Maandamano
ya wananchi wa mji mdogo wa sirari wilaya ya Tarime mkoani Mara
waliotaka kujua chanzo cha mauaji ya kijana mmoja mkazi wa eneo hilo
ambaye anadaiwa kukamatwa na Jeshi la polisi na kisha mwili wake kukutwa
katika chumba cha kuhifadhiwa maiti katika hospital ya wilaya ya Tarime
yamesababisha vurugu kubwa na kusimama kwa shughuli mbalimbali za
kijamii kwa saa kadhaa
Kijana
huyo aliyefahamika kwa jina la kitandika Ryoba anadaiwa kukamatwa siku
nne zilizopita na askari wa jeshi la Polisi katika mkoa wa kipolisi
Tarime Rorya kwa tuhuma za kukutwa akicheza kamali lakini tangu siku ya
tukio hilo kijana huyo hakupatikana hadi taarifa za kifo zilipowafikia
ndugu zake na mwili wake kuhifadhiwa katika chumba cha Maiti katika
hospital ya wilaya ya Tarime
Taarifa
hizo zilisababisha wananchi wa eneo hilo kufanya Maandamano ikiwa ni
njia ya kushinikiza jeshi la Polisi kueleza chanzo cha kifo cha
kijana huyo ambapo jeshi la polisi liliingia kati kuzima maandamnao hayo
hali ambayo ilisababisha wananchi hao kuifunga barabara kuu ya
inayotumika kwa safari za Mwanza,Tarime na nchi jirani ya Kenya kwa
kutumia Mawe lakini pia wakichoma matairi ya Magari.
Kwa
upande wake Kamanda wa Polisi kanda Maalum ya Tarime Rorya Kamishana
msaidizi Mwandamizi Justus Kamgisha amesema Mtuhumiwa huyo kitandika
Ryoba baada ya kukamatwa alifikisha kituo cha Polisi kuhojiwa na wakati
Mahojiano yakiendelea alidai kujisikia vibaya ambapo nalikimbizwa
hospital na wakati anapatiwa matibau akafariki dunia. -






No comments:
Post a Comment