Pamoja na kauli ya Rais Kikwete aliyoitoa jana wakati akilihutubia Taifa
kupitia wazee wa Dodoma, Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein jana
hiyohiyo, aliwataka Wazanzibari kuipitisha Katiba Inayopendekezwa bila
kufanya makosa.
Nyuma ya kauli hizo za marais, Ukawa umesema umeandaliwa mkakati kabambe
wa kuvitumia vyombo vya habari kwa fedha za umma kutoka Ikulu
kuwashawishi wananchi kupigia kura ya ‘ndiyo’ katiba hiyo.
Kauli ya Rais Kikwete
“Kwa sababu hiyo naomba Watanzania wenzangu tuzingatie mamlaka ya Sheria
ya Kura ya Maoni ambayo imeelekeza vizuri lini kura ya maoni itafanyika
na lini kampeni zitafanyika, lini wadau watatoa elimu naomba tuwe na
subira. Tukizingatia sheria hii hakuna ugomvi.”
Aliongeza hadi Tume itakapotoa maelekezo ya utekelezaji, wakati wa
kampeni na kutoa elimu kwa umma bado na kwamba sheria ipo na imezipanga
siku maalumu za kufanya hivyo.
Alisema licha ya sheria kuruhusu kampeni kufanyika ndani ya siku 60
kabla ya kura za maoni kupigwa, kwa mamlaka yake akiwa kiongozi wa nchi,
kura na kampeni vitafanyika ndani ya siku 30 tu.
“Kampeni zitaanza tarehe 30 Machi na kumalizika tarehe 29 Aprili ikiwa
ni siku moja kabla ya kupiga kura ya maoni. Muda huo ndiyo utakuwa wa
kufanya hivyo,” alisema Kikwete.
Dk Shein aipigia debe
Wakati Kikwete akisema hayo, Dk Shein amesema Katiba Inayopendekezwa ni
mwarobaini wa kero nyingi za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na
Wazanzibari wasifanye makosa kuikataa wakati wa kura ya maoni mwakani.
Akizungumza katika kongamano la kuadhimisha miaka minne ya Serikali ya
Umoja wa Kitaifa Zanzibar, Dk Shein alisema iwapo Katiba hiyo
itapitishwa, itasaidia kuimarisha Muungano kwa kuwa imezingatia
makubaliano ya Muungano ya kuwa na Serikali mbili.
No comments:
Post a Comment