Rais Jakaya Kikwete ametangaza kuanza mara moja
mpango mkubwa wa ujenzi wa kimataifa wa reli ya
kati baada ya kupatikana kwa mafanikio makubwa
ya ujenzi wa miundo mbinu ya barabara kwa
kiwango cha lami nchini kote.
Mh rais kikwete ametangaza mpango huo mkubwa
wa ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha
kimataifa,wakati akihutumia maelfu ya wananchi
wa mji wa Old Maswa wilayani Bariadi mkoani
Simiyu muda mfupi kabla ya kuweka jiwe la msingi
kwa ujenzi wa barabara ya kilometa 71.7
inayojengwa na kampuni ya cc ya nchini China kwa
kutumia fedha za ndani kiasi cha shilingi bilioni 70.
Hata hivyo rais Kikwete,amesema serikali,imekuwa
ikitumia fedha nyingi katika ujenzi wa
miundombinu ya barabara yakiwemo madaraja ili
kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi, huku akisema
kati ya madaraja makubwa matano yalipangwa
kujengwa baada ya uhuru,rais wa kwanza Mwl
Julius Nyerere ameweza kujenga daraja la Kirumi
mkoani Mara na rais wa awamu ya tatu Benjamin
Mkapa amejenga daraja la mto Rufiji na sasa
serikali yake imekamilisha ujenzi wa madaraja
matatu yaliosalia.
Awali waziri wa ujenzi Mh. John Pombe
Magufuli,akimkaribisha rais Kikwete kuzungumza
na wananchi ambao wamejitokeza kushuhudia
uwekaji wa jiwe hilo la msingi,amesema ujenzi wa
barabara hiyo itakuwa na manufaa makubwa kwa
wananchi wa mkoa wa Simiyu kwa kuunganishwa
na mikoa ya Mwanza na mara pamoja na nchi jirani
ya Kenya,huku mtendaji mkuu wa wakala wa
barabara mhandisi Patrick Mfugale,akitoa kilio kwa
rais kusaidia upatikanaji wa fedha kwa ajili ya
kulipa wakandarasi nchini.
Thursday, 28 November 2013
RAIS JK ATANGAZA KUANZA KWA UJENZI WA KIMATAIFA WA RELI YA KATI.....SOMA HAPA...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment