Stori: Gabriel Ng’osha
Kijana Mohamed Said almaarufu Ngwea feki, anayefananishwa na aliyekuwa staa wa Bongo Fleva, marehemu Alberth Mangweha ‘Ngwea’, ameingia katika mzozo mkali na ndugu zake akidaiwa kugombea maiti ya mama yake mzazi, Mariamu Enock (54).
Kijana Mohamed Said almaarufu Ngwea feki, anayefananishwa na aliyekuwa staa wa Bongo Fleva, marehemu Alberth Mangweha ‘Ngwea’, ameingia katika mzozo mkali na ndugu zake akidaiwa kugombea maiti ya mama yake mzazi, Mariamu Enock (54).
Kwa mujibu wa chanzo chetu, tukio hilo lilijiri kwenye makazi ya familia
hiyo, Tandale, Dar hivi karibuni ambapo mama huyo alifariki dunia kwa
kuugua kwa muda mrefu.
Ilidaiwa kwamba, baada ya kifo hicho, uliibuka mzozo ambapo ndugu wa
upande wa mama yake walitaka mwili wakaupumzishe mkoani Iringa huku
Ngwea feki akitaka uzikwe Dar. Ilisemekana kwamba jamaa huyo alitaka iwe
hivyo kwa sababu alikuwa na mama yake muda wote na alitumia gharama
kubwa kumtibu.
Akizungumza na mwanahabari wetu kuhusiana na sakata hilo, msemaji wa
familia hiyo, Laurence Enock ambaye ni kaka wa marehemu (yaani mjomba wa
Ngwea feki), alisema: “Sisi kama familia tumeamua kumsafirisha ndugu
yetu kwenda kumzika Iringa, ndiko kuna mashamba ya familia yetu lakini
Mohamed (Ngwea feki) amekataa.”
Alisema kwamba, baada ya vuta nikuvute ndipo Ngwea feki akadai alipwe
shilingi laki tatu (300,000/=) alizotumia kumtibu mama yake wakati
anaumwa.Kwa upande wake, ndugu wa Ngwea feki aliyefahamika kwa jina la
Hassan Said alionekana kutomuunga mkono ndugu yake.
Hassan alisema: “Mimi siko tayari kugawana vitu vya mama yangu kwa kuwa
ndugu yangu amekataa mwili wa mama usisafirishwe hadi alipwe fidia yake
hivyo imebidi tuuze vitu vya mama ili alipwe hiyo laki tatu.
Alipofuatwa Ngwea feki ili kusikia upande wake aligoma kutoa ushirikiano: “Siko vizuri kwa sasa nicheki baadaye.”
Kwa mujibu wa baba wa marehemu, Enock Mayenje, mjukuu wake huyo amekuwa
akijitenga na familia hivyo hawezi kumlazimisha ila amesikitika kwa
kitendo chake cha ‘kuwauzia’ maiti ya mama yake mzazi.
Kamanda wa Ulinzi Mtaa wa Mkunduge, Tandale jijini Dar, Yusuph Banda,
amekiri kutokea kwa tukio hilo na wamekubaliana kuuzwa kwa vitu vya
marehemu ili gharama hizo zilipwe kwa Ngwea feki ili mwili huo
usafirishwe kwenda Iringa kwa mazishi.
No comments:
Post a Comment