
Picha ya mtandaoni ya Christina Kigahe
Mfanyabiashara
na mkazi wa Mikocheni, Christina Kigahe (36) jana alipandishwa katika
kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka
matatu ya kuingiza nchini dawa za kulevya zenye thamani ya zaidi ya Sh99
milioni.
Wakili
wa Serikali, Janeth Kitali alidai mahakamani hapo kuwa Desemba 11,
2013, mshtakiwa alikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere (JNIA) akiingiza nchini gramu 1227.37 za dawa za kulevya aina
ya Heroine Hydrochloride zenye thamani ya Sh55,231,650.
Kitali
alidai kuwa siku hiyo ya tukio, mshtakiwa huyo pia alikamatwa akiingiza
nchini gramu 670.06 za dawa za kulevya aina ya Heroine Hydrochloride
zenye thamani ya Sh30,152,700.
Alidai
kuwa Chritina siku hiyo hiyo ya tukio pia alikamatwa akiingiza kiasi
kingine cha dawa za kulevya aina ya Heroine Hydrochloride kiasi cha
gramu 310.02 chenye thamani ya Sh13,950,900.
Hata
hivyo, mshtakiwa aliyakana mashtaka hayo na upande wa mashtaka ulidai
kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na hivyo kuomba kesi hiyo
ipangiwe tarehe nyingine ya kusikilizwa.
No comments:
Post a Comment