MZEE mmoja kigogo wa biashara ya kuuza mbao jijini Dar
es Salaam, hivi karibuni alinaswa kitandani ndani ya
chumba akiwa na mrembo aliyedaiwa ni mwanafunzi wa
shule moja ya msingi Tegeta Wazo, Dar.Mfanyabiashara
huyo aliyetajwa kwa jina moja la Kyando, anasemekana
amekuwa na ukaribu na denti huyo anayeitwa Fatty kwa
siku nyingi, kitu ambacho kiliwapa maswali baadhi ya
majirani wa nyumbani kwa msichana huyo.
Katika harakati za kuchunguza ukaribu wa msichana huyo
na mtu mzima huyo, mama mdogo wa binti aligundua kuwa
wawili hao wana ukaribu usiofaa.
Ikaelezwa kuwa, mama mdogo wa mwanafunzi huyo
aliponyetishiwa ishu hiyo, aliandaa mtego unaofyatuka kwa
kasi kuliko ule wa panya ili kumtia mikononi mzee huyo
mpenda kukaa na watoto wa wenzake.
“Mtego mkali uliandaliwa, siku ya siku, ma mdogo huyo
alijifanya anakwenda mbali na nyumbani, binti akaona
dakika tisini za mchezo lazima aibuke kidedea wa mahaba,
alimwita mwanaume huyo na kumkaribisha chumbani,
kumbe arobaini zao zilikuwa zimetimia,” kilisema chanzo.
Mashuhuda wa sakata hilo walidai kuwa mama mdogo na
watu wengine waliwanasa wawili hao wakiwa juu ya
kitanda kama walivyozaliwa, bila kufafanua walichokuwa
wakikifanya.
Ili kushika ushahidi mkononi, mama mdogo wa binti huyo
na wapambe wake walipiga picha za mnato na za video
kisha wakaanza kumuuliza maswali ‘mlalamikiwa’ ambaye
inaaminika ni mume wa mtu.
Haikuelezwa wazi ni maswali ya aina gani aliyokuwa
akiulizwa lakini inadaiwa yalihusu historia ya kujuana
kwao.
Aidha, inadaiwa kuwa mama mdogo huyo alitaka
kumtwanga ndoa ya mkeka mfanyabiashara huyo lakini
chondechonde zake nyingi zilimwokoa na kuahidi kurejea
siku inayofuata kwa ajili ya kukata mshiko wa fidia baada
ya kuambiwa binti huyo bado anasoma na shuleni
kulilipwa fedha nyingi.
Habari nyingine zinadai kuwa wawili hao walifahamiana
miezi kadhaa nyuma kupitia lifti ya gari ambayo
mshitakiwa alimpa mrembo huyo maeneo ya Boko, jijini
Dar....
Wednesday, 27 November 2013
FUMANIZI!!! KIGOGO AKAMWATWA AKIVUNJA AMRI YA SITA NA MWANAFUNZI BILA AIBU..................CHEKI HAPA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment