MOYO;
huhifadhi mengi mazito hasa ya kuumiza! Staa mkubwa wa
sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe amejikuta
akimwaga machozi wakati akianika siri tano nzito kuhusu
mapenzi katika mahojiano (exclusive interview)
Katika ‘intavyu’ hiyo iliyofanyika Jumatatu iliyopita kwenye
Ofisi za Global Publishers, Bamaga-Mwenge jijini Dar
kuanzia saa 8:44 alasiri hadi saa 10:44 jioni, Wolper
alifunguka vitu vingi.
KISA/MKASA
Akizungumza kwa masikitiko, uchungu na majuto, Wolper
alisema hawezi kumsahau mwanaume huyo ambaye ni
Abdallah Mtoro ‘Dallas’ kwa namna alivyomwingia kijanja
na kutaka kumvunjia heshima aliyoijenga karibia miaka
kumi nyuma.
ALIANZIA WAPI NA DALLAS?
“Siku ya kwanza Dallas alinipigia simu na kuniambia
aliniona Magomeni (Dar). Naikumbuka sana siku hiyo,
ilikuwa baada ya mizunguko yangu, mwanzoni sikupokea
simu yake kwa sababu ilikuwa namba ngeni kwangu.
“Nilimsikiliza sana. Jamani yule mwanaume anaongea kwa
ushawishi wa hali ya juu mno. Nilishangaa aliponieleza
kila kitu kuhusu familia yangu na nyumbani kwetu. Kumbe
tayari alishaunda urafiki na baba yangu (mzee Massawe).
“Mwanzoni nilidhani ni tapeli. Nikamkatia simu.
Akaendelea kunipigia na nilipoona imekuwa kero kubwa
nilipokea. Ili kuthibitisha anawajua wazazi wangu,
alinitajia namba zao za simu ambazo ni za kweli.
“Pamoja na hilo nilimfanyia nyodo, si unajua mtoto wa
kike? Lakini aliniongelesha kwa upole hadi nikapunguza
nyodo zangu.
“Aliniuliza nataka anifungulie biashara gani. Nikamwambia
biashara ya nguo. Akaniuliza nataka mtaji kiasi gani.
nikamwambia dola laki moja kwa sababu nilikuwa sitaki
fremu moja, nilitaka nyumba nzima. Akaniambia hakuna
tatizo.
“Pia aliniuliza naishi wapi? Nikamwambia Sinza (Dar)
alionesha dharau kwenye simu akaniambia atanihamishia
Mbezi Beach.
“Aliniuliza natembelea gari gani? Nikamwambia Toyota
Noah. Akaniambia ningependa aninunulie gari gani?
Nikamjibu Toyota Discovery lakini yeye akasema
ataninunulia Toyota Harrier.
“Kweli baada ya siku mbili-tatu nililetewa Toyota Harrier
nyeusi nyumbani. Niliogopa isijekuwa mtego nikaingia
kwenye matatizo hivyo nilimzungusha mtu aliyeniletea
hadi Sinza-Mori nikamwambia apaki kwenye kituo cha
teksi, nikaenda na dereva nikalichukua hadharani ili lolote
likitokea nipate msaada.
“Nilikabidhiwa funguo za lile gari na documents zake,
nikaondoka nalo hadi nyumbani kwangu. Kesho yake
Dallas alimtuma mtu aniletee dola za Kimarekani 15,000
(zaidi ya Sh. milioni 24). Nilipouliza za nini aliniambia ni
kwa ajili ya shopping ya kutembelea Harrier niachane na
zile swaga za kwenye Noah (fedha inaongea). Kisha
akanitumia cheni ya dhahabu.
“Siku iliyofuata alinitumia Sh. milioni 15 nipeleke nyumbani
nikawaambie wazazi nimepata mchumba ambaye
angeenda kujitambulisha baadaye. Niliwaambia ni Dallas
ambaye walikiri kumfahamu kwa sababu alishawapigia
simu na kujitambulisha kuwa ni mkwe wao.”
AMESHAKUTANA NA DALLAS?
