Staa wa Bongowood, Blandina Chagula ‘Johari’.
Tukio
hilo lilichukua nafasi kwenye msiba wa mwigizaji Sheila Haule ‘Recho’
Sinza-Palestina, Dar, hivi karibuni ambapo vijembe viliibuka baada
Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Nyerere’ kumuuliza kwa
lugha ya utani Chuchu kuwa RJ itachangia nini msibani hapo, Johari
akadakia:
“Kampuni yangu si ya uchochoroni au ya chumbani, nina TIN namba kabisa siyo kama hiyo nyingine, iweje umuulize asiyehusika...”
Baada ya Johari kutamka maneno hayo, waombolezaji waliokuwepo msibani hapo walipigwa na butwaa na kuhoji kulikoni?
Mastaa wa Bongo Muvi akiwemo Chuchu Hans (wa pili kushoto) wakiwa msibani kwa Recho.
Johari
amekuwa akidaiwa kuwa na uhusiano na Ray kipindi cha nyuma huku kukiwa
na taarifa kuwa Chuchu ana kampuni iitwayo Chura ikimaanisha Chuchu na
Ray hivyo ilitafsiriwa kuwa alikuwa akiipiga kijembe kwa madai kuwa
haiwezi kufikia levo za RJ.
Alipofuatwa
na paparazi ili kupata ufafanuzi juu ya ishu hiyo, Johari hakuwa tayari
kwani alisema ana majonzi ya kuondokewa na kipenzi chake Recho hivyo
hakutaka malumbano na watu katika kipindi hiki kigumu.
No comments:
Post a Comment