Mwigizaji
wa Kundi la Vituko Show linalorusha vipindi vyake kwenye Runinga ya
Channel Ten, Jasmini Emiry akiwa katika hali ya sintofahamu.
Mauzauza? Katika hali ya kushangaza, mwigizaji wa Kundi la Vituko Show
linalorusha vipindi vyake kwenye Runinga ya Channel Ten, Jasmini Emiry
anadaiwa kuzua timbwili kanisani na kusababisha tafrani madhabauni
ikisemekana ni mapepo.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na mwanahabari wetu lilijiri kwenye Kanisa
Kuu la Mtakatifu Patriki mjini hapa, mwishoni mwa wiki iliyopita, wakati
wa kuaga mwili wa msanii mwenzake, Shirley Edward almaarufu Sherry
Magali.
Awali, kabla ya zoezi la kuaga mwili wa marehemu, Jasmini, akiwa benchi
la mwisho nyuma sambamba na wasanii wenzake akiwemo Asha Boko na mke wa
Mzee Majuto, Rehema Majuto, alionekana mwenye simanzi kupita kiasi.
Ulipofika muda wa kuaga, Jasmini alipomaliza kulizunguka jeneza
lililobeba mwili wa Sherry mbele ya madhabahu, alianguka na kuanza
kurusha mateke kama pundahuku akizungumza maneno yasiyoeleweka.
Baada ya kuona hivyo, baadhi ya wasanii wa Bongo Movies mjini hapa
wakiongozwa na Chediel Senzighe walimbeba msanii huyo na kumtoa nje
hukuakiwapiga na kuzua tafrani ya aina yake.
No comments:
Post a Comment