Profesa
Hassan Bical Mshauri katika Bodi ya Chuo akionesha baadhi ya Nakala ya
Gazeti la Citezens lilivyoandika habari zisizo za ukweli, kushoto ni
Nabeel Almandhy.
Waandishi wa habari na Mhariri wa gazeti la The Citizen wanakurupuka
kuandika stori bila ya kufanya uchunguzi wa kina juu ya habari
wanazopata, pamoja na kuhoji upande wa pili wa wahusika.
Hayo yalisemwa na Profesa Hassan Bical Mshauri wa Bodi ya Chuo cha
Cyprus baada ya gazeti hilo kuandika makala ya chuo hicho hakitambuliki
hapa nchini na nje ya nchi na wanafunzi 200
wanasoma chuo hicho taaluma
inayotolewa katika chuo hicho na vyeti ni feki, kwa kufuatia kuandika
kwa taarifa hiyo, gazeti la The Citizen wamepewa saa 48 kuanzi sasa
kuomba radhi kwa kuandika kitu ambacho cha uwongo.
Kama hawajaomba radhi kwa saa hizo basi gazeti hilo watalipeleka
Mahakamani kwa kuandika habari za uwongo, ambazo hazijafanyiwa
uchunguzi.
“Wanatakiwa kuandika makala za uchunguzi sio kukurupuka na kuandika
stori bila ya kuwa na uhakika wa ukweli wa stori hiyo, na wasichanganye
mambo ya elimu na siasa wanatakiwa wajue kuwa elimu ni kitu cha msingi
sana kwa nchi ya Tanzania na siasa ni siasa tu.”alisema Profesa Bical.
Aidha kabla ya kuitisha mkutano Profesa alipiga simu kwa mara ya
kwanza ilipokelewa lakini hawakuelewa na aliyepokea simu, alipiga simu
mara ya pili lakini simu haikupokelewa, ndio akaamua kuitisha mkutano
huo.
Chuo hicho kwa sasa kinatambulika na umoja wa vyuo vikuu duniani
(INQAAHE) lakini pia kuna wanafunzi 70 kutoka nchi mbalimbali duniani,
chuo cha 641 kujulikana duniani na kinawakilisha nchi 120 duniani.

No comments:
Post a Comment