Baadhi ya ndugu katika kikao hicho
Sakata
la mke kuishi na wanaume wawili lachukua sura mpya baada ya kikao cha
ndugu wa mume halali Rogers Halinga kuketi kikao Kijiji cha Ishungu Kata
ya Ruiwa Mbarali Mkoani Mbeya na kumtaka Biton Mwashilindi kufanya
mazungumzo nao kabla hawajafungua madai ya ugoni Mahakani na kudai
fidia.
Kikao
hicho kizito kilichofanyika nyumbani kwa Baba mzazi wa Rogers Halinga
mzee Jason Halinga(95) Novemba mosi mwaka huu na kuhudhuriwa na ndugu
lukuki na kumsikiza mke wa Rogers ili abaini ukweli juu ya mtoto
aliyezua utata kuwa ni wa nani baina ya Rogers au Biton Mwashilindi.
Mwanamke
huyo a(22) akijikanganya mara kadhaa katika kikao hicho akidai kuwa
mtoto huyo ni wa Rogers kwa kuwa aliondoka baada ya kutokea mapishano na
mumewe akiwa na ujauzito wa miezi minne ndipo alipoanza mahusiano ya
kimapenzi na Biton hadi siku anajifungua mwaka 2012 akiwa mikononi mwa
Biton ndipo alipoamua kumwandikisha mtoto katika kadi ya kliniki na
cheti cha kuzaliwa jina la Biton.
Huku
ndugu wakihamaki kutokana na kauli hiyo na kwamba yeye atamke wazi
mtoto ni wa nani ndipo Juliana bila aibu kwa Baba Mkwe Mzee Jason
Halinga alijibu kuwa mtoto ni wa Biton Mwashilindi,ambapo alimkabidhi
mtoto huyo mwishoni mwa mwezi Octoba kwa hiari na wala hakuporwa kama
alivyotoa taarifa Polisi.
Kauli
hiyo ya Juliana ililazimu kikao kupiga simu kwa mzazi wa Juliana
anayeishi Lwanjilo wilayani Chunya kujua mustakabali wa kauli ya mtoto
wao kwani ilidaiwa kuwa Biton aliwahi kwenda huko kujitambulisha kuwa
yeye anaishi na mtoto wao na kwamba Biton hakujua kuwa Juliana aliwahi
kuolewa kwani alidai kuwa yeye ni mwanafunzi wa VETA Mbeya na asimwambie
kuwa yeye ni mwanandoa.
Baba
mzazi wa Juliana Hosea Mwalukasa alidai kuwa ni kweli Biton alifika
kwake lakini hakumpokea kwa kuwa alidai kuwa Juliana ni mke halali wa
Rogers Halinga hivyo kama amezaa na Juliana amefanya kosa na kwamba
atatozwa ugoni kwani Juliana hakuwahi kupewa talaka na Halinga.
Kikao
hicho baada ya mvutano wa muda mrefu kiliamua kuwa endapo Biton anadai
kuwa mtoto aliyezaliwa na Juliana aliyefahamika kwa jina la Zalida
Biton(2) ni mtoto wake basi alipe fidia ya kuzaa na mke wa mtu kiasi cha
shilingi milioni kumi au alipe n'gombe saba ili aweze kumkomboa mtoto
wake na kwamba Juliana bado ni mke halali wa Rogers.
Kwa
upande wake Biton Mwashilindi alidai kuwa hayuko tayari kulipa pesa
hizo na kwamba yeye alikabidhiwa mtoto kihalali na Jeshi la Polisi
Ocktoba 31 mwaka huu kituo kikuu cha kat mbele ya maafisa wa Jeshi la
Polisi na kwamba hana kesi ya kujibu na kwamba anasubiri tu mtoto
afikishe umri wa miaka saba ndipo amchuke.
Katika
suala hili baadhi ya wadau wamelalamikia Jeshi la Polisi kwa kuamua
masuala ya kisheria katika vituo vya Polisi badala ya mamlaka za
kisheria zipo kama mahakama kuliko uamuzi uliotolewa na hali hii
husababisha baadhi ya wananchi kujichukulia sheria mkononi.
Wamedai
kitendo cha kukabidhiwa mtoto Biton bila kuchukuliwa vipimo vya DNA
bado hakujatutua mgogoro huu na kwamba bado suluhu katika ndoa hiyo hiyo
itakuwa ni kitendawiri kisicho na majibu.
|
No comments:
Post a Comment