Makasisi wanaoshiriki katika mkutano wa maaskofu wanaangazia masuala ya
mafunzo ya kanisa katoliki kwa familia ,wametoa mwito kwa kanisa hilo
duniani kuwachukulia watu wenye mapenzi ya jinsia moja kwa usawa
Kauli hii inakuja baada ya Maaskofu kuandika ripoti wakati wa mkutano wa
synodi ukiendelea huko Vatican na kusema kuwa wapenzi wa jinsia moja
wana zawadi na viwango vya kutoa kwenye jumuiya za kikristo hii ikiwa ni
ripoti iliyotolewa mapema wiki hii.
Ripoti hiyo haitoi changamoto yoyote kwa msimamo wa muda mrefu wa kanisa
hilo juu ya kupinga ndoa za jinsia moja,lakini baadhi ya vikundi vya
kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja wanachukulia kauli hiyo kuwa ya
mafanikio makubwa kwa jamii zao.
Na moja ya makundi yenye kushikilia msimamo mkali kikanisa wametupilia mbali ripoti hiyo na kuuita ya kisaliti.
Zaidi ya maaskofu 200 wa kanisa katoliki wanakutana kwenye mkutano wa
synodi tangu mapema mwezi huu,katika mkutano huo ni papa Francis
aliyetoa mwito wa kujadili masuala ya utoaji wa mimba,vidonge vya uzazi
wa mpango,mapenzi ya jinsia moja na talaka.
Papa Francis amewataka viongozi wa juu wa kanisa hilo kuzingatia Zaidi
suala la wapenzi wa jinsia moja chanya kuliko kuwa kinza na amefanikiwa
kuwateka maaskofu wanaohudhuria mkutano huo wa sinodi.
Mwaka uliopita katika ripoti aliyo itoa papa Francis kuhusiana na
mwenendo wa kanisa katoliki kuwa waumini walio wengi waliliacha mkono
kanisa hilo kutokana na mafunzo yahusianayo na ngono na dawa za uzazi wa
mpango.
Papa huyo anazichukulia ndoa hizo za jinsia moja kama zisizo na
utaratibu akiinukuu ripoti ya kanisa katoliki iliyochapishwa mwaka
1986,wakati Papa Francis alipokua mshauri mkuu wa masuala ya teolojia ya
kanisa katoliki wa hayati papa John Paul wa pili.
Nguvu kubwa ya vikundi vya kutetea haki za watu wenye mapenzi ya jinsia
moja ni juu ya kauli ya papa Francia aliyoitoa mwishoni mwa mwaka wa
jana alipokuwa kwenye kambi ya vijana wa kanisa hilo huko Rio de Jeneiro
alitoa kauli kua kama mtu anamtafuta Mungu na ana nia njema ,yeye ni
nani wa kuhoji?
Papa Francis anaingia katika historia ya kanisa katoliki ulimwenguni
kutumia jina (hasha kum si matusi) WASENGE hadharani kuliko kutumia neno
wapenzi wa jinsia moja.
No comments:
Post a Comment