Thursday, 28 November 2013

JE? WAJUA KWAMBA, KUA NA HIPS AU MAKALIO MAKUBWA....NI ISHARA YA AFYA KITAALAM


Uchunguzi uliofanywa nchini Uingereza umeendelea
kulipandisha chati umbo la kibantu, kwa kusema
kwamba, kuwa na unene zaidi eneo la mapajani,
katika makalio na katika mahips ni vizuri kiafya, na
humzuia mtu asipate matatizo ya kiafya.
Wataalamu wanasema kuwa, mafuta yanayopatikana
katika mahips, huondoa fati asidi mbaya kiafya
ambazo huwa na mada za kuzuia uvimbe ambazo
huifanya mishipa ya damu isizibe. Timu hiyo ya
wachunguzi imesema kuwa, makaliao
makubwa ni bora kuliko mafuta ya zaida
yanayojilundika katika mzunguko wa kiuno, ambayo
hayasaidii chochote.
Wachunguzi hao wamesema katika Jarida la Kimataifa
la Obesiti kwamba, sayansi inapaswa kuangalia jinsi ya
kuongeza mafuta katika eneo la mahips na pengine
katika siku zijazo madaktari watatakiwa kuangalia
njia za kuyahamisha mafuta mwilini na kuyapalekea
katika sehemu za mahips ili kulinda afya za watu
kutokana na magonjwa ya mishipa ya moyo na
magonjwa mengineyo kama kisukari.
Watafiti hao wameeleza kwamba, kuwa na mafuta
kidogo katika hips kunaweza kupelekea matatizo
makubwa ya umetaboli.
Wataalamu hao wameendelea kusema kwamba,
ushahidi unaonyesha kwamba, mafuta yanayozunguka
mapaja na sehemu za nyuma ni vigumu kuyeyuka
kuliko yale yaliyo katika kiuno.
Ingawa suala hilo linaonekama kana kama ni kinyume,
lakini ni kweli kwamba kutoyeyuka huko kuna faida
kwani, wakati mafuta yanapoyeyuka kwa urahisi
hutoa mada inayoitwa cytokines ambayo huleta
uvimbe katika mwili.Mada za cytokines zinahusiana
moja kwa moja na magonjwa ya moyo na kisukari.
Kuyeyuka taratibu kwa mafuta katika mapaja pia
husababisha homoni ya adiponectin izalishwe kwa
wingi na husaidia kudhibiti sukari katika damu na
jinsi mafuta yanavyochomeka.
Dakta Konstantinos Manolopoulos aliyeongoza utafiti
huo kutoka chuo kikuu cha Oxford amesema kuwa, la
muhimu ni umbo na wapi mafuta yanakusanyika, na
kwamba unene wa mahips na mapaja ni mzuri kuliko
unene wa tumbo.

No comments:

Post a Comment