Jamaa aliyetajwa kwa jina moja la Lugali akihusishwa kuchepuka na mke wa mpangaji wake, akiwa amenaswa kwenye gesti moja maeneo ya Buguruni, Dar.
Vunja jungu! Saa kadhaa kabla ya kuanza kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, jamaa aliyetajwa kwa jina moja la Lugali ameibua sekeseke kwenye nyumba ya kulala wageni (gesti), kisa kikidaiwa ni mchepuko akihusishwa na mke wa mpangaji wake,
mzee
huyo alichomolewa kutoka chumbani huku damu zikimvuja baada ya kula
kichapo kutoka kwa jamaa na ndugu wa mwanaume aliyedai kuwa jamaa huyo
alikuwa anamsumbua mkewe.
Kwa
mujibu wa mashuhuda, kabla ya jamaa hao kuingia chumbani humo kwanza
walivunja mlango wa chumba hicho baada ya kupata idhini kutoka kwa
msimamizi wa gesti hiyo kufuatia baba mwenye nyumba huyo kukahidi
kuwafungulia mlango ili wamchukue mke wa ndugu yao aliyedaiwa kuwa ndani
na mzee huyo.
Walidai
kwamba mzee huyo ambaye ni baba mwenye nyumba, alikuwa akimtolea udenda
mke huyo wa mpagaji wake ambaye ni jirani yake huku akimsumbua mara kwa
mara kwa simu na ujumbe mfupi wa SMS.
Ilisemekana kuwa mume huyo alimweleza mkewe ili aamini kweli baba mwenye nyumba alipania kumtaka basi amkubali ili amkute naye gesti amkomeshe kwa tabia hiyo ya baadhi ya wenye nyumba ambao huwataka wake wa wapangaji wake.
“Nilimwambia
mke wangu amkubali kwa sababu nilikuwa na nia ya kukomesha tabia yake
ya kutongoza wake wa wapangaji wake, akamwita Buguruni ndipo nikawapigia
ninyi waandishi wa habari ili mje mchukue ushahidi,” alisema mume huyo.
Baada
ya kukutwa gesti humo, mzee huyo aliomba msamaha kwa mpangaji wake huyo
na kuahidi kulipa fidia ambapo aliwaandikia cheki feki kisha akakimbilia
Kituo cha Polisi cha Buguruni na kufungua shauri kuwa alitekwa,
akapigwa kisha akapelekwa gesti.
Shauri
hilo ambalo liliandikishwa kwa jalada namba BUG/RB 6182/2014- utekaji.
Mzee huyo alidai kutekwa na mpangaji wake huyo na kumpeleka nje ya mji
kisha kumpiga ili kuua soo.
Hadi paparazi tunaanua jamvi kituoni hapo, polisi walikuwa wakichunguza ili ukweli ujulikane.
Hadi paparazi tunaanua jamvi kituoni hapo, polisi walikuwa wakichunguza ili ukweli ujulikane.
No comments:
Post a Comment