Wednesday, 2 April 2014

BARUA NZITO: DADA MAINDA, HEBU ONA AIBU BASI!!



BARUA NZITO: DADA MAINDA, HEBU ONA AIBU BASI!!








Staa wa Bongo Muvi, Ruth Suka ‘Mainda’.
KWAKO,
Ruth Suka ‘Mainda’, zamani uliitwa
Mwanaidi kabla ya kungia kwenye ‘njia hii’. Ni imani yangu unaendelea
vyema na shughuli zako za kila siku. Kwanza nakupa pole kwa habari
iliyotoka katika gazeti damu moja na hili, Ijumaa Wikienda, toleo la
Jumatatu iliyopita (achana na la juzi).
Habari hiyo ilikuwa na kichwa kinachosomeka: MADAI MAZITO... MAINDA MJAMZITO!Inawezekana habari hiyo haikukufurahisha kutokana na maneno uliyoandika kwenye mitandao ya kijamii ukikanusha vikali.

Ulichokuwa unajaribu kufanya ni
kutudhalilisha sisi kama wanataaluma ya habari tuonekane ni wazushi,
hatujui miiko ya kazi yetu. Nilipitia ujumbe wako mstari kwa mstari,
nikagundua mahali palipokukwaza.
Lakini Mainda, hebu nikuulize kitu:
kuwa na mimba ni kosa? Ni kashfa? Isitoshe, gazeti  lilieleza juu ya
madai hayo na kuyafuatilia.
Habari ilizingatia kanuni zote,
ikiwemo kukupa haki ya kutoa ufafanuzi. Siku kadhaa nyuma, uliwahi
kueleza mwenyewe kuwa kutokana na chango lililokuwa linakusumbua,
ulishauriwa kupata mimba ili uwe sawa. Hapo tulitunga sisi?
Mwisho wa waraka wako, nikapata picha
ya tofauti. Hasa pale ulipokanusha kuwa eti umezushiwa kuwa uliwahi
kuchoropoa mimba! Nani angejua siri zako kama usingesema?
Nafikiri
tatizo siyo mimba, ila kinachoonekana kuwa tatizo kwako ni Ray (Vincent
Kigosi) kuhusishwa katika habari ile. Tatizo ni nini? Si wewe mwenyewe
ulisema uliwahi kutoa mimba ya Ray?
Ulizungumza mbele ya wahariri huku vyombo vya kurekodia vikiwa mbele yako, iweje leo unakanusha?

Ngoja ninukuu sehemu ya habari hiyo
ambayo pengine ndiyo imekuchefua: ‘Kama kweli Mainda atakuwa mjamzito
basi itakuwa ni mimba ya pili baada ya kukiri kuwa aliwahi kuchoropoa ya
aliyekuwa mtu wake, mwigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ ambaye
walishamwagana’.
Kuna kosa hapo? Maana umelalamika ni
kwa nini unahusishwa na mtu ambaye huna uhusiano naye. Sikia Mainda,
huwezi kubadili historia. Ray ni sehemu ya historia ya maisha yako,
maana umekiri mwenyewe kuwa aliwahi kuwa mpenzi wako.
Umesema mwenyewe kuwa, uliwahi kupata mimba yake, lakini baadaye ukaichomoa. Nikukumbushe? Angalia chini hapa...
Risasi:
Unauzungumziaje uhusiano wako na Ray? Namaanisha ni nini hasa ambacho
hakitaweza kufutika kirahisi katika kumbukumbu zako?
Mainda: Daah! (anavuta pumzi ndefu
kisha anazishusha) nilimpenda sana Ray. Ilifikia hatua nikapata mimba
yake. Mapenzi yetu yakaongezeka lakini kwa bahati mbaya ilitunga nje ya
kizazi na ilinitesa sana, tena kwa kuwa ilikuwa ni mimba ya kwanza
sikuwa nimejitambua mapema. Madaktari wakashauri niitoe, nikakubaliana
nao.
Hiyo ni sehemu ya mahojiano yako na
wahariri wa Global ambayo habari yake iliandikwa na Mwandishi Wetu,
ikatoka katika gazeti hili ikiwa na kichwa: MAINDA: NIMETOA MIMBA YA
RAY!


Nani anadanganya? Sisi au wewe? Kuwa
mkweli bwana. Heshima yako kama kioo cha jamii ni kubwa. Si jambo jema
kuwashushia heshima watu ambao wamechangia kukupa heshima!
Hebu ona aibu basi!

Yuleyule,

Mkweli daima,

.............................

Joseph Shaluwa.

No comments:

Post a Comment