WAKATI Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) kikimwandikia Mbunge wa Kigoma Kaskazini,
Zitto Kabwe barua ya kumtaka ajieleze dhidi ya tuhuma
zinazomkabili, yeye ameamua kukimbilia polisi akimshitaki
mmoja wa viongozi wenzake.
Habari za kuaminika zimedai kuwa Zitto ambaye hivi
karibuni alivuliwa cheo chake cha unaibu katibu mkuu wa
CHADEMA, inadaiwa amefungua mashitaka polisi
akimtuhumu Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Dar es Salaam,
Henry Kileo kwa madai ya kusambaza waraka katika
mitandao ya kijamii.
Akithibitisha tukio hilo, wakili wa Kileo, Peter Kibatara,
alisema kuwa mteja wake amemriwa kufika makao makuu
ya Jeshi la Polisi leo Jumatano saa nane mchana na
kuonana na mmoja wa maofisa wa juu wa jeshi hilo,
aliyetajwa kwa jina moja tu la Mbutta, kufuatia mashitaka
yaliyofunguliwa na Zitto dhidi yake.
Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wetu, Kileo
alikiri kuitwa polisi, ingawa alidai hajui ni waraka gani
anaotuhumiwa kuusambaza unaomchafua Zitto.
“Kwa kweli sijui hata mimi ni waraka gani, ingawa hivi
karibuni kulikuwa na waraka wa siri uliodaiwa kutoka
CHADEMA, na ambao ulijaa tuhuma za usaliti. Lakini huo
tuliishaukana siku nyingi. Labda kuna mwingine,” alisema
Kileo.
Zitto kutwa nzima ya jana hakuweza kupatikana kwa njia
ya simu kufafanua mashitaka aliyofungua polisi. Simu
zake zote za kiganjani zilikuwa zimezimwa.
-Tanzania daima......
Wednesday, 27 November 2013
KUMEKUCHA.!!.CHADEMA bado hali ni tete...Zitto Kabwe amburuza polisi katibu wa chama hicho akimtuhumu kuusambaza waraka wa siri uliomchafua...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment