Ni ajabu kuwa watu wengine katu hawawezi kuona
kile walichonacho; wakionacho pekee ni kile
wasichonacho, ni kile wanachokosa.
Wakati mwingine inahitaji roho ya paka kuendelea na
nguvu kufanya kile unachofanya wakati watu
wanaendelea kukudhihaki.
Zaidi ya muziki, kuna kitu gani kizuri kinachoitangaza
Tanzania nje ya nchi kwa sasa? Tusaidiane
kuuchambua ukweli huu unaomezeka kwa fundo la
mate la kulazimisha kinywani.
Ni lini mara ya mwisho Tanzania imefanya vizuri
kimataifa kwenye soka? Hakuna habari njema zaidi ya
kuendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu, iwe
kwetu hata nje.
Ni lini mara ya mwisho mkimbiaji riadha wa
Tanzania ameshinda mbio zozote za kimataifa?
Hakuna.
Kimichezo ni kama bado tumeendelea kuwa
wasindikizaji tu. Au umesahau jinsi Selemani Kidunda
alivyodundwa mwaka 2012 kwenye mashindano ya
Olimpiki? Ukitoa mwaka 2005 pale Nancy Sumari
alipokuwa Miss World Afrika, ni lini mrembo yeyote
wa Tanzania amewahi kuiletea sifa nchi yetu?
Ni nini hasa kinachoweza kuifanya Tanzania
kuipeperusha bendera yake kwenye jukwaa la
kimataifa kwa sifa nzuri? Au labda kipindi hiki
tumegeuka kuwa mabingwa wa biashara ya dawa za
kulevya na Watanzania ndio wamekuwa vinara wa
kukamatwa kila kukicha nchi za nje.
Angekuwepo Kanumba na zile jitihada alizokuwa
akizifanya, labda tungesema Bongo Movies ilikuwa
inaelekea kuwa njia nzuri ya kutupa heshima pia.
Lakini tangu afariki, hakuna mwingine anayeonesha
dalili za kufanya kile alichokuwa anakifanya na filamu
zetu zimeendelea kuwa za nyumbani pekee.
Hivyo, ukiangalia kwa mifano hiyo, ni muziki pekee
wenye matumaini ya kuliongezea ‘kiki’ jina la nchi
yetu kwenye ‘google search’. Lakini kama muziki ndio
unaonekana kuwa kitu muhimu kinachoitangaza
Tanzania, mbona wale wanaofanya vizuri kwa
kutuwakilisha nje tunawabeza?
Mpaka muda huu, ukimtoa AY, hakuna msanii
mwingine wa Tanzania anayevuma kimataifa kama
alivyo Diamond Platnumz. Amefanikiwa kiasi cha hivi
karibuni kumshirikisha staa wa Nigeria Davido kwenye
remix ya wimbo wake, Number 1 na video
iliyogharimu si chini ya dola 25,000 iko mbioni kutoka.
Amekuwa ni msanii mwenye kujituma, kutake risk na
kutochoka kujaribu kufanya kile wengi wamekuwa
wakikiogopa kufanya. Lakini bado kuna watu wengi
hawaoni anachokifanya na wameendelea kumkejeli.
Wanasema hakuna binadamu aliye mkamilifu, lakini
pamoja na kwamba unaweza kumnyonga mnyonge, ni
vyema kukumbuka kumpa haki yake. Ni asili ya
mwanadamu kuumizwa na mafanikio ya mtu
mwingine, na ndio kinachotokea kwa Diamond.
Ameendelea kufanikiwa kiasi mpaka anaanza
kuwakera wengine. Si kosa kuchukia maisha na
scandal zake, lakini si kosa pia kusifia kile
anachoifanyia Tanzania.
Siwezi kubisha kuwa, mimi binafsi Diamond amekuwa
akinikera kwa baadhi ya vitu (kama mimi pia
ninavyokera wakati mwingine, nobody is perfect)
lakini siwezi kuukataa ukweli kwamba Diamond ana
kipaji, anajituma, anapendwa na anajua
anachokifanya. Kubwa zaidi ya hayo, Diamond
amekuwa mstari wa mbele kuitangaza Tanzania na
Kiswahili pia lugha yetu adhimu kupitia nyimbo yake.
Ni jambo tunalolihitaji Watanzania kuwa na msanii
wetu mkubwa mwenye hadhi na mafanikio kama ya P-
Square. Pengine tusisahau ukweli huu kwamba ni
mapenzi watakayoyapata wasanii wetu hapa nyumbani
pekee ndio yatakayowapata mafanikio zaidi.
Utafanikiwa vipi nje ya nchi kama nyumbani
wanahate?
P-Square walikiri kuwa ni Wanaijeria wenyewe ndio
waliowafanya wawe wakubwa kiasi hicho na
kuwataka Watanzania pia wafanye hivyo kwa wasanii
wao.
“Wanamuziki wenu wanafanya kile kile sisi
tunachokifanya, mnaowaona watu hawa hapa?
Mnaweza kuwafanya wawe wakubwa kuliko P-Square.
Ukweli ni kwamba tunapromote muziki wa Africa.
Waafrika huu ni muda wetu. Wamarekani nasema
wanaogopa sasa hivi.
Ningependa kuona mnaweka jitihada zaidi kwa
wanamuziki wenu hapa. Nataka kuwaona wanakuja
Nigeria na kuongoza concert. Hakuna mtu anayeza
kufanya hivyo vizuri isipokuwa ninyi,” alisema Peter
kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar,
siku moja kabla ya show yao ya Leaders Club.
Diamond ni binadamu kama wengine. Anaumia
anapoona anakosolewa hata katika mambo yasiyokuwa
ya msingi. Kwa mfano hivi karibuni alihudhuria
harusi ya Peter wa P-Square jijini Lagos, Nigeria.
Inasemekana kuwa mwaliko huo aliupata kutokana na
kuwa karibu na Iyanya aliyemshirikisha kwenye
wimbo wake. Katika harusi hiyo, Diamond alipiga
picha na Peter na kuiweka Instagram..
Wednesday, 27 November 2013
KWANINI BAADHI YA WATU WANACHUKIA MAFANIKIO YA DIAMOND PLATNUMZ??
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment