Tuesday, 27 May 2014

NJEMBA ‘AWAVUA’ NGUO WEMA, AUNT EZEKIEL



NJEMBA ‘AWAVUA’ NGUO WEMA, AUNT EZEKIEL

Mastaa
wawili wa Filamu za Kibongo, Wema Sepetu na Aunt Ezekiel walikipata cha
moto walipokuwa kwenye msiba wa Adam Kuambiana, Bunju nje kidogo ya
Jiji la Dar, baada ya kutukanwa na njemba mmoja aliyekuwa amelewa.




Mastaa wawili wa Filamu za Kibongo, Wema Sepetu na Aunt Ezekiel wakiwa katika Msiba wa Adam Kuambiana.
Sakata
hilo lilijiri usiku mwingi wakati  mastaa hao walipokuwa wameenda
kulala kwenya matanga ambayo yalihudhuriwa na mastaa kibao, nyumbani kwa
mke wa marehemu


Mwanaume
mmoja (jina lake halikupatikana) alianza kumtukana Wema kuwa hana uzuri
wowote kama walivyokuwa wakimuona kwenye runinga.
Kitendo cha njemba huyo, kilimkera Wema na kuanza kujibishana naye, Aunt akaununua ugomvi na kujikuta naye akitemewa mbofumbofu.
Hata
hivyo, mwisho wa sakata hilo Wema na Aunt waliamua kunyamaza kwani
walibaini kuwa walikuwa wakijibishana na mtu ambaye ‘network’ yake
ilikuwa bize kwa gambe.

No comments:

Post a Comment