PSPF KUPITIA PSS YAZIDI KUCHIMBA HADI MIZIZI KATIKA KUFANIKISHA KUWAFIKIA WANANCHI KWA URAHISI
Afisa
mfuko wa pensheni wa pspf Hadji.H.Jamadary akizungumza namna yakuweza
kufaidika na uchangiaji wa hiari katika mfuko wa pensheni wa PSS.
Debora
Danniel afisa masoko PSPF ambaye alikuwa akifanya zoezi la kusajiri
wanahisa wa kikundi cha Tandika Grain Agents Company PLC baada ya semina
Mmoja
wa wanachama akifuatilia kwa makini maelezo ya majibu baada ya kuuliza
swali ambalo lilijibiwa na maofisa wa mfuko wa pensheni kuhusu
uchangiaji wa hiari Bw.Rashidi Iloko
Bw.Hemed Abdullah akiwa makini kufuatilia
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Tandika Grain Agents plc Bw.Hassani Abdallah Matimbula
Afisa masoko PSPF Debora Danniel akiwagawia vipeperushi vikiwa vina elezea PSS mfuko wa hiari
Afisa masoko Akiwa katika usajiri wa wanachama walio weza kujiunga na mfuko wa hiari
Zoezi la upigaji picha likiwa linaendelea kwa walio jaza fomu za kujiunga na mfuko wa huari PSS
baadhi ya wanahisa wa chama cha Tandika Grain agents comany plc
Maofisa wa
mfuko wa penshe wakitoa shukrani kwa wanachama walio weza
kuhudhuria semina,kutoka kushoto ni Debora Danniel na kulia ni Hadji
Jamadary.
Leo
katika kuendelea kuchimba kwa mizizi kwa kuwapa elimu wananchi
mbalimbali mfuko wa pensheni wa Pspf katika mpango wa kuchangia kwa
hiari Pss umeweza kuwafikia wananchi wa Tandika na mashirika mbalimbali
wameweza kuhudhuria katika semina hiyo iliyo andaliwa na mfuko huo
semina
hiyo ililenga katika wafanya biashari wa aina mbalimbali ambao
hujulikana kama wajasiliamali ambapo kufuatiwa kwa wafanyabiashara hao
kufika na kuweza kupata elimu nayo kampuni ya Tandika Grain Agents
Plcambayo inajishughulika na uuzaji wa nafaka mbalimbali iliweza kufika
na wanachama wake ili kupta elimu itakayo wasaidia katika kuendeleza
biashara yao na maendeleo ya familia zao
Akizungumza
na wanachama walio hudhuria semina hiyo Afisa mufuko wa Pensheni wa
PSPF Bw.Hadji Jamadary mbaye ndiye aliye kuwa akitoa maelezo katika
semina hiyo alianza kwa kuwafahamisha mfuko wa pensheni wa PSPF ni nini
na kuweza kuwapa utangulizi wa wa semin hiyo ambayo ilikuwa ikilenga
uchangiaji wa hiari (PSS).
Vilevile
aliweza kutoa ufafanuzi wa namna ya kujiunga ,manufaa utakayo yapata
endapo utajiunga na mfuko huu wa PSPF kwa mpango wa hiari PSS ambapo
aliwaeleza kuna namna ya mafao ambayo unaweza ukachagua ili kuweza
kuendelea kuchangia ambapo aliyataja mafao hayo ambayo ni Fao la elimu,
fao la ujasiriamali,fao la uzeeni,fao la kifo,fao la ugonjwa na fao la
kujitoa aliweza kutoa ufafanuzi katika kila fao ambapo kwakuwa semina
ilikuwa na wafanyabiashara aliweza kuwa fundisha kuhusu fao la
ujasiliamali na faida zake .
Baada
ya kutoa maelekezo hayo wafayabiashara waliruhusiwa kuuliza maswali na
kuweza kuchagua na kujiunga na mpango huo wa hiari .
Nao
wafanya biashara hususani katika kampuni ya Tandika Grain Agents Plc
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Bw.Hassani Matibula aliweza
kuwashukuru waelimishaji na waandaaji wa semina hiyo hususani mfuko wa
PSPF kuweza kuwafikia sehemu waliko na kuwafungu kwakuwa hawakuweza
kupata watu watakao kuja na kuwapa elimu ya kuwajenga katika biashara
zao alitoa wito kwa wafanya biashara wenzake waweze kujiunga ili waweze
kupata manufaa na kuhifadhi sehemu salama kw fedha zao.
No comments:
Post a Comment