Mbeba
‘niuzi’ wa awamu hii ni Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,
Josephat Gwajima, baada ya Mbasha kuona isiwe tabu, hivyo kuamua
kupambana na mtumishi huyo wa Mungu kwa njia ya kiroho zaidi.
Habari
zinadai kuwa, mbele ya Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste
Mkoa wa Dar es Salaam, Bruno Mwakibolwa ambalo Gwajima ni memba hai,
ameshapokea mashitaka kuhusu mchungaji huyo kuhusika kuitikisa ndoa ya
waimbaji hao wa Neno la Mungu na mlalamikaji ni Mbasha mwenyewe.
Wikiendi
iliyopita, Mbasha aliketi na kiongozi huyo na kushusha tuhuma zake
dhidi ya Gwajima kama zilivyothibitishwa na mlalamikaji mwenyewe, nazo
ni hizi zifuatazo;
MOSI; Gwajima ni kiongozi wa kiimani wa Mbasha na Flora lakini tangu matatizo ya ndoa yao yalipojitokeza, mchunga kondoo huyo wa Bwana hajawahi kufanya lolote kunusuru muunganiko huo uliohalalishwa kwa jina la aliye juu.

Emmanuel Mbasha
PILI;
Gwajima anajua kila kitu kuhusu mgogoro wa Mbasha na mkewe lakini
kipindi chote cha matatizo, Kanisa la Ufufuo na Uzima limekuwa mfadhili
wa Flora kwa sehemu kubwa. Hapa anauliza, huu ufadhili una kipi nyuma
yake?
TATU;
Gwajima anatambua kuwa Flora ni mke wa mtu, mwenye mali ameshaomba
aachiwe mwandani wake bila mafanikio. King’ang’anizi kina msukumo upi?
NNE; Gwajima amekuwa akimuumiza Mbasha kihisia, kiakili na kiroho kwa sababu yeye anagombana na mkewe lakini mchungaji huyo bila kufikiria maumivu aliyonayo, humwita Flora madhabahuni katika ibada na kumpa nafasi ya kuimba.

TANO;
Flora anaishi hotelini na yeye mwenyewe alishakiri kuwa fedha za kulipia
hoteli alizipata kutokana na michango ya waumini wa Kanisa la Ufufuo na
Uzima. Hapa Mbasha analalamika, inakuwaje kanisa limfadhili mke wa mtu
kuishi hotelini ikiwa mumewe hajui?
SITA;
Katika hoja zote hizo, Mbasha amelieleza Baraza la Maaskofu wa
Kipentekoste kuwa hana imani na Gwajima kwa vile kama ni busara baada ya
kuona ndoa hiyo imetikisika yeye (Gwajima) angekaa pembeni kwa namna
yoyote ile, hivyo Mbasha akaiomba menejimenti ya baraza hilo kumpa
adhabu kali mwenzao.
Mbasha
alipozungumza na Amani, Jumanne iliyopita, alisema baraza hilo
liliahidi kushughulikia shauri lake na uamuzi utachukuliwa baada ya
kumwita Gwajima na kumsikiliza kwa upande wake.
WENYE KWENU KWAHERI!
Kesi ya Mbasha kudaiwa kumbaka shemeji yake ilipoanza, mume huyo wa Flora alikimbilia mafichoni, kwa hiyo swali kwamba anaabudu kwenye kanisa gani halikuwa na mashiko kwa sababu mhusika mwenyewe hakuwa akionekana.

Baada
ya Mbasha kujitokeza na kufikishwa mahakamani, kupelekwa mahabusu kwenye
Gereza la Keko kabla ya kuachiwa kwa dhamana, ndipo swali kuwa anaabudu
kanisa gani lilipoanza kutokana na ukweli kuwa yupo uraiani kwa
‘bondi’.
Swali
hilo lilitokana na hoja kwamba kabla ya mgogoro na mkewe walikuwa
wakisali kwenye Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Gwajima
ambaye alishamtuhumu kumfadhili Flora na akamtaka amwachie ‘waubani’
wake huyo ili maisha yaendelee.
Jawabu
la swali hilo, lilijibiwa Jumapili iliyopita baada ya Mbasha kutinga
Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT), maarufu kama
Mito ya Baraka, linaloongozwa na Mchungaji Bruno Mwakibolwa, na
kukamilisha haja zake za kuabudu pale.
Mbasha
alipozungumza na Amani kuhusu kusali kwa Mchungaji Mwakibolwa badala ya
kwa Gwajima, alijibu: “Nimehama Kanisa la Ufufuo na Uzima, sisali tena
kule. Kuanzia sasa shughuli zangu za kuabudu nitazifanyia Mito ya Baraka
kwa Mchungaji Mwakibolwa.
“Siwezi
kwenda kwa Gwajima kwa sababu simuelewi na ndiyo maana nimeamua
kumshtaki kwa Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste. Roho yangu ya kuabudu
isingekuwa timilifu, ingejaa mashaka kwenda sehemu ambayo imenijeruhi na
nisiyoiamini.
“Kwa
kifupi si kwamba nimeanza kuabudu Mito ya Baraka hili ndilo kanisa letu
tangu zamani, mimi na mke wangu. Tulihamia Kanisa la Ufufuo na Uzima
baada ya Gwajima kutushawishi, kwa hiyo nimerejea kundini.
MCHUNGAJI MWAKIBOLWA
Juzi, Amani lilimsaka Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Mkoa wa Dar es Salaam, Mchungaji Mwakibolwa lakini simu yake ilipokelewa na kusikika sauti za watu wakiwa kwenye maombi kama si ibada.
Juzi, Amani lilimsaka Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Mkoa wa Dar es Salaam, Mchungaji Mwakibolwa lakini simu yake ilipokelewa na kusikika sauti za watu wakiwa kwenye maombi kama si ibada.
GWAJIMA
Baada ya hapo, Amani lilimsaka Mchungaji Gwajima kwa njia ya simu yake ya mkononi lakini yeye hakupokea hata pale alipopigiwa kwa kurudiarudia.
Baada ya hapo, Amani lilimsaka Mchungaji Gwajima kwa njia ya simu yake ya mkononi lakini yeye hakupokea hata pale alipopigiwa kwa kurudiarudia.
KESI YA MBASHA
Kesi ya Mbasha kudaiwa kubaka itatajwa tena Julai 17, mwaka huu kwenye Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam.
Kesi ya Mbasha kudaiwa kubaka itatajwa tena Julai 17, mwaka huu kwenye Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam.
VIPI KUHUSU KUPATANA?
Habari zinasema, taratibu hizo zinandelea licha ya Mbasha kumshitaki Gwajima kwenye Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste Mkoa wa Dar es Salaam.
Habari zinasema, taratibu hizo zinandelea licha ya Mbasha kumshitaki Gwajima kwenye Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste Mkoa wa Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment