Wakati Kenya, Rwanda na Uganda zimeunda umoja
unaoitwa `Umoja wa Walio Tayari’ , Tanzania, Burundi na
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC ) nazo zimeanzisha
ushirikiano baina yao.
Katika siku za karibuni kumekuwa na mtikisiko ndani ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) baada ya Tanzania na
Burundi kutengwa na wenzao wa Kenya, Rwanda na
Uganda katika baadhi ya masuala muhimu ya ushirikiano
hasa wa kiuchumi.
Tanzania, Burundi na DRC nazo zimekutana ikiwa ni
utekelezaji wa ahadi ya Waziri wa Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Samuel Sitta ambaye aliliambia Bunge lililopita
kuwa Tanzania inafikiria kushirikiana na nchi hizo.
Mkutano wa ujirani mwema
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano
wa Ujirani Mwema uliofanyika mjini Bujumbura, Burundi
jana, Sitta alisema Tanzania, Burundi na Kongo
zimekubaliana kuendeleza miundombinu ya barabara, reli,
anga na usafiri wa maji katika Ziwa Tanganyika.
Alisema mkutano huo ulilenga kuboresha miundombinu ya
usafiri katika Ziwa Tanganyika ambalo linaziunganisha
Burundi Tanzania, DRC na Zambia.
“Pia tumepanga kuendeleza reli ya kati kutoka eneo la
Uvinza, Tanzania hadi Msongati, Burundi na pia
kuunganisha Barabara ya Manyoni - Tabora - Kigoma
kupitia Bujumbura hadi Kivu ya Kusini, DRC, ” alisema Sitta.
Mkutano huo ulihudhuriwa na Sitta pamoja na Waziri wa
Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Burundi, Leontine
Nzeyimana na Waziri wa Uchukuzi wa DRC, Jack Lukeba.
“Pia tulitembelea Bandari ya Kalindo iliyoko katika Ziwa
Tanganyika upande wa Burundi kwani tunataka kuboresha
bandari za ziwa hilo, ” alisema Sitta.
Waziri huyo alisema Tanzania na Burundi zitaunganishwa
na Barabara ya Manyoni – Tabora - Kigoma na Barabara
ya Manyovu - Mgina, Mabanda - Bujumbura
itakayounganishwa mpaka Kivu ya Kusini, DRC.
Kuhusu usafiri wa anga, Sitta alisema nchi hizo zinaangalia
uwezekano wa kuanzisha safari za ndege za Dar es
Salaam mpaka Bujumbura.
Thursday, 28 November 2013
TANZANIA..CONGO NA BURUNDI WAUNDA MUUNGANO WAO BAADA YA KUTENGENGWA..
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment