Wednesday, 28 May 2014

MREMBO ANASWA KAVAA NGUO ZA KUAMBIANA:kumbe ni kimada alipewa na marehemu amfulie kabla ya umauti kumfika... soma zaidi hapa mrembo akifunguka!!



MREMBO
ANASWA KAVAA NGUO ZA KUAMBIANA:kumbe ni kimada alipewa na marehemu
amfulie kabla ya umauti kumfika... soma zaidi hapa mrembo akifunguka!!

Takribani
siku kumi tangu alipofariki dunia  Kuambiana (38), mrembo
aliyejitambulisha kwa jina Mary Njombe amenaswa na nguo za staa huyo
wakati mali za marehemu hazijagawanywa.


Mary Njombe aliyenaswa akiwa amevaa nguo za marehemu Adam Phillip Kuambiana.
Kwa
mujibu wa vyanzo vyetu makini, Mary ambaye ni mkazi wa Magomeni
Hospitali, Dar amekuwa akipigilia pamba za marehemu hasa baada ya jamaa
huyo kutangulia mbele ya haki.


“Jamani
njooni huku Magomeni Hospitali hapa mtaa wa pili kuna mwanamke anatinga
nguo za marehemu Kuambiana,” kilisema chanzo chetu.
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, paparazi alifanya msako eneo hilo hadi wakamnasa Mary.

Katika
mahojiano na paparazi, Mary alisema kuwa alikuwa mchumba wa Kuambiana
na alichobahatika kubaki nacho ni nguo ambazo alimpatia mara ya mwisho
amfulie (zinaonekana pichani).


Mary alisema kuwa yeye na Kuambiana walifahamiana tangu mwaka 2006 ambapo alikuwa akimbembeleza kuwa naye.
“Mwaka
2008 ndiyo tulianza rasmi uhusiano kwani mimi nilikuwa sina mwanaume na
yeye hakuwa na mtu hivyo tulikubaliana na alikuwa akijulikana nyumbani
kwetu,” alifunguka Mary.
Mwanadada
huyo alisema kuwa yeye na Kuambiana walikuwa wakikutana kwenye Hoteli
ya Grand iliyopo Magomeni, Dar na mara nyingi alikuwa akimpikia chakula
na kumpelekea ‘lokesheni’.


“Nimeumia
sana na sijielewi, Kuambiana ameniachia donda kubwa, nakumbuka neno la
mwisho aliniambia nimpende sana kwani ipo siku nitamkubuka,” alisema
Mary huku akiangua kilio.
Adam Phillip Kuambiana enzi za uhai wake akiwa amevaa shati alilonaswa nalo mrembo.
Alipoulizwa
kama kweli nguo hizo ni za marehemu Kuambiana, alizama ndani akatoka
akiwa amevaa pensi na shati la ‘drafti’ alilokuwa anapendelea kulivaa
staa huyo ambalo ni maarufu sana.


Kuambiana alifariki dunia usiku wa kuamkia Mei 17, mwaka huu baada ya kuanguka chooni kutokana na kusumbuliwa vidonda vya tumbo.

No comments:

Post a Comment