Tukio hilo lilitokea wikiendi
iliyopita maeneo ya Mgeni-Nani, Mbagala jijini Dar na kusababisha
sekeseke kubwa lililofunga mtaa kufuatia mvutano ulioibuka baina ya
wakazi wa mtaa huo huku baadhi wakiamini ushirikina wakimhusisha
kikongwe huyo.
Mama aliyetajwa kwa jina la Khadija Omari anayemtuhumu mzee huyo.
Kwa mujibu wa Khadija ambaye ni mama
mzazi wa mtoto anayedaiwa kuchukuliwa msukule aitwaye Tausi, mwanaye
huyo alifariki dunia Agosti, mwaka jana katika mazingira ya kutatanisha.
Alisema kifo cha mwanaye kilimtatiza
hivyo alikwenda kwa waganga wa jadi ‘kuchungulia’ kama alifariki dunia
kweli au ni mauzauza ndipo akabaini kuwa kikongwe huyo ambaye alikuwa
mwenye nyumba wake anahusika.
Mganga akijaribu kutoa dawa ya kurejesha mtoto.
Kufuatia hali hiyo, Khadija aliamua
kuondoka kwenye nyumba ya kikongwe huyo kwani alikuwa akikutana na
mauzauza kila kukicha na kutimkia mkoani Mwanza huku akijipanga kutafuta
mtaalam wa kumtoa mwanaye alipowekwa msukule.
Alisema hivi karibuni alirejea Dar na kutinga kwa kikongwe huyo akiwa na waganga wa jadi ili kumpata mwanaye.
Baadhi ya mashuhuda waliofika kushuhudia sekeseke hilo.
Hata hivyo, zoezi hilo halikufanikiwa
baada ya ndugu wa kikongwe huyo kuingilia kati na kuanzisha timbwili la
aina yake wakimtetea kwa madai hawana imani kama anajihusisha na
vitendo vya aina hiyo.
No comments:
Post a Comment