Taasisi isiyo ya kiserikali inayoshughulikia mambo
ya utawala bora na maendeleo nchini (The Center
for Good Governance and Development in Tanzania
-CEGODETA), imeitaka Serikali ya Tanzania
kumshtaki Rais wa Malawi, Joyce Banda Umoja
wa Nchi za Afrika (AU).
Taarifa ya taasisi hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi
Mtendaji wa taasisi hiyo, Thomas Ngawaiya
ilisema uamuzi huo ni kutokana na kauli za dharau
za Banda dhidi ya viongozi wanaoshughulikia
mgogoro wa Ziwa Nyasa.
“Serikali imshtaki kiongozi huyo wa Malawi AU ili
aulizwe ana dhamira gani kwa Tanzania na Afrika
kabla hajaleta madhara makubwa kwa nchi yetu na
Bara zima la Afrika.
Waswahili husema ‘Mchelea mwana kulia hulia
yeye’ na ‘Mdharau mwiba mguu huota tende’,
maana yake ni kuwa inawezekana huyu mtu ana
mtandao mbaya sana tusioujua, tufanye uchunguzi
kuubaini,” inasema taarifa hiyo.
Inasema kuwa, mara tu baada ya kuingia
madarakani Rais Banda alidai kuwa Ziwa Nyasa ni
mali ya Malawi kwa asilimia 100 na Tanzania
haina haki ya kulitumia ziwa hilo kwa njia yoyote
ile.
Taarifa hiyo inasema kuwa, mgogoro huo kwa sasa
uko kwenye jopo la usuluhishi la marais wastaafu
wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa
Afrika (SADC) chini ya Rais Mstaafu, Joachim
Chissano wa Msumbiji.
Thursday, 28 November 2013
RAIS WA MALAWI JOYCE BANDA ASHITAKIWE UMOJA WA NCHI ZA AFRICA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment