Muigizaji na mwimbaji nchini Kitale yuko Tanga alipoenda
kuhudhuria Dua ya kumuombea marehemu Sharo Milionea
ikiwa ni mwaka mmoja tangu afariki dunia kwa ajali mbaya
ya gari.
Kitale ambaye ndiye msanii pekee aliyefika Tanga siku ya
jana amesema kuwa amejifunza mambo mengi katika
msiba wa rafiki yake Sharo Milionea, ikiwa ni pamoja na
misiba ya wasanii wengine waliotangulia mbele ya haki,
Kanumba na Sajuki.
Akiongea kwa njia ya simu na Edson Mkisi katika kipindi
cha Hatua Tatu cha 100.5 Times Fm, Kitale amesema
kutokana na funzo alilopata amempa ujumbe mama yake ili
kwamba pindi atakapotangulia mbele ya haki mambo hayo
yasijirudie kwake.
“Nimejifunza vitu vingi na nimejua marafiki walio wema na
marafiki wasio wema. Ina maana kwamba kuna marafiki
wanafiki na marafiki wasio wanafiki. Amesema Kitale.
“Kuna vitu vingi nimejifunza baada ya kuondoka marehemu
Steven Kanumba, nimejifunza baada ya kifo cha Sharo
Milionea, na nimejifunza baada ya kifo cha Sajuki.
Nimejifunza vitu vingi sana sana sana.” Amesisitiza.
“Ina maana hata mimi kama ntatangulia kuna mambo
ambayo nimeshamweleza mama yangu na nimeshaieleza
familia yangu, nafikiri hakitakuja kutokea kama
kilichotokea kwa wenzangu. Nimejifunza vitu vingi hasa
ukiwa msanii...” Kitale ameiambia Hatua Tatu.
Hata hivyo Kitale alikataa kueleza ujumbe huo na kudai
kuwa ni siri kati yake na familia yake kwa kuwa hafahamu
nani atatangulia kati yake na wazazi wake.
Kitale amewashauri wasanii kumkumbuka Mungu wakati
wanapoendelea na shughuli zao na ndio sababu watu
wengi wanaamini kuwa asilimia kubwa ya wasanii ni
‘Freemason’, na kwamba hiyo inatokana na kitendo cha
wasanii hao kumsahamu Mungu wao.
Siku kama ya leo mwaka uliopita (November 27,2012) ndio
siku ambayo marehemu Sharo Milionea alizikwa huko
Tanga.
Apumzike kwa Amani........
Wednesday, 27 November 2013
Kitale: nimejifunza mengi kwenye kifo cha Sharo Milionea, nimeacha ujumbe kwa mama yangu nikifa yasijirudie kwangu.....
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment