Ni picha ambazo zimekua zikizungumziwa kwenye
mitandao ya kijamii na hata kwenye mitandao
mingine ya habari nchini Tanzania zikimwonyesha
mchezaji wa Yanga Mrisho Ngassa akiwa
mapenzini na mwimbaji Snura wa bongofleva.
Snura anasema mwanzo wa hizi picha kusambaa
ni baada ya kupoteza simu yake, namnukuu
akisema ‘Millard hizo picha hazina uhusiano
wowote unaounganishwa kimapenzi kati yangu na
Ngassa ila ni sehemu ya vipande vya movie yangu
inaitwa ‘Majanga’ ambayo nimeanza kuifanya na
Ngassa amecheza ndani yake kwenye scene za
mapenzi, yani Snura kwenye movie amecheza
kama binti mrembo anaerukiarukia Wanaume’
‘Simu yangu ilipotea ndio maana wamezipata hizo
picha, wakati tunashoot tulikua tunapigapiga tu
hayo mapicha, mi sikuwa nataka kuzitoa kabisa
manake movie yenyewe bado naifanya nusunusu
kutokana na kukosa muda, hii ishu imeniletea sana
matatizo manake mwingine anakua haamini
unachokiongea na hakuna kitu kinauma kama
kuongea ukweli alafu mtu anasema unadanganya’
– Snura
Kwa kumalizia Snura anasema ‘Ngassa alinipiga
muda mfupi tu baada ya picha kuanza kusambaa
akauliza mbona hizi picha zinasambaa hivi Snura?
nikamwambia usinielewe tofauti babaangu kwa
sababu mimi mwenyewe sikutaka zitoke, picha
nilizopiga nyinginyingi tu wakati tunatengeneza
movie ila naona watu wameona hizi ndio nzuri kwa
skendo’..
Wednesday, 27 November 2013
UKWELI WA ISHU YA SNURA NA MRISHO NGASSA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment