Mwinjilisti ambaye jina lake halikufahamika mara moja akikagua vifaa vya wachawi baada ya kuangushwa.
Tukio
hilo la aina yake lilijiri usiku wa Mei 25, mwaka huu maeneo ya
Tazara-Maghorofani, Dar hivyo kuibua hofu kubwa kwa wakazi wa eneo hilo
wakihofia kulogwa.
Habari zilieleza kwamba alfajiri ya siku ya tukio hilo, watu waliona matunguri kwenye uchochoro unaokatiza katika nyumba zao.
Watoto wakishuhudia tukio hilo.
Ilielezwa
kwamba baadhi ya watu walidai kuwa matunguri hayo yalidondoshwa na
wachawi waliopita eneo hilo wakielekea kuwaloga watu mahali fulani na
kuongeza kuwa inawezekana kutokana na kanisa kuwa karibu na eneo hilo
ndipo wakapata tafrani angani kiasi cha kudondosha rada zao.
Watoto wakizishangaa tunguri za wachawi.
“Hapa
lazima wachawi walikuwa wanakwenda kuloga sehemu, lakini kutokana na
kanisa kuwa karibu na njia zao wakajikuta wakipita kwa tabu. Mwishowe
wakadondosha mizigo yao,” alisema mmoja wa mashuhuda.
Ilidaiwa
kuwa umati uliofurika eneo hilo ulipatwa na wasiwasi na kutafuta msaada
wa kiroho kwa kuwatafuta wachungaji wa kanisa hilo ambapo walikutana na
wainjilisti wawili ambao walifika eneo la tukio na kuvikusanya vifaa
hivyo kwenye kiroba huku wakiviombea.
Kuhusu maji meusi ilidaiwa kuwa hutumiwa na wachawi wasionekane wakiwa katika shughuli zao.
Wakizungumza
na paparazi baada ya kuvikabidhi vifaa hivyo kanisani kwa ajili ya
kuvichoma, wainjilisti hao waliojitambulisha kwa majina ya Amos Beda na
Innocent Gervas wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) walisema
kuwa, vifaa hivyo vinaonekana kuwa na uhusiano mkubwa na nguvu za giza.
Walimtaka mwenye navyo kujitokeza kanisani ili amrudie Mungu.
No comments:
Post a Comment