Monday, 25 November 2013

DARASA LA WAKUBWA..!MAMBO YA KUMFANYIA MSICHANA ILI UWEZE KUMTEKA ASIKUACHE HATA KAMA HUJAMTONGOZA......

Habari yako ndugu msomaji? Natumaini u mzima na
mwenye afya njema.
1. KILA siku usisahau kumsifia kwa kumwambia ni
kiasi gani alivyo mzuri. Kumbuka kila msichana
anapenda kusifiwa hivyo unapomuambia yeye ni
mzuri anaona una mthamini kuliko msichana yeyote
awaye.
2. Wakati wowote ukipata nafasi muandikie barua au
msg kwenye simu mueleze hisia zako kiasi gani
unampenda. Kumbuka wasichana hupenda kusikia
zaidi kutoka kwa wapenzi wao ni kiasi gani
wanapendwa. Haitakiwi iwe tu katika kipindi cha siku
ya wapendanao ndio umuoneshe kuwa unampenda.
Muoneshe msichana ni kiasi gani yeye ni muhimu
sana kwako.
3. Busu la ghafla na kumshika mkono wakati
mkitembea pamoja itamfanya yeye kujisikia raha zaidi.
Na wakati mwingine msuprise kwa kumtembelea mara
kwa mara hi humfanya akuone wewe ni mtu muhimu
pale usipokuwa naye karibu na kumfanya kukuhitaji
zaidi ukiwa naye mbali
4. Tambua mahitaji yake. Uwe msaada kwake kipindi
ambacho mpenzi wako amekasirika kuwa pale kwa
ajili yake na ukimpooza kwa sauti ya upole na
mahaba. Utashangazwa sana na kiasi gani msaada huo
umeleta mabadiliko kwake. Hakikisha unamsaidia
katika shida zake hapa ndipo kuna tatizo kwa
wavulana wengi. Mapenzi si pesa lakini kuna kipindi
ambacho pesa huitajika kulinda penzi lako. Si
msichana anapokuomba pesa ina maana ana nia ya
kukuchuna au amekupendea pesa kuna shida nyingine
inabidi akuombe wewe tena kwa kukupima kama
utakuwa tayari kumsaidia.
5. Mchukue mpenzi wako out mara nyingine itamfanya
ajisikie furaha sana kwa sababu wasichana hupenda
enjoyment na boyfriend zao. Hii haitamfanya mpenzi
wako tu kuwa na furaha bali itawafanya nyie kwa
pamoja kujuana na kufahamiana zaidi.
6. Kuwa muwazi kwake usimfiche jambo
linalokuhusu. Msichana hupenda kutoa ushauri kwa
mtu ampendaye hivyo unapokuwa muwazi atajisikia
kuthaminiwa nawe na kukuona umemuamini
7. Ukijiona upo busy sana usithubutu kuacha japo
kumpigia simu mara mbili kwa siku hata kama
ukishindwa kumpigia wakati upo ofisini darasani au
kwingineko hakikisha unapopata nafasi japo ujumbe
mfupi wa kumwambia unampenda.
8. Mkumbatie mara kwa mara katika tukio la
kumbatizi kuna jambo kubwa sana hutokea. Si kwake
tu hata kwako mvulana. Hali ya joto lenu huwaweka
pamoja kifikra hata pale msipokuwa pamoja.
9. Epuka maugomvi na hasira za mara kwa mara
ukiwa nae. Mwanamke hupenda ustaarabu kwa mtu
ambaye yupo serious naye hivyo ukionesha hasira
kabla hata hujamtongoza unaweza ukamkosa
msichana hivihivi wasichana huwaogopa wavulana
wenye hasira na wagomvi kwa sababu hupenda
kubembelezwa.
10. Mdekeze. Msichana anapenda kudeka anaenda
kudeka sana na kubembelezwa sana hivyo mvulana
ukidekewa usikasirike eti huyu msichana kazidi wewe
ndio wakati wako wa kumuonesha msuchana wako
unampenda mdekeze mpaka aone aibu kudeka siku
nyingine. Wasichana wameumbwa kwa jili ya
wavulana ndio maana hudeka hii ndiyo silaha pekee
na ya mwisho kumpata msichana hata kamasi wako ni
wa rafiki yako unaweza ukatumia silaha hii kumpora
msichana huyo kwa mwenzio usipojua kudekeza
utaachwa pia

No comments:

Post a Comment