
Wakala wa
Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), bila shaka mko vizuri mnaendelea
kusimamia jukumu zito katika taifa letu.Usajili, Ufilisi na Udhamini
siyo kazi ndogo. Ni kazi inayohitaji umakini wa hali ya juu maana
matokeo ya ufanisi wenu ndiyo majibu ya shughuli nyingi katika nchi.
Watu wakitaka kusafiri, kutambulika katika maeneo mbalimbali nyinyi lazima mhusike kutatua.
Mkitaka
kujua afya yangu, mimi ni mzima. Namshukuru Mungu naendelea na majukumu
yangu kama kawaida. Nimewakumbuka leo kupitia barua hii ili niweze
kuwafikishia yaliyoko katika akili yangu ndogo.
No comments:
Post a Comment