Wednesday, 2 April 2014

UTAJIRI WA MASANJA KUFURU:ANAMAGARI 6 YA KIFAHARI,KAMPUNI YA ULINZI NA MASHAMBA YA MPUNGA



UTAJIRI WA MASANJA KUFURU:ANAMAGARI 6 YA KIFAHARI,KAMPUNI YA ULINZI NA MASHAMBA YA MPUNGA

UTAJIRI wa komediani maarufu Bongo, 
Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ ni kufuru! Tena unatisha na sasa
anaonekana kuwa miongoni mwa wasanii wanaomiliki fedha na mali nyingi
Bongo, 
Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ akiwa mbele ya usafiri na mjengo wake.

Awali, habari kuhusu utajiri wa
Masanja ilitua mezani kama kidokezo, hapo mwandishi wetu akaingia
mzigoni na kuanza kuchunguza kwa kina mali anazomiliki msanii huyo na
kugundua kuwa ni kati ya mastaa mabilionea Bongo.
“Masanja sio yule tena. Ana mpunga
(fedha) mrefu sana. Hakuna msanii wa maigizo Bongo anayeweza kumfikia
kwa sasa. Hao wengine ni mbwembwe tu, lakini pesa imelala kwa Masanja,”
kilipasha chanzo chetu.
Kikaongeza: “Kwanza ana ghorofa lipo
Tabata, hapo ndipo anapoishi. Pia ana magari kibao ya kifahari, mashamba
ya mpunga na Kampuni ya OK Security inayolinda sehemu mbalimbali
zikiwemo taasisi nyeti nchini.
Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ akiwa kwenye pozi na miongoni mwa magari yake.
“Ni msanii gani mwenye kampuni kubwa
kama ya Masanja? Wengi wanaishia kudai wanatayarisha filamu ambazo hata
matunda yake hayaonekani.”

Mdogomdogo, Risasi Mchanganyiko likajitupa mtaani kuchimba kuhusu madai hayo ambayo awali liliyatilia shaka kama si wasiwasi.
Uchunguzi wetu ulibaini ukweli wa mali za msanii huyo na mambo mengine mengi yanayoingia kama vyanzo vya mapato yake.
MAGARI SITA
Ilibainika
kuwa, Masanja anamiliki magari sita, yakiwemo ya kifahari. Baadhi ya
magari hayo ni Toyota Land Cruiser V8, Nissan Hardboad na Toyota
Verossa.

NYUMBA TATU BONGO
Pia,
mkali huyo wa kuvunja mbavu, anamiliki nyumba tatu za maana jijini Dar
es Salaam, moja ni ghorofa ipo Tabata, nyingine Kigamboni na nyingine
haifahamiki eneo rasmi ilipo.
Hata hivyo, imebainika kuwa mbali na mijengo yake hiyo iliyopo jijini Dar, nyumbani kwao Mbarali, Mbeya ana mjengo wa maana.

MASHAMBA KIBAO
Msanii
huyo hayupo nyuma kwenye kilimo, ana mashamba kadhaa Kigamboni jijini
Dar es Salaam lakini linalotia fora ni lile lililopo Mbarali lenye
ukubwa wa hekari 50 ambalo analima mpunga.

NI MSANII WAMAIGIZO TAJIRI ZAIDI?
Kwa utajiri huo, ipo minong’ono kuwa, nyota huyo anaweza kuwa kwenye namba za juu za wasanii wa maigizo wenye mkwanja mrefu.
Wengine
wanaotajwa kwenye orodha ya waigizaji matajiri Bongo ni Husna Posh
‘Dotnata’, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ na Amri Athumani ‘Mzee Majuto’.
MATAJIRI BONGO FLEVA
Katika
muziki wa Bongo Fleva, wasanii wanaoaminika wana utajiri mkubwa zaidi
ni Judith Wambura ‘Lady Jaydee’, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Joseph Haule
‘Profesa Jay’.
Wasanii hao wanamiliki mijengo ya maana, achilia mbali magari ya kifahari na miradi kadhaa.

MASWALI KUHUSU MASANJA
Utajiri
wa Masanja umeonekana kuibuka ghafla huku vyanzo vyake vya kumwingizia
kipato vikijulikana ni sanaa ya uigizaji, muziki na huduma ya uchungaji.
Je, kwa uigizaji tu katika Kundi la Orijino Komedi ‘OK’ ndiko alikopata mkwanja huo na kuanzisha miradi hiyo mikubwa?
Kama ndiyo, kwa nini memba wenzake ndani ya kundi hilo hawana maendeleo makubwa kama yeye?
Kazi
nyingine ya Masanja ni muziki wa Injili ambapo kwa sasa albamu yake ya
Hakuna Jipya iko sokoni. Je, albamu hiyo na shoo anazofanya zinaweza
kuwa chanzo cha utajiri huo?
Lakini pia Masanja ni mchungaji
ambaye anahudumu katika Kanisa la Evangelist Assemblies of God Tanzania
(EAGT) ‘Mito ya Baraka’ lilicho chini ya Askofu Bruno Mwakiborwa. Je,
mshahara anaoupata kutokana na huduma hiyo unaweza kuwa chanzo cha
mapato yake?
paparazi alikutaka kupasua kichwa,
juzi lilimsaka Masanja kwa simu na kumhoji juu ya mali zake ambapo
kwanza alithibitisha kweli anamiliki mali hizo na nyingine ambazo
hakupenda kuzitaja.
“Ni kweli nina nyumba tatu hapa
mjini, kampuni ya ulinzi na mashamba ya mpunga eka 50 nyumbani Mbarali,
Mbeya. Kuhusu magari pia ni kweli kabisa. Mimi ni mtumishi sitakiwi
kusema uongo,” alisema Masanja.
paparazi: Lakini mbona utajiri wako umekuwa wa haraka sana mtumishi, vipi vyanzo vya mapato yako?
MASANJA: Orijino Komedi ndiyo chanzo cha vyote... pale ndipo kwenye koki.
paparazi: Kuchekesha tu kaka? Au kwenye muziki wa Injili pia kunalipa?
MASANJA:
Injili na uchungaji ninaotumika kanisani ni huduma kaka, sitegemei
mapato kutoka huko. Nipo kwa ajili ya kulisha kondoo wa Bwana.
paparazi: Wasanii wenzako wa Orijino Komedi wanachukuaje mafanikio yako?
MASANJA:
Wanafurahia, wananiunga mkono maana ni sehemu ya mafanikio yao pia.
Sisi tunaishi kama ndugu. Kwa hiyo kuna baadhi ya aidia ni zao, hivyo
wanajivunia sana mafanikio yangu.
Tuituitui! Simu ikakatika! Risasi likaenda mtamboni.

No comments:

Post a Comment