DAVIDO ASHINDA TUZO
Davido alikuwa anawania kipengele hicho na wakali wengine kutoka Afrika akiwemo Diamond Platinumz, Mafikizolo, Toofan, Sarkodie na Tiwa Savage.
Na Davido ameandika Hivi Twitter Instagram

dd 4

Show kamili ya tuzo hizo imeanza muda mfupi baada ya kutoa tuzo hiyo kwa msanii wa Afrika.
Ingawa Diamond Platinumz hakubahatika kuichukua tuzo hii, lakini hatua aliyopiga ni kubwa sana inayoweka Tanzania kwenye historia ya tuzo hizo kubwa za muziki duniani.

Kabla ya tuzo hizo, Diamond alipata nafasi ya kufanya mahojiano na vituo vikubwa na kuhudhuria mkutano maalumu wa wanamuziki wa kimataifa, na jana usiku aliungana na wanamuziki wenzake wa kimataifa katika BET Pre Awards Party.