Friday, 6 June 2014

MBUNGE JOSHUA NASSARI KUFANYA HARUSI YA ALAIKI KESHO JIMBONI KWAKE

     

MBUNGE JOSHUA NASSARI KUFANYA HARUSI YA ALAIKI KESHO JIMBONI KWAKE

Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Meru Dr PaulBAkyoo akifanya maombi kwa Bw Joshua Nassari ,Mbunge wa jimbo laNArumeru Mashariki na Bi Anande NNnko wanaotarajia kufunga ndoa JumamosiNhii.

Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari akimwimbia mchumba wake Bi Anande Nnko wakati wa sherehe ya Send off iliyofanyika nyumbani kwao na Bi Harusi Mtarajiwa ,Meru.
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari akiwa amekumbatiana na Mchumba wake Bi Anande Nnko muda mfupi baada ya kumtafuta kwa muda katika sherehe ya Send Off iliyofanyika nyumbani kwa Bi Harusi Mtarajiwa ,Meru.
Bi ,Harusi Mtarajiwa Anande Nnko akimpatia zawadi ya T-Shirt Mumewe Mtarajiwa Bw Joshua Nassari wakati wa sherehe ya Send Off iliyofanyika nyumbani kwao Meru.

Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.

MBUNGE wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Mh Joshua Nassari kesho anatarajia kufunga ndoa na Bi Anande Nko katika kanisa la Pentekoste, Kilinga lililoko wilaya ya Meru ambako Mh Nassari alianzia masuala ya Kiimani ikifuatiwa na Sherehe kubwa ya Harusi itakayo fanyika katika viwanja vya Usa-River Academy jirani na Hotel ya Ngurdoto.

Kwa Mujibu wa Mh Nassari ,sherehe hizo zitakazoanza majira ya saa saba mchana  watu wote wamealikwa wakiwemo ndugu, marafiki, Jamaa na wananchi jimbo la Arumeru Mashariki kwenye tukio hilo na kamba hakuna
kadi.

"Nichukue tena fursa hii kuwakaribisha ndg, marafiki, Jamaa na zaidi sana
wananchi wangu wa jimbo la Arumeru Mashariki kwenye tendo hadhimu la
kusherekea harusi yangu , Jumamosi Juni 7, Usa-River academy grounds
kuanzia saa saba mchana. Kwa Pamoja Tulianza na Mungu, Tutamaliza na
Mungu Pamoja. ...No cards on entrance!"alisema
Nassari.

Na ssari amesema watu zaidi ya 8000 wanatazamiwa kushiriki katika sherehe hiyo ya aina yake wakiwemo viongozi mbalimbali na wabunge kutoka maeneo mbalimbali
     

No comments:

Post a Comment