Wednesday, 27 November 2013

Diamond akiwa na Peter Okoye


Inasemekana kuwa P-Square walipokuja Tanzania
waliulizwa kama wanamfahamu Diamond na kwamba
wakasema lahashaa, hawamjui. Cha ajabu suala hilo
limegeuka gumzo na watu wamekuwa wakimkejeli
Diamond kuwa kaumbuka. Jamani, kwani ni lazima
Peter awe anamfahamu Diamond?
Amfahamu kwa njia ipi? P-Square ni wasanii namba
moja Afrika, unaweza kufikiria ni wasanii wangapi
Afrika wenye level za Diamond wanaotaka walau
kupata contacts zao? Ni wengi mno, na unadhani ni
rahisi kuwapata? Na hata hivyo, wote tunajua harusi
zinavyokuwa na pilikapilika, unahisi Peter alikuwa na
uwezo wa kumkariri kila mtu aliyehudhuria harusi
yake. Unadhani ilikuwa rahisi kwa Diamond
kujitambulisha vizuri kwa Peter kiasi cha kumfanya
amkumbuke? Ni ngumu.
Haya, jana Rais Jakaya Kikwete alisema kwenye
semina ya fursa kuwa Diamond ni msanii mwenye
nidhamu ya kazi ama kwa Kiingereza ni ‘work ethic’.
Wengi wemepingana na kauli ya mkuu wa nchi kwa
kuona kampa Diamond sifa asiyostahili.
Lakini kwanza tujiulize, ni nini maana na nidhamu ya
kazi? Ni thamani iendanayo na uchapakazi, umakini
na kujituma. Nidhamu ya kazi ni pamoja na kuwa
‘reliable’ kuwa na uwezo wa kuanzisha vitu na
kutafuta ujuzi mpya. Kwa tafsiri hiyo, unaweza
kumpiga Rais Kikwete kwa kusema Diamond ana
nidhamu ya kazi? Maisha binafsi, scandal na
ubinadamu, havina uhusiano wowote na nidhamu ya
kazi.
Sibishi kuwa wakati mwingine maisha ya Diamond
hasa ya kimapenzi yamekuwa na sifa mbaya, lakini
hiyo haiuondoi ukweli kuwa, ni msanii anayejituma
sana. Tumkosoe pale ambapo anastahili kukosolewa na
pia tumpe sifa pale anapostahili kusifiwa lakini sio
kuhate pasipo na sababu za msingi.
Labda wengine wanamchukia kwasababu hupenda
‘kubrag’ kwa kupost picha za dola, cheni, saa, nguo
ama viatu vya thamani kwenye Instagram? Kama
ndivyo, basi nakumbuka kauli ya Joh Makini
aliyoniambia hivi karibuni kuwa watu wengine
wamekuwa na chuki kwa wenzao waliofanikiwa
kwakuwa maisha kwao ni magumu.
“Ukichungumza kitu gani kinachosababisha haya
mambo yote, utagundua kuwa watu wengi hawawezi
kukidhi gharama za maisha jinsi ambavyo zinapanda.
Huo ni mwanzo wa kuwekeana chuki kwenye kazi au
mtu anakuwa anakusikia wewe kwa kitu ambacho
unafanya, utagundua ni kwamba kwasababu yeye
anashindwa kulipia bili zake za kila siku, hata kama
hausikika kwa namna moja au nyingine kwenye kipato
chake lakini unakuta tu mtu anakuwa na chuki
binafsi. Tatizo bei ya mkaa,” alisema Joh.
Ina make sense hata hivyo. Unapogundua kuwa
huduma ya maji imekatwa nyumbani na huna hela ya
kulipa au mchana unapita mkavu bila ‘kupiga menu’
halafu kwenye Instagram unaona picha ya Diamond
akiwa na buruguntu la dola za kimarekani, lazima
kiroho kiume na unajikuta unageuka hater ghafla!!!
Tatizo ni bei ya Mkaa.

No comments:

Post a Comment