Kupitia
paparazi, Juni 13, mwaka huu, Nabii Bendera alisema ameoneshwa kwamba
wasanii 20 wangekufa hivyo kama wanataka kujinusuru, wafike kanisani
kwake na kupakwa mafuta.
Wakati paparazi tulipoingia mtaani, ukurasa wa mbele uliambatanisha picha mbalimbali za baadhi ya wasanii waliofariki pamoja na wengine ambao wapo hai akiwemo Aunt Ezekiel (pichani) ndipo utata ulipoanzia.
Wakati paparazi tulipoingia mtaani, ukurasa wa mbele uliambatanisha picha mbalimbali za baadhi ya wasanii waliofariki pamoja na wengine ambao wapo hai akiwemo Aunt Ezekiel (pichani) ndipo utata ulipoanzia.
Chanzo
kilicho karibu na staa huyo, kilipenyeza habari kuwa, ndugu zake
walimpigia simu Aunt ambapo walionesha kuwa na hofu ya kifo ambayo
ilimfanya mwigizaji huyo naye aangue kilio mara kwa mara.
“Ndugu zake walilia sana kwani baada ya kuona picha ya Aunt katika paparazi, waliamini maneno ya nabii huyo kwa kujua pengine anayefuata kufa kati ya hao kumi ni ndugu yao.
“Ndugu zake walilia sana kwani baada ya kuona picha ya Aunt katika paparazi, waliamini maneno ya nabii huyo kwa kujua pengine anayefuata kufa kati ya hao kumi ni ndugu yao.
“Aunt
alilia sana siku hiyo na Wema (Sepetu) ndiye alisimama kumsihi
asiendelee lakini kama haitoshi, bado amekuwa akiteseka mara kwa mara
kila anapokumbuka tu, anakosa amani na kujikuta analia,” kilisema
chanzo.
Hata
hivyo, chanzo kimeeleza kuwa baada nguvu kubwa kutoka kwa marafiki wa
karibu wa Aunt akiwemo Wema wamekuwa wakimsihi amuombe Mungu kwani si
kwamba picha yake kutumika paparazini ndiyo atakufa wala maneno ya nabii
huyo si sababu ya kuamini kwamba kweli vifo hivyo vitatokea.
“Wamemtaka
amuombe Mungu na kutosikiliza maneno ya watu maana kuna watu ambao
wamekuwa wakishadadia ishu hiyo katika mitandao na kumfanya Aunt aingiwe
na hofu ya kifo, kidogo ameanza kuwaelewa,” kilisema chanzo.
Baada
ya kupata habari hizo,paparazi tulimtafuta Aunt, alipopatikana aliweka
wazi kuwa suala hilo limemkosesha amani sana pamoja na ndugu zake.
“Walijua
ndiyo nakufa, na mimi pia niliposikia harakaharaka niliamini nimetajwa
mimi hususan waliponiambia picha yangu imetumika paparazini, nililia
sana siku hiyo na siku zilizofuata pia watu walizidi kuniliza
mitandaoni, mwisho wa siku nimemwomba Mungu anisimamie, atakaponichukua
ni kwa mapenzi yake kama maandiko yanavyosema,” alisema Aunt.
Kwenye
utabiri huo, nabii huyo alinukuliwa kuwa ndani ya mwezi Juni, idadi ya
wasanii 20 wangefariki lakini hadi sasa hakuna kifo chochote
kilichotokea hali ambayo inawafanya baadhi ya watu kuamini kwamba
masuala ya kifo ni Mungu pekee anayejua nani atakufa lini.
No comments:
Post a Comment