“Hadi hapo nilikuwa sijamuona Dallas kwa sura na fedha
nilikuwa natumiwa kila siku.
“Wakati hayo yakiendelea akaagiza nihamishiwe Mbezi
Beach na kununuliwa lile gari lililoibua mzozo BMW X6.
“Nakumbuka siku niliyokabidhiwa lile gari nililia sana.
Sikuamini macho yangu kwa sababu Dallas aliniambia
amenitumia kazawadi kumbe ni BMW X6 (lina stori ndefu
inakuja)!
“Kumbuka mwanzoni nilikuwa na boyfriend ambaye
tulipendana sana lakini hatukupanga kufunga ndoa.
Nilimweleza kila kitu akakubaliana na mimi japokuwa
aliumia.
“Maskini! Kuanzia hapo nikawa nimeachana na yule
boyfriend wangu lakini hakukuwa na namna kwa sababu
niliamini nimepata mchumba wa kunioa.
ATAKIWA KUBADILI DINI
“Baadaye Dallas aliniambia nimeshakuwa mchumba wake
hivyo nibadili dini. Kweli nilibadili nikawa Muislam na jina
langu likawa Ilham. Hicho kilikuwa kipindi kigumu sana
maishani mwangu kwa sababu nilionekana ni muasi katika
dini yangu ambayo mama ni mzee wa usharika na mwimba
kwaya, baba ni mtu wa kanisani sana.”
NINI KILIFUATA?
“Siku moja nilikuwa Tanga nashuti filamu, nilikuwa nikitoka
hapo niende Morogoro. Dallas alinipigia simu akaniambia
yupo Nairobi (Kenya) anakuja Tanzania. Nilimwambia nipo
Tanga akaniambia atanifuata kule. “Niliendelea kupiga
mzigo. Zilipita saa nyingi, baadaye nikiwa na kruu yangu,
Dallas alinipigia simu akaniambia ameniona.
“Nilikataa, akaniambia namna nilivyo, nguo nilizovaa na
watu niliokuwa nao, alipatia. Kumbe alikuja na Toyota
Prado.
WOLPER MORO, DALLAS DAR
“Tulipomaliza kurekodi Tanga tulikwenda Morogoro, yeye
aliniambia anaelekea Dar. Tulikuwa tunawasiliana.
Nilipomaliza kurekodi Moro nilirejea Dar. Hapo ndipo
vituko vikawa juu ya vituko.
“Niliambiwa mara kaonekana sehemu akiwa na mwanamke
au wanawake. Mimi sikujali kwa sababu nilipomuuliza
aliniambia hatuwezi kuonana kwa sababu kipindi hicho
alikuwa katika swaumu hivyo akionana na mimi
nitamharibia. (ulikuwa mwezi mtukufu).
BADO HAWAJAKUTANA?
“(Mguno) Hapo bado hatujakutana lakini yupo mjini na
amejaa tele kwenye kumbi za starehe.
“Baada ya kumaliza swaumu, siku moja aliniambia anakuja
nyumbani Mbezi Beach. Niliwaalika marafiki zangu
tukapika vyakula, tukafanya usafi na kufukiza udi
chumbani. Nilitandika mashuka meupe kitandani na
kujipara kisha nikavaa ushungi kuanzia mchana nikakaa
kama malkia nikimsubiri mchumba.
“Huwezi amini, hadi giza linaingia Dallas hakutia mguu.
Nilipataje aibu kwa rafiki zangu waliotaka kumuona huyo
mchumba? Ninyi acheni tu!
“Nilipomuuliza aliniambia alipata dharura kuna biashara
alikuwa anafanya
HATIMAYE WAKUTANA LAKINI…
“Nilikasirika sana, nikasema huyu ni mchumba gani
asiyetaka kuja kwangu? Nikampa muda wa siku tatu aje
nyumbani na alete nguo zake zote. Kweli, siku ya tatu,
asubuhi nilimsikia mtu akiita ‘Ilham Wolper Dallas’.
Nilishajua sauti yake kupitia simu hivyo nilimkaribisha na
nguo zake nikaingiza ndani. Lakini cha kushangaza alikuja
na pikipiki!
“Alishinda nyumbani siku hiyo maana kuna ndugu zake
walikuja. Hatukufanya chochote. Dallas aliishia kunibusu
shavuni kisha jioni akaondoka.
“Mjini kukawa hakukaliki. Natumiwa picha akiwa na
wanawake tofautitofauti. Mmoja wa wanawake hao
niliambiwa eti ana ‘ngoma’! Jamani hii dunia ina kichaa!
“Muda ukasonga, vitimbi vikawa vingi. Dallas simuoni.
Muda wa kukaa kwenye ile nyumba uliisha hivyo nikahama
na nikamwambia akachukue nguo zake.
UCHUMBA WAVUNJIKA, SASA ANAPUMZIKA HAPA
“Baadaye uchumba ukavunjika tena mimi ndiyo
nilimwambia simtaki tena. Nilikaa muda hadi baadaye
nilipopata mwanaume wangu wa sasa. Anani-control vizuri
kwa sababu kanipita umri na ana busara. Tunapendana
sana. Najuta kumfahamu Dallas. Siwezi kusahau tukio hilo
katika maisha yangu. Dallas alicheza na hisia za moyo
wangu. (akaangua kilio) Niliteseka sana. Ni Mungu tu
anajua…
VIPI KURUDIA UKRISTO?
“Nimekaa muda siendi kanisani. Nilikuwa najifungia ndani
nalia kama mama yangu alivyokuwa anafanya. Siku moja
nilimwambia mwanaume wangu akaniambia kuliko kulia
kila siku bora nirudi kanisani. Ndipo nikarudia ukristo. Kwa
sasa nasali Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),
Usharika wa Kijitonyama, Dar,” alisema.
MBALI NA DALLAS
Kwa mara ya kwanza Wolper alikubali kuorodhesha listi ya
wanaume aliowahi kuwa nao kimapenzi kwa kuwachambua
mmoja mmoja.
ALI KIBA
Bila kupepesa macho, Wolper alikiri kuwa msanii wa Bongo
Fleva, Ali Saleh Kiba ndiye aliyemfundisha mapenzi: “Ni
kitambo kidogo. Wote hatukuwa mastaa lakini yeye
alifanikiwa kuchomoka. Kabla ya Ali (Kiba) nilikuwa na
mwanaume lakini hatukuduu kwa maana ya utu uzima,
ilikuwa yale ya kitoto. Lakini Ali ndiye hasa aliyeniingiza
kwenye ulimwengu wa mapenzi.
KWA NINI WALIACHANA?
“Ali akawa staa. Alipokwenda nje nikasikia wanawake
wanamshobokea. Sasa mimi sikutaka karaha nikakaa
pembeni lakini jamaa ni mtu poa sana na tukikutana
tunasalimiana freshi kabisa.”
DIAMOND VIPI?
“Ni kweli niliwahi kuwa na Diamond (msanii wa Bongo
Fleva, Nasibu Abdul). Tulikuwa na uhusiano lakini pia
alikuwa mshirika wa kibiashara (hataki kuitaja). Yeye
alikuwa hawezi kulala bila kuniona, lakini tulikaa kama
mwezi mmoja, kwa sasa amebaki kuwa rafiki yangu na siyo
mpenzi tena kama zamani,” alisema Wolper.
VIPI KUHUSU JUX?
“Jux (msanii wa Bongo Fleva, Juma Khalid) nilikuwa naye
kabla ya Dallas na yule mwanaume wangu niliyeachana
naye wakati wa Dallas. Katika maisha yangu nilimpenda
sana Jux. Siyo marioo ni mwanaume mtafutaji aliyejiamini.
Kwa sasa sipo naye. Dallas pia alichangia mimi kuachana
na Jux,” alimalizia Wolper ambaye kwa sasa ana
mwanaume asiyependa kumwanika.
-Gpl
Thursday, 28 November 2013
JACKLINE WOLPER "ALIKIBA NDIYE ALIYENITOA USICHANA WANGU",SIWEZI KUMSAHAU KAMWE...!!!....
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment