LICHA ya kuwa na kichanga, staa wa filamu za Kibongo,
Flora Festus Mvungi amenaswa usiku wa manane ‘akila
bata’ jambo lililozua mshangao kwa wadau waliokuwepo
eneo hilo.
Msanii huyo alinaswa na ‘kiranja’ wa gazeti hili hivi
karibuni ndani ya Ukumbi wa Vijana Social, Kinondoni jijini
Dar kulipokuwa na tamasha la vipaji, alipofotolewa picha,
aling’aka!.
“Sitaki picha bwana, wewe hujui kama nimetoroka usiku
huu kuwa hapa! Naomba ufute hizo picha tafadhali,
usiniudhi bwana,” alisema Mvungi huku akikwepa miale ya
kamera.
No comments:
Post a Comment