KUTOKANA na
hivi karibuni mumewe, Hamis Baba ‘H. Baba’ kuugua ugonjwa wa homa ya
Dengue ‘Dengi’ na kulazwa Muhimbili, msanii wa filamu Bongo, Flora
Mvungi amesema alijikuta kwenye wakati mgumu kuhofia mumewe angepoteza
maisha.
Akizungumza
na paparazi hivi karibuni, Flora alisema ni Mungu tu mumewe kupona
kwani alikuwa katika hali mbaya ambayo mpaka yeye kama mkewe alikuwa na
hofu kubwa ya kifo haswa ukizingatia vifo vya wasanii vilivyotokea
mfululizo.
“Nilipoona
wasanii wenzangu wakifariki dunia na mume wangu kuzidiwa mpaka kulazwa
Muhimbili, nilikuwa nina hofu kubwa ya kifo lakini namshukuru Mungu
amepona na tunaendelea na maisha kama kawaida, dengue noma sana,”
alisema Flora.
No comments:
Post a Comment