‘Baby Madaha’ akiwa kwenye pozi.
STAA wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’ amesema anaishi katika staili ya kivyake hivyo kamwe hawezi kuolewa kwa kufuata mkumbo kama ilivyo kwa wasanii wengine.
Akipiga stori na paparazi, Baby
Madaha alikiri kuwa ana mchumba ambaye ni Joh Kairuki, anampenda sana
ila katika suala la kufunga ndoa bado yupoyupo sana kwa sababu haolewi
kwa kufuata mkumbo kwani amejifunza kupitia kwa walioolewa na kuachika.
“Nitaolewa nitakapokuwa tayari siyo
kwa kufuata mkumbo vinginevyo bora nibakie hivihivi kwa sababu pesa
kwangu ndiyo kila kitu, mambo mengine yanafuata,” alisema.
No comments:
Post a Comment