Siku
ya leo msanii Queen Darleen anasherehekea siku yake ya kuzaliwa,
tumebahatika kufanya nae mahojiano na tumemuuliza ni vitu gani hua
anafanya siku kama ya leo na Queen alisema ” Siku kama ya leo inapofika
saa 6 (Usiku) kama mwili wangu haupo msafi basi natia udhu kisha naanza
sala na kumuomba mwenyezi Mungu kwa sababu kuna kuugua na pia kuna
kufakwa najaribu kumuomba mwenyezi Mungu anisaidie uhai mrefu”
Alipoulizwa
kuhusu kama atafanya sherehe, Queen Darleen alisema ” Sijawahi kufanya
sherehe mimi kama mimi lakini leo marafiki zangu wakina Mwasiti, Almasi,
K Star Diamond kina shilole wote wameamua kunifanyia kitu hapa nyumbani
kwangu kuanzia saa 2 usiku, mi sijui ni kitu gani watanifanyia. Kwa
hiyo suprise lakini nimesema sitaki zawadi ya gari, nimeshampa warning
kabisa Diamond”
No comments:
Post a Comment