JESHI la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, linamshikilia
Philemon Ng’ambi, mkazi wa Madale Kata ya Wazo, jijini
Dar es Salaam kwa tuhuma za kumuua mkewe, Enea
Kagine kwa kumshambulia kwa mawe na matofali hadi
kumuua.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Enea Kagine likibebwa na
waombolezaji.
Philemon anadaiwa kufanya unyama huo kwa marehemu
mkewe aliyekuwa amebakiza siku mbili kabla ya
kujivungua usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita
nyumbani kwake Wazo-Hill.
Akisimulia mkasa huo kwa mapaparazi wetu, jirani wa
wanandoa hao aliyejitambulisha kwa jina la Fikiri Rashid
alisema:
“Mimi nyumba yangu na yao zinatazamana hivyo siku ya
tukio majira ya saa tisa usiku, nilianza kumsikia marehemu
akipiga mayowe ya kuomba msaada akisema mumewe
anamuua.
Marehemu Enea Kagine enzi za uhai wake.
“Nilitoka nje kwa lengo la kutaka kutoa msaada lakini
nilihofia maisha yangu hivyo ilinibidi niwaite vijana wa
ulinzi shirikishi ambao baada ya muda walifika eneo la
tukio na kumkuta mtuhumiwa akivunja vyombo vya ndani
kama mtu aliyechanganyikiwa, wakati huo tayari alikuwa
ameshamuua mkewe.
“Baada ya kuwaona ulinzi shirikishi, alikimbilia chumbani
na kwenda kujificha uvunguni kwenye kitanda huku watoto
wao watatu wakiwa wamelala.
Mtuhumiwa wa mauaji hayo, Philemon Ng’ambi.
“Bila kuchelewa, askari wa ulinzi shirikishi walimkamata
na kuwasiliana na Askari wa Kituo cha Polisi cha Wazo
ambao walifika eneo la tukio na kumtia mbaroni
mtuhumiwa pamoja na kuuchukua mwili wa marehemu kwa
ajili ya taratibu za kipolisi,” alisema Fikiri.
Mama mzazi wa marehemu Enea akiwa na simanzi nzito.
Kufuatia tukio hilo la kusikitisha wanahabari wetu walifika
katika Hospitali ya Mwananyamala ulipohifadhiwa mwili
wa mwanamke huyo na mtoto wake waliyemtoa akiwa
amefia tumboni.
Miili hiyo ilizikwa Jumatatu iliyopita (Novemba 25) mwaka
huu katika kaburi moja kwenye Makaburi ya Madale, Dar es
Salaam.
Thursday, 28 November 2013
MUME AMUUA MKEWE MWENYE MIMBA YA SIKU 2 AJIFUNGUE KWA KUMPIGA NA MAWE NA MATOFALiI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment