Chama cha demokrasia na maendeleo Chadema
kimewaandikia barua za kuwavua rasmi nyadhifa za
uongozi aliyekuwa naibu katibu mkuu Mh. Zitto Kabwe na
wenzie sambamba na kupewa siku kumi na nne za
kujieleza kwa nini wasivuliwe uanachama kufuatia waraka
wa siri walioundika na kukamatwa hivi karibuni.
Mkurugenzi wa habari na uenezi Chadema Mh. John
Mnyika amesema barua hizo zilizoainisha makosa kumi na
moja ya kukiuka katiba na itifaki za chama hicho
zitawataka wahusika kujieleze kwa maandishi na baadae
mbele ya chama kwa nini wasifukuzwe na kuvuliwa
uwanachama kufuatia waraka waliouandaa uliosemekana
ulilenga kikupindua chama hicho.
Aidha Mh. Mnyika ameongeza kuwa waraka uliochapisha
kwenye baadhi ya magazeti na mitandao mbalimbali ya
kijamii sio ule uliowahukumu wahusika hao na kuwaomba
watanzania na wafuasi wa chama hicho kutoutilia maanani
waraka huo na siku itakapobidi kuutoa waraka husika
watafanya hivyo.
Awali mwanasheria mkuu wa chama hicho Mh. Tundu
Lissu akizungumzia mkutano uliofanywa na Mh. Zitto na
wenzie licha ya kukata kusema hatua zitazozochukuliwa
pindi watakaposhindwa kutimiza mashati waliyoyaweka
amesema mkutano huo ulilenga kupoteza lengo kuu la
kuvuliwa madaraka na kuwa kilichowafukuza ni mkakati
wao wa siri uliolenga kukipindua chama hicho na si
vinginevyo.........
Wednesday, 27 November 2013
VIDEO: Msikilize Tundu Lissu akimsomea makosa 11 Zitto Kabwe ya kupanga kukipindua chama cha CHADEMA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